UGONJWA wa kipindupindu umeripotiwa katika Jiji la Dar es Salaam na watu wawili wamethibitika kufa.
Wengine zaidi ya 30 wamelazwa katika hospitali za Mwananyamala na Sinza zilizopo Manispaa ya Kinondoni.
Kutokana na tishio la ugonjwa huo, shughuli za kampeni za kisiasa za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu wa Rais, wabunge na madiwani, zilizo kuwa zianze mwishoni mwa wiki hii, zimesogezwa mbele.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki alithibitisha hayo jana alipokuwa akitoa taarifa ya ugonjwa huo kupitia Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC 1).
Alisema watu hao wawili waliofariki, mmoja ni mwanamume na mwingine ni mwanamke na wanatoka Manispaa ya Kinondoni.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Meninah Atick ‘Mennahladiva’ mwishoni mwa wiki aliuaga ukapera kwa kufunga ndoa na mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Abdukarim Haule.
Meninah, ambaye kipaji chake cha muziki kilianza kuonekana kupitia shindano la Bongo Star Search, ametamba na nyimbo za ‘Dream Tonight’, ‘Ka-Copy Ka-Paste’.
Mtoto huyo wa Waziri Muhongo, Peter Haule, amebadili dini na kuitwa Abdukarim Haule na harusi yao ilifanyika Kigamboni, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Licha ya wengi kumpongeza msanii huyo, ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kwamba: “Usichague msichana ambaye ni mzuri duniani, chagua anayekupa furaha duniani, maisha ni mafupi na huwezi jua kesho kuna nini, fanya mazuri, asante Mungu kwa kila njia ninayopitia, nazidi kukumbuka kwa kubadilisha maisha yangu na kutumaini milele”.
MWIGIZAJI wa filamu ambaye jina lake limepitishwa nafasi ya ubunge viti maalumu Mkoa wa Tabora kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Irene Uwoya, amesema malezi aliyopewa na wazazi wake ndiyo yatakayomsaidia kuwa kiongozi bora.
Irene alisema hayo juzi katika hafla fupi iliyoandaliwa na wazazi wake kumpongeza kupitishwa katika nafasi hiyo ambapo pia marafiki zake wa karibu walihudhuria sherehe hiyo.
“Nisingekuwa hapa nilipofika kama wazazi wangu wasingenionyesha moyo na ushirikiano wa kutosha, najivunia kwani wamenisaidia kujenga moyo wa ujasiri ndani yangu na naamini nitawatendea haki kwa kuhakikisha ninakuwa kiongozi bora,” alisema Irene.
Irene alieleza kuwa lengo lake la kugombea nafasi hiyo ni kuhakikisha anaingia bungeni kuwatetea vijana wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali, hasa katika Mkoa wa Tabora.
KUNDI linalofanya vizuri na wimbo wao wa ‘Nerea’ kutoka nchini Kenya, Sauti Sol, limetangaza kutafuta wachumba wa kuoa nchini Tanzania, huku wakiwaomba radhi wasichana wa Kenya.
“Samahani kwa wasichana wa nchini Kenya kutokana na maamuzi yetu ya kutaka kuoa huku Tanzania. Dar es Salaam. Kwa sasa tunatafuta warembo wa kuwaoa,” waliandika wasanii hao kupitia akauti yao ya Twitter.
Wasanii hao kwa sasa wanafanya vizuri nchini humo na wamefanikiwa kuchukua tuzo mbalimbali nje ya nchi ya Kenya.
Nyota namba tatu kwa ubora wa mchezo wa tenesi muingereza Andy Murray ametwaa ubingwa wa michuano ya Rogers
Murray ametwaa ubingwa huu baada ya kumshinda mpinzani wake Novack Djokovic kwa seti 6-4 4-6 6-3 katika mchezo uliochukua muda wa saa tatu.
Kwa ushindi huu Murray anavunja mwiko wa kupoteza mapambano manane dhidi ya Novack ambae anashilikia nafasi ya kwanza kwa ubora.
Murray amemzawadia ushindi huo kocha wake Amelie Mauresmo, aliyepata mtoto wa kiume siku ya jumapili.
