Wakati
mwingine unaweza kudhani binadamu tunageuka kuwa wanyama, lakini huu
sio mfano tosha kwani hata wanyama wakali kama simba huwa na huruma na
huwalinda watoto wao hadi kufa, baadhi ya binadamu wamekuwa na roho ya
ukatili isiyo ya kawaida hata kwa mtoto waliyemzaa wenyewe.
Huko
Uingereza mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Magdelena Luczack na
mpenzi wake Mariusz Krezolek ambao walihamia uingereza wakitokea Poland,
wamefikishwa katika mahakama kuu mjini Birmingham wakikabiliwa na
mashtaka ya mauaji.
Watu
hao wanashtakiwa kwa kushirikiana kumuua kwa kumtesa wka vipigo
na kumyima chakula kwa makusudi mtoto Daniel aliyekuwa na umri wa
miaka minne tu,aliyefariki mwezi march mwaka jana akiwa na jeraha
kichwani.
Magdalena
ambae ni mama mzazi wa mtoto huyo anatuhumiwa kushirikiana kwa karibu
na baba wa kambo wa mtoto huyo kusababisha kifo chake wakiwa na nia ya
kutafuta amani na utulivu katika nyumba yao.
Mwendesha
mashtaka wa serikali Jonas Hankin ameiambia mahakama hiyo kuwa ujumbe
wa njia ya simu uliopatikana ni ushahidi tosha unaoonesha kuwa
washtakiwa walikuwa na nia ya kumuua mtoto huyo.
Amesema
katika moja ya ujumbe uliutumwa unaonesha kuwa mwezi February mama wa
mtoto huyo alimtumia mpenzi wake ujumbe uliosema, “amepoteza
fahamu(Mtoto) kwa muda kama vile nimemzamisha kwenye maji. Sasa ninapata
muda wa utulivu.”
Mwezi
October mwaka juzi kuna ujumbe ambao Krezolek ambae ndie baba wa kambo
wa mtoto Daniel, alimtumia ujumbe mama wa mtoto huyo uliosomeka,
“Mpeleke (mtoto) kwenye chumba na umfungie huko. Utakuwa na amani na
unisubirie mimi.”
Na siku nyingine alimtumia mpenzi wake ujumbe kuwa, “Tutadili na Daniel akitoka shule, hatapata muda wa kuona wadudu kabisa.”
Mwendesha
mashtaka huyo wa serikali ameiambia mahakama kuwa ushahidi mwingine wa
wazi ni kwamba inaonekana kuwa March 2 mwaka jana majira ya saa 10:34
jioni wakati mtoto huyo akiwa bado yuko hoi, mama yake alimtumia ujumbe
mpenzi wake kwa lugha ya kipolish ukimaanisha, “atapona kufikia kesho,
hakuna haja ya kujipa stress na kuita ambulance kwa kuwa hiyo ndiyo
italeta tatizo zaidi.”
Washitakiwa
hao wamekana mashtaka yote na kurudishwa rumande, kesi hiyo imepangwa
kusikilizwa na kumalizika ndani ya wiki nane, hii ikiwa ni wiki ya
kwanza.
No comments:
Post a Comment