Hii
ndio picha ambayo imesambaa kwenye mitandao mingi ya msichana
anesemekana ni Fatma aka Brown Berry wa Ilala Dar es Salaam ambae
amehukumiwa kunyongwa huko egypt baada ya kukamatwa na unga.
Wednesday, June 05, 2013
MR NICE APIGWA CHINI NA LABEL ALIYOKUA AKIFANYA NAYO KAZI KENYA, KISA NI MVIVU.
GrandPa
Records Ya Kenya Imevunja Mkataba Wake Wa kazi na Msanii Mr Nice kutoka
Tanzania Baada ya miezi michache ya kufanya nae kazi. Fahamu Mr Nice
alipewa mkataba na GrandPa Records huku akijua kuwa ana mkataba mwingine
Tanzania na Producer Lamar. GrandPa Wamesema Mr Nice Ni Msanii Mvivu na
Asiye toa ushirikiano kwenye kazi kabisa ndio maana wameamua Kuvunja
mkataba wake. Hii Ni Post ya FaceBook Ya GrandPa Records. Bado Taarifa
Zina Kuja Kaa Na Mimi Utaiskia Interview Yao Hapa Soon
KESI DHIDI YA RUTO KUHAMISHIWA KENYA AU TANZANIA
Nairobi, Kenya.
Kesi inayomkabili makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto kwenye
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huenda ikahamishiwa nchini
Tanzani au Kenya.
Hiyo inatokana na uamuzi unaotajwa kufikiwa
na majaji wa ICC ambao wametoa mapendekezo wakimtaka Rais wa ICC
aangalie umuhimu na kutoa ruhusa ya kesi hiyo kusikiliziwa nchini Kenya
au kama ikishindikana basi isikiliziwe nchini Tanzania.
Uamuzi
huo unaweza pia kusababisha athari za kuichochea mahakama hiyo
kuhamisha pia kesi ya aina hiyo inayomhusu Rais Uhuru Kenyatta ambaye
pia mawakili wake wameomba kesi dhidi yake ihamishiwe nchini Kenya au
Tanzania.
Ruto pamoja na mtuhumiwa mwenzake, aliyekuwa
mtangazaji wa Redio, Joshua Arap Sang wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ya
uhalifu dhidi ya ubinadamu wakidaiwa kuhusika kuchochea vurugu za
baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 zilizosababisha vifo vya zaidi ya
watu 1,000.
Mapendekezo hayo yametokana na ombi hilo
lililotumwa Januari 24 mwaka huu ambalo lilikuwa bado likiendelea
kujadiliwa n amamlaka zinazohusika kwenye mahakama hiyo.
Februari
mwaka huu, Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Fatou Bensouda aliieleza
mahakama hiyo kwamba hana pingamizi iwapo itakubalika kesi hiyo
isikiliziwe Tanzania au Kenya.
Hata hivyo mahakama hiyo
ilieleza kuwa mapendekezo hayo bado yanaendelea kujadiliwa kwa mujibu
wa taratibu zilizowekwa na mahakama hiyo.
Hata hivyo, jana
ICC ilitoa taarifa ikisema kesi dhidi ya Ruto anayetuhumiwa kufanya
makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu itaanza Septemba 10 mwaka huu.
Taarifa hiyo imesema majaji wameamua kupanga tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo mapema zaidi kuliko ilivyopangwa awali.
Rais
Kenyatta na naibu wake wanahitajika kupandishwa kizimbani ili kujibu
mashtaka yanayowakabili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, makosa ambayo
waliyafanya wakati wa vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa Rais
wa mwaka 2007/08.
"SITANYAMAZA KUSHAMBULIWA KWANGU.NI LAZIMA JAMII IJUE"...HII NI KAULI YA KIBANDA BAADA YA KURUDU TANZANIA
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda (wa tatu kulia) akiwasili jana.
MWENYEKITI
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda amerejea chini
jana kutoka Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa na kusisitiza kwamba
hatanyamaza kuzungumzia janga la kushambuliwa kwake.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege
wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Kibanda alisema asingependa kuona
jambo hilo linamtokea mwandishi mwingine wa habari.
Kibanda,
ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd,
alikuwa akitibiwa huko baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu
wasiofahamika usiku wa Machi 5, mwaka huu.