Ligi kuu ya England imeendelea tena kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja vya Etihad na Selhurst Park.
Katika mchezo wa kwanza Arsenal walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace
Arsenal walianza kuandika bao lao la kwanza dakika ya 16 liliwekwa kimiani na mshambuliaji Olivier Giroud.
Crystal Palace wakasawazisha bao hilo kupitia kwa mlinzi wake Joel Ward.
Bao la kujifunga la beki Damien Delaney likawapa ushindi Arsenal .
Katika mchezo wa pili Chelsea walikubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa Manchester City
Magoli ya City yakifungwa na mshambuliaji Sergio Aguero, Vincent Kompany na Mbrazil Fernandinho akahitimisha kwa ushindi kwa bao la tatu kwa mkwaju mkali uliomshinda mlinda mlango wa Man City Joe Hart.
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa watumiaji
vibaya na wahalifu wote wa mitandao nchini, kuwa siku zao zinahesabika
kwani ifikapo Septemba mosi, mwaka huu, Sheria ya Uhalifu wa Mitandao
itaanza kutumika na wengi huenda wakaishia gerezani.
Mamlaka hiyo imebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inaongoza kwa kuwa na
watumiaji vibaya wengi wa mitandao ya kijamii, jambo linalosababisha
taarifa za mitandao mingi kutoaminika hadi nchi za nje kutokana na kujaa
uzushi, uongo, uchochezi na lugha na picha za matusi.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa
TCRA, Innocent Mungy alikiri kuwa pamoja na kwamba mamlaka hiyo imefanya
kazi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya utumiaji sahihi wa mitandao hiyo,
bado matumizi yake si mazuri hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na
kwa watu maarufu.
“Napenda kuwatahadharisha Watanzania na watumiaji wa mitandao hii kwa
ujumla kuwa sheria hii si ya kupuuzwa, kwani kwa hali ilivyo wengi
watatozwa faini na watashindwa kulipa na kuishia gerezani,” alisisitiza. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe amesema
uchovu ndiyo sababu iliyomfanya kuugua ghafla jana na kulazwa katika
Hospitali ya Taifa, Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Akiwa
katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,
Edward Lowassa, kuchukua fomu jana, Mbowe aliugua ghafla eneo la
Manyanya, Kinondoni na kulazimika kukimbizwa Muhimbili ambako amelazwa
hadi leo.
Hata hivyo, mwanasiasa huyo
ambaye anawania ubunge katika jimbo la Hai kupitia Chadema
amewahakikisha wanachama na wafuasi wa Ukawa kuwa afya yake ni njema na
huenda akaruhusiwa kutoka hospitalini ndani ya saa 48.
Akizungumza
na Mwananchi jana, Ofisa Uhusiano wa Muhimbili Aminieli Aligaesha
pamoja na kukiri kulazwa kwa mwanasiasa huyo, hakutaka kuweka hadharani
kilichokuwa kinamsumbua Mbowe. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
MAKAMU wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal amekanusha taarifa za uzushi
ziliposambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anakihama Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Akizungumza jana, Katibu wa Makamu wa Rais, Zahor Mohammed Haji kwa
niaba ya Dk Bilal, alisema taarifa hizo ni za uongo na uzushi wa aina
yake. Zahoro alisema, Dk Bilal yupo nchini Uingereza katika shughuli za
ujenzi wa taifa na kwamba hana mpango wa kuondoka CCM na wanaoeneza
uzushi huo wana lao jambo.
Katibu huyo amemnukuu Dk Bilal akisema; “Ndugu zangu wa CCM, na
Watanzania kwa ujumla, napenda kuchukua fursa hii kuwa taarifu kwamba
kuna taarifa inayoenezwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo
facebook na whatsApp kuwa nitaitisha mkutano na vyombo vya habari ili
kujitoa CCM.
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Mtwara nje ya ofisi ya CCM jana. Picha na Ofisi ya CCM
Waziri wa Ujenzi na
mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema kuwa wana-CCM mwaka huu
wanapaswa kufanya kampeni za kisayansi zaidi kuhakikisha wanapata
ushindi wa tsunami utakaowezesha kuundwa kwa Serikali imara
itakayowaletea maendeleo Watanzania wote.
Alisema kwa
kufanya hivyo kutawasaidia kupata viti vingi na kusimamia shughuli zote
za maendeleo na kwa manufaa ya wanaCCM na Watanzania wote kwani mahitaji
yao na matarajio yao ni kupata maendeleo makubwa.
“Niwaombe
wana CCM wenzangu, tushikamane tuwe wamoja. Kampeni za mwaka huu ni
lazima tufanye kampeni za kisayansi zaidi, ni lazima kampeni zianze
katika ngazi ya nyumba kumi, vitongoji kwa vitongoji, vijiji, mitaa,
kata majimbo, wilaya, mikoa na baadaye urais kwa ujumla. Katika umoja
huu nataka niwahakikishie ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga, ni
wa tsunami,” alisema Dk Magufuli. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vingine
vitatu vya upinzani vinavyounda umoja unaofahamika kwa jina la Ukawa,
Edward Lowassa jana alichukua fomu za kuwania rasmi nafasi hiyo kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani aliyejiunga Chadema hivi karibuni
baada ya kushindwa katika mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi
ya CCM, sasa ameungana na wagombea wengine kujitokeza NEC kuchukua fomu
za kuwania urais.
Ametanguliwa na mgombea wa CCM, Dk John Magufuli ambaye pia ni Waziri
wa Ujenzi na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa. Wengine ni Mchungaji
Christopher Mtikila wa DP, Mac-Millan Lyimo wa TLP, Hashim Rungwe wa
CHAUMMA, Chifu Lutasola Yemba wa ADC na Dk Godfrey Malisa wa CCK. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Kiongozi
wa mashtaka nchini Burundi amesema kuwa watu kadhaa wanaoshukiwa
kutekeleza mauaji ya jenerali Adolphe Nshimirimana wamekamatwa. Hata hivyo Afisa huyo anasema kuwa viongozi waliopanga njama ya kumua jenerali huyo wangali wanasakwa.
Kufuatia mauaji ya kiongozi huyo wa kikosi
cha ulinzi wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Mwanaharakati maarufu
wa haki za kibinaadamu nchini humo alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya
na watu waliokuwa katika pikipiki .
Pierre Claver Mbonimpa alishambuliwa katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura mapema wiki hii. Mbonimpa amekuwa mkosoaji mkubwa wa tangazo la rais Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu.
Hadi kufikia sasa haijajulikana ni nani aliyekuwa amelenga kumtoa uhai.
Wakati
huohuo taharuki imetanda katika mji mkuu wa Bujumbura baada ya milio ya
risasi kusikika katika maeno kadha ya mji huo usiku wa kuamkia leo.
Hakuna taarifa zaidi ila habari zinasema huenda wanajeshi kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa. Inaelezwa milio hiyo ya risasi ilisikika baada ya gari moja kutoka ofisi ya Rais wa nchi hiyo kuchomwa moto.
Burundi imekabiliwa na ghasia tangu hatua ya rais Nkurunziza mnamo mwezi Aprili kutaka kuwania muhula wa tatu. Wapinzani wamedai kwamba hatua hiyo ni kinyume na katiba huku jaribio la mapinduzi likifeli mnamo mwezi Mei.
Uchaguzi wa urais ulifanyika mwezi uliopita ambapo bwana Nkurunziza alishinda lakini ulisusiwa na upinzani.
Mbunge wa Bariadi Magharibi,
Andrew Chenge amekiri mbele ya Baraza la Maadili kupokea Sh1.6 bilioni
kutoka Kampuni ya VIP Enginering and Marketing Limited, zikiwa ni malipo
ya kutoa ushauri.
Pia, alihoji kama kuna tatizo kutumia taaluma yake ya sheria kuzishauri kampuni binafsi na kujipatia fedha.
Chenge
ambaye alitoa utetezi wake jana saa 7:30 mchana, alisema hakulipwa
fedha hizo kwa sababu ni kiongozi wa umma, bali kwa kutoa ushauri.
Alisema
aliingia mkataba na kampuni hiyo wa kutoa ushauri wa kisheria dhidi ya
Kampuni ya Mechmer ambazo ni kampuni binafsi zilizokuwa na mgogoro. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.