Tume
ya Mabadiliko ya Katiba imependekeza katika rasimu ya Katiba Mpya ukomo
wa wabunge na kufutwa kwa nafasi za Viti Maalumu bungeni.
Mwenyekiti
wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Joseph Warioba alisema jana, wanapendekeza
kwamba ubunge uwe na ukomo wa vipindi vitatu vya miaka mitano, mitano
akimaanisha kwamba kipindi cha mtu kuwa mbunge hakiwezi kuvuka miaka 15.
Rasimu
hiyo ya Katiba imependekeza kutokuwapo tena kwa Viti Maalumu na badala
yake, imetaka kuwapo kwa nafasi tano za uteuzi zibaki kwa Rais ambazo
zitahusisha makundi maalumu ya watu wenye ulemavu pekee.
Jaji Warioba alisema Tume imependekeza kuwapo kwa
majimbo 25 ya uchaguzi kwa Tanzania Bara na 20 kwa Zanzibar ambayo kila moja litakuwa na wabunge wawili, mwanamke na mwanamume. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75.

huyo alisema, wananchi watakuwa na mamlaka ya kumwondoa madarakani
mbunge wao endapo hawataridhishwa na utendaji kazi wake.
Alisema
hakutakuwa na uchaguzi mdogo wa wabunge kwa wabunge watakaopitia kwenye
vyama vya siasa na badala yake jimbo litakapokuwa wazi chama
kilichokuwa kikiongoza kitateua atakayeshika wadhifa huo.
“Uchaguzi
mdogo utafanyika pindi tu aliyekuwa akiongoza alitokana na mgombea huru
(binafsi) hivyo, Tume huru ya Uchaguzi itatakiwa kuandaa uchaguzi
mdogo,” alisema Jaji Warioba.
Kuhusu
kiti cha Spika na Naibu Spika, alisema baada ya kupokea maoni na
wananchi mbalimbali, Tume hiyo imependekeza viongozi hao wasitokane na
vyama vya siasa.Alisema Tume inapendekeza Spika na Naibu Spika
wasitokane na wabunge na wasiwe viongozi wa vyama vya siasa wala
wasitokane na asasi za kiraia ambao wataidhinishwa na Bunge.
Wafurahia mapendekezo
Mkazi
wa Uhindini, Mbeya, Boniface Mwakinga alisema amefurahishwa na
mapendekezo yanayotaka kuwapo kwa ukomo wa madaraka ya wabunge.
Mfanyakazi
wa Hospitali ya Kilema, Kilimanjaro, Dennis Mfumbulwa alisema kati ya
mambo yaliyomgusa katika rasimu hiyo ni hatua ya wananchi kupewa nguvu
ya kumwondoa mbunge ambaye hawajibiki kwa wapigakura wake akisema hilo
sasa ni kitanzi kwa wabunge wababaishaji.
Mbunge
wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Shyrose Bhanji alieleza kufurahishwa
kwake na kuondolewa kwa Viti Maalumu na kupendekezwa kwa utaratibu mpya
wa kusimama na kugombea wanawake majimboni.
“Lengo la kuanzishwa Viti Maalum ilikuwa ni kuwapa upendeleo maalumu wanawake kuingia katika siasa na vyombo vya uamuzi, nadhani imefanikiwa na sasa tunapaswa kushindanishwa sisi kwa sisi,” alisema Bhanji.
MWANANCHI

No comments:
Post a Comment