Azam yawatupia virago Babi, Uhuru
Abdi Kassim ‘Babi’ |
Wachezaji waliotupia virago ni pamoja na Lewis Cosmas aliyejiunga na Ruvu Shooting na Abdulhalim Humoud aliyepata timu Afrika Kusini ya Jomo Cosmos. Akizungumza na gazeti hili Abdi Kassim alisema “Ni kweli mkataba wangu kuitumikia Azam umeisha ingawa walinitaka nisaini mpya, lakini tukashindwa kuafikiana. “Naamini bado nina nguvu na uwezo wa kucheza soka. Kwa hiyo niko tayari kujiunga na timu yoyote ambayo itaonyesha nia ya kunitaka.” alisema Babi aliyekipiga na klabu za Mlandege ya Zanzibar, Mtibwa Sugar, Yanga, DT Long ya Vietnam pamoja na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.Anaeleza kuwa yuko tayari kujiunga na Yanga, Mtibwa Sugar ama Coastal Union iwapo zitaonyesha kutaka kumsajili kwa ajili ya msimu ujao. Klabu ya Mtibwa iliwahi kukiri kutaka kumrejesha Babi nyumbani katika dirisha dogo la usajili Januari mwaka huu.
RONALDO AGOMA KUONGOEZA MKATABA REAL MADIRD
MSHAMBULIAJI
Cristiano Ronaldo ameziweka kiporo Manchester United na Paris
Saint-Germain baada ya kusema hataongeza Mkataba Real Madrid baada ya
2015.Real imegoma kumuuza Mreno huyo msimu huu wakati United na PSG zinabakiwa mstari wa mbele atakapotiwa sokoni.Alex
Ferguson alimuuza Ronaldo kwenda Madrid mwaka 2009, lakini nyota huyo
mwenye umri wa miaka 28 ameeleza mara kadhaa hivi karibuni kwamba hana
furaha sana katika Jiji hilo na Hispania.
Rais
wa Madrid, Florentino Perez alisema anatarajia kuona Ronaldo
akitungikia daluga zake katika klabu hiyo, lakini inaonekana atatafuta
klabu nyingine miaka miwili ijayo.
Ikiwa
Ronaldo atakuwa mkweli kwa kauli zake, ataondoka bure, kitu ambacho
Madrid hawatapenda baada ya kumsajili kwa Pauni Milioni 80.
DIAMOND ANA UTAJIRI WA ZAIDI YA BILIONI 1 ZA BONGO, NA HAYA NDIO MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU DIAMOND
2. Yupo kwenye mazungumzo na promoter wa Rwanda kufanya show moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 190.
3. Malipo ambayo hupokea kwa show zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000.
4. Tangia mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya shilingi milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa alizopangisha.
6. Wimbo Mawazo alimwandikia Jacqueline Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake.
7. Kamwambie na Mbagala alimwambia mpenzi wake aitwaye Sarah aliyemkataa (Diamond) sababu hakuwa na uwezo.
8. Ukimwona alimwandikia Wema Sepetu baada ya kumsaliti.
9. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake Papa Misifa, ilibidi amlipe shilingi milioni 18.
10. Ana timu (anayoilipa mshahara) ya watu zaidi ya 12 wakiwemo dancers, mtu wa mavazi, msaidizi wake, wapiga picha wawili nk.
ANGALIA PICHA ZA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU ALBERT MANGWEA ZAANZA KUTOLEWA.
Tuesday, June 04, 2013
Jokate aongea baada ya Diamond kukiri kuwa anajuta kumkosea na kuuvunja moyo wake
Diamond alifunguka hayo kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, kilichorushwa wiki iliyopita.
Akiongelea jinsi alivyomuumiza Jokate, Diamond alisema, “Kwasababu alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea.”
Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”
Bongo5 imewasiliana na Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli ya Diamond aliyesema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli.
“Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” amesema Jokate.
MAPOKEZI YA MANGWEA JIJI ZIMA LAZIZIMA
Gari
iliyobeba mwili wa Albert Mangwea ikisukumwa na washabiki,wapenzi ndugu
jamaa na marafiki mara baada kuanza kuondoka eneo la Eapoti hivi punde
wakielekea Muhimbili kwa taratibu nyingine,Mungu ailaze roho ya marehemu
mahali pema peponi--Amen
ANGALIA PICHA MWILI WA ALBERT MANGWEA ULIVYOWASILI DAR
Gari maalum la Kubeba Mwili wa Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Marehemu Albert Mangwea likiwa tayari kwa kubeba mwili.
Wadau
mbali mbali wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege
Julius Nyerere kwa ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Albert Mangwea
uliowasili mchana huu kutokea nchini Afrika ya Kusini.
Wadau kibao wapo uwanjani hapa hivi sasa tayari kwa kuupokea Mwili wa Marehemu Mangwea.
Rafiki kipenzi wa Marehemu Albert Mangwea,Jay Mo akihojiwa na vyombo vya habari uwanjani hapa.
MAMA NA MPENZI WAKE WAMUUA MTOTO WA MIAKA 4 ILI WAFAIDI PENZI LAO
Wakati
mwingine unaweza kudhani binadamu tunageuka kuwa wanyama, lakini huu
sio mfano tosha kwani hata wanyama wakali kama simba huwa na huruma na
huwalinda watoto wao hadi kufa, baadhi ya binadamu wamekuwa na roho ya
ukatili isiyo ya kawaida hata kwa mtoto waliyemzaa wenyewe.
Huko
Uingereza mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Magdelena Luczack na
mpenzi wake Mariusz Krezolek ambao walihamia uingereza wakitokea Poland,
wamefikishwa katika mahakama kuu mjini Birmingham wakikabiliwa na
mashtaka ya mauaji.
Watu
hao wanashtakiwa kwa kushirikiana kumuua kwa kumtesa wka vipigo
na kumyima chakula kwa makusudi mtoto Daniel aliyekuwa na umri wa
miaka minne tu,aliyefariki mwezi march mwaka jana akiwa na jeraha
kichwani.
Magdalena
ambae ni mama mzazi wa mtoto huyo anatuhumiwa kushirikiana kwa karibu
na baba wa kambo wa mtoto huyo kusababisha kifo chake wakiwa na nia ya
kutafuta amani na utulivu katika nyumba yao.
M2 THE P ANA USHAHIDI WOTE KATIKA KIFO CHA ALBERT MANGWAIR.
Na Mwandishi Wetu
MBIVU na mbichi sasa zinaweza kujulikana, kinachoombwa ni muda tu, kwani mng’amuzi halisi kuhusu kifo tata cha mwanamuziki mwenye kipaji kikubwa Bongo, Albert Mangwea ‘Ngwea’, yupo kwenye mazingira mazuri kueleza kilichotokea.
KWA NINI ANA USHAHIDI WOTE?
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mgaza Pembe ‘M2 The P’, ndiye mwenye ushahidi wote kwani aliambatana na Ngwea kila sehemu waliyotembelea mpaka nukta ya mwisho nchini Afrika Kusini.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mgaza Pembe ‘M2 The P’, ndiye mwenye ushahidi wote kwani aliambatana na Ngwea kila sehemu waliyotembelea mpaka nukta ya mwisho nchini Afrika Kusini.
M2
The P, alipatwa na matatizo sawa na marehemu Ngwea, isipokuwa mwenzake
ilifikia hatua mbaya na kupoteza maisha huku yeye akibaki mahututi
kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) katika
Hospitali ya St. Helen Joseph, jijini Johannesburg nchini humo.
Jambo la faraja ni kwamba, M2 The P yupo vizuri kwa sasa, atakaporuhusiwa kutoka, atajibu maswali mengi tata ambayo yamejitokeza tangu Ngwea alipofariki dunia Juni 28, mwaka huu, nchini humo alipokwenda kwenye shughuli zake.
Jambo la faraja ni kwamba, M2 The P yupo vizuri kwa sasa, atakaporuhusiwa kutoka, atajibu maswali mengi tata ambayo yamejitokeza tangu Ngwea alipofariki dunia Juni 28, mwaka huu, nchini humo alipokwenda kwenye shughuli zake.
JAWABU LA SUMU
Moja
ya mambo yanayozungumzwa pembeni ni kwamba kuna uwezekano mkubwa
marehemu Ngwea na M2 The P waliwekewa sumu kwenye chakula au
kupuliziwa ‘laivu’ kisha kutokea yaliyotokea, lengo likiwa kuwadhulumu
mzigo wa fedha nyingi waliokuwa nao, hivyo kupona kwa mmoja huyo ni
matakwa ya Mungu ili awe shahidi namba moja wa kifo cha Ngwea.
Subscribe to:
Posts (Atom)