Monday, March 21, 2016
SHEIN ASHINDA URAIS KWA ASILIMIA 91.4
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha amemtangaza Rasmi Mgombea urais wa CCM Dr. Ali Mohammed Shein kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Zanzibar akiwa na kura 299.982 sawa na asilimia 91.4.
Sunday, March 13, 2016
Friday, March 11, 2016
HATIMAE MAGUFULI AWAPA SAFARI YA NJE MAWAZIRI WAWILI
Tangu Novemba 5 wakati Dk John Magufuli alipoapishwa, ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pekee waliotoka nje ya nchi, lakini jana Rais aliwaruhusu mawaziri wengine wawili kusafiri nje.
Rais Magufuli alizuia safari za nje siku chache baada ya kuapishwa akisema watumishi wa umma watakaokuwa wakitaka kwenda nje watalazimika kuomba kibali kutoka Ikulu, ikiwa ni mkakati wake wa kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali.
Tangu wakati huo, safari za nje kwa watumishi wa umma zimekuwa za nadra na mawaziri wamekuwa wakifanya ziara za kwenda mikoani kufuatilia utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
MBOWE: NAWALETEA KATIBU MKUU MAKINI
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja ukimya na kusema atawasilisha jina makini la mrithi wa nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.
Akizungumza mjini hapa jana, baada ya kumalizika kikao cha kwanza cha Kamati Kuu, Mbowe alisema sifa za kiongozi anayepaswa kushika wadhifa huo zinafahamika.
Alisema wajumbe na wanachama wa Chadema watarajie kumpokea mtu makini ambaye jina lake atalipendekeza kisha kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza Kuu kesho. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
MAREKANI YAMFILISI MTANZANIA MUUZA UNGA
SERIKALI ya Marekani juzi ilitangaza kutaifisha mali za bilionea Mtanzania, Ali Khatib Haji Hassan, maarufu Shikuba pamoja na mtandao wake wa kimataifa wa biashara ya dawa za kulevya.
Shikuba ambaye ni mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam, anamiliki msururu wa biashara kama vile maduka ya kubadili fedha (bureau de change), kampuni za ulinzi, majumba na utitiri wa magari ya kifahari.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani kupitia ofisi yake ya Udhibiti wa Mali Haramu za Raia wa Kigeni (OFAC), Shikuba na taasisi yake wameangukia katika sheria za nchi hiyo za kudhibiti mapapa wa unga wa kigeni (Kingpin Act).
Mbali ya sababu za kisheria, Marekani imesema bilionea huyo amekuwa akitumia faida haramu kutokana na biashara zake chafu kuhonga maofisa wa Serikali ya Tanzania ili asikamatwe na kushtakiwa. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
TRUMP NA RUBIO WATOFAUTIANA KUHUSU UISLAMU
Mgombea wa urais
kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu Donald
Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani katika mjadala uliokuwa
moja kwa moja runingani.
Bwana Rubio ambaye anakabiliwa na
ushindani wa maisha yake katika jimbo la Florida siku ya Jumanne amesema
kuwa Uislamu una tatizo la itikadi kali lakini akaongezea kuwa Waislamu
wengi wanapenda Wamerekani.
''Marais hawawezi kusema kile wanachotaka ,kuna madhara'',alisema huku raia wakimpigia makofi. Wagombea hao wanne wa chama cha Republican walisikia maombi kutoka kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mjadala wa amani.
Ikilinganishwa
na mjadala uliopita ambao ulikabiliwa na na matusi ya kibinafsi mjadala
huu ulikuwa na muongozo mzuri huku wagombea wote wakitoa malengo ya
sera zao.
''Kufikia sasa siamini vile tumekuwa watulivu hapa'',bwana Trump alinukuliwa akisema. Lakini
katika swala la Uislamu,kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na
wagombea wengine huku wenzake wote wakitofautiana naye kwamba familia za
magaidi ziangamizwe. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
SIMBA YARUDI KILELENI YAINYUKA NDANDA 3-0
TIMU ya soka ya Simba jana ilirejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kishindo baada ya kuinyuka Ndanda FC mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo ya ushindi wa jana yameiwezesha Simba kufikisha pointi 51 na
kuwashusha mahasimu wao wa jadi Yanga hadi nafasi ya pili, wakiwa
wamejikusanyia pointi 50 huku Azam FC wakibaki nafasi tatu na pointi 47.
