Tanzania na Uganda zimeshuka katika viwango ya FIFA vilivyotolewa Alhamis huku Kenya, Sudan na Rwanda zikipanda.
Licha ya kushuka, Uganda, ambayo hivi karibuni imeitoa Tanