Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Cecilia
Pareso.
Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Cecilia
Pareso amesema kama serikali ina lengo la kuwabana na kuwanyima haki
wapinzani, basi ni bora mfumo wa vyama vingi ukafutwa ili ifahamike
kwamba nchi ni ya chama kimoja.
Pareso ameyasema hayo jana Aprili 5,
Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia katika Mjadala wa Bajeti ya
Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2018/19 huku akidai kwamba vyama
vya upinzani vimekuwa vikionewa ikiwemo viongozi wake kukamatwa mara kwa
mara na kufunguliwa mashtaka huku wengine wakifungwa jela.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Amesema
vyama hivyo vimekuwa ni adui mwingine kwa kuwa kwa sasa vinapigwa vita
na Serikali iliyopo madarakani, kuzuiwa kufanya shughuli za siasa
majukwaani.
Pia alidai chaguzi ndogo zilizofanyika
hivi karibuni, zilikuwa ni kati ya Chadema na Jeshi la Polisi na kudai
kwamba wabunge na madiwani walinunuliwa, wakahama vyama vyao, hivyo
kukalazimika kufanyika chaguzi nyingine ndogo alizodai zimegharimu zaidi
ya Sh bilioni 6.