Simba wamerejea kileleni kwa kuwazidi mahasimu wao Yanga kwa pointi moja, lakini Wanajangwani hao wapo nyuma kwa mchezo mmoja kutokana na kushuka dimbani mara 21 huku wapinzani wao wakicheza mara 22. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Simba wamerejea kileleni kwa kuwazidi mahasimu wao Yanga kwa pointi moja, lakini Wanajangwani hao wapo nyuma kwa mchezo mmoja kutokana na kushuka dimbani mara 21 huku wapinzani wao wakicheza mara 22. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Thursday, March 10, 2016
UTUMBUAJI MAJIPU WAOKOA BILLION 700/=
KASI
ya kuzuia ukwepaji kodi za Serikali uliofanywa kwa kipindi cha miezi mitatu na
utawala wa Rais Dk. John Magufuli kwa ‘kutumbua majipu’ umeokoa wastani wa Sh
bilioni 700.
Katika
utawala wa Serikali iliyopita ya awamu ya nne, wastani wa makusanyo ya kodi kwa
kiwango cha juu kwa mwezi yalikuwa Sh bilioni 900, lakini baada ya kuingia kwa
awamu hii kumekuwapo na ongezeko la zaidi ya Sh bilioni 700 kwa miezi mitatu ya
Desemba hadi Februari.
Akitangaza
ongezeko hilo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, alisema katika kipindi cha
Desemba 2015, pia TRA iliweza kuvuka lengo kwa kukusanya kiasi cha zaidi ya Sh.
trilioni 1.4 sawa na ongezeko la wastani wa Sh. bilioni 490 kwa mwezi.
Alisema
kiasi hicho ni kikubwa kikilinganishwa na wastani wa makusanyo kwa mwezi Julai
hadi Novemba mwaka jana ambapo ilikuwa ni Sh. bilioni 900 kwa mwezi. Like page
yetu ya facebook Jambo Tz
'NITAFANYA KAZI NA ALI KIBA BILA VIKWAZO' HARMONIZE
LICHA ya tetesi kwamba wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Ali
Kiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kutoonyesha nia ya kushirikiana katika
muziki wao, msanii anayetamba na wimbo wa ‘Bado’, Rajabu Ibrahimu
‘Harmonize’, amesema yupo tayari kufanya kazi na Ali Kiba bila kikwazo
chochote.
Msanii huyo alisema Ali Kiba ni msanii wa Tanzania na ni msanii mzuri
katika muziki hivyo kufanya naye ‘kolabo’ ni kitu cha kawaida kama
wasanii wengine anavyofanya nao.
“Mimi sijui kiukweli kama kuna bifu kati ya Diamond na Ali Kiba kwa
sababu sijawahi kumsikia Diamond akimzungumzia Ali Kiba kwamba wana
ugomvi,” alisema Harmonize.
Harmonize ambaye hivi karibuni alijinadi kutoanzisha uhusiano wa
kimapenzi, anazidi kujizolea umaarufu kutokana na nyimbo zake tatu
ukiwemo ‘Aiyola’, ‘Kidonda Changu’ na ‘Bado’ huku akizidi kujipanga kwa
mambo mengine makubwa yatakayokuja kupitia kampuni ya wasafi
anayoifanyia kazi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
MKWASA ATAJA SABABU ZA KUMUITA KAZIMOTO
KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya soka ‘Taifa Stars’, Boniface Mkwasa, amesema uwezo mkubwa aliokuwa nao kiungo wa Simba,
ndio umemfanya amuite kwenye kikosi chake kitakachocheza na Chad, Machi
23 kwenye mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon),
utakaochezwa mji wa Djamena, nchini Chad.
Mkwasa alimjumuisha mchezaji huyo kwenye kikosi chake hicho chenye jumla ya wachezaji 25, licha ya kuwa tayari ameshatangaza kuacha kuichezea timu ya Taifa ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Mkwasa alisema, Mwinyi ameonyesha mchango mkubwa kwenye timu yake ya Simba na ndio sababu iliyompelekea kumjumuisha kwenye kikosi chake ambacho kulingana na ratiba ilivyobana anahitaji kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa ili kuweza kupambana na Chad kwani hawana muda mrefu wa kujiandaa.
“Hizo taarifa za kuwa amestaafu kuichezea timu ya Taifa sijazipata hivyo haikuwa kikwazo kwangu kumuita, lakini pia bado ana kiwango kizuri ni kijana mkongwe na amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake, bado ana nafasi kubwa ya kulisaidia Taifa lake,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Mkwasa alimjumuisha mchezaji huyo kwenye kikosi chake hicho chenye jumla ya wachezaji 25, licha ya kuwa tayari ameshatangaza kuacha kuichezea timu ya Taifa ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Mkwasa alisema, Mwinyi ameonyesha mchango mkubwa kwenye timu yake ya Simba na ndio sababu iliyompelekea kumjumuisha kwenye kikosi chake ambacho kulingana na ratiba ilivyobana anahitaji kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa ili kuweza kupambana na Chad kwani hawana muda mrefu wa kujiandaa.
“Hizo taarifa za kuwa amestaafu kuichezea timu ya Taifa sijazipata hivyo haikuwa kikwazo kwangu kumuita, lakini pia bado ana kiwango kizuri ni kijana mkongwe na amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake, bado ana nafasi kubwa ya kulisaidia Taifa lake,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
LIVERPOOL KUCHUANA NA MAN U EUROPA
Mkufunzi wa timu ya Liverpool Jurgen
Klopp ameitaja mechi ya Alhamisi ya kombe la Europa kati ya Liverpool
na Manchster United kuwa mechi kubwa sana.
Liverpool wanaikaribisha Anfield timu ya Manchester United ikiwa ni mkutano wao wa kwanza Ulaya.
Hatahivyo
Klopp anasema :''kila siku kombe la Europa linafurahisha.Ni Mechi kubwa
sana.Ijapokuwa sio kubwa zaidi katika kazi yangu kama mkufunzi wa
Liverpool lakini ni muhimu sana''.
Manchester United imeshinda makombe 3 ya bara Europa hivi karibuni ikiwa 2008,huku Liverpool ikilibeba kombe hilo mara tano.
Mkufunzi
wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa wale wanaomkosoa kwa
kushushwa katika kombe la Europa hawaelewi huku Klopp akisema kuwa
anaamini mechi hiyo itasisimua mashabiki katika uwanja wa Anfield.
Saturday, March 05, 2016
Friday, March 04, 2016
MAGUFULI "MAJIPU YAKINISHINDA SINA SABABU YA KUENDELEA KUWA RAIS"
RAIS Dk. John Magufuli, amesema kama atashindwa kutumbua majipu dhidi
ya wazembe na wabadhirifu serikalini, hana sababu ya kuendelea kushika
wadhifa huo.
Amesema endapo hali hiyo ikitokea ni bora arudi nyumbani kwake
akalale, kwa sababu lengo lake la kuwapatia wananchi Tanzania mpya,
litakuwa halijatimia.
Rais Dk. Magufuli aliyasema hayo jana, wakati wa hafla ya kuweka jiwe
la msingi la ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili yenye urefu wa
kilometa 234.3, itakayogharimu Sh bilioni 209.3
“Ndugu zangu kazi hii ni ngumu, wapo watu ambao hawataki mimi na
Serikali yangu kuwatumbua, nitapambana hadi nihakikishe ninafanikiwa.
“Na iwapo nitashindwa hakuna sababu ya mimi kuendelea kuwa Rais wa nchi hii, ni bora nirudi nyumbani kwangu kulala,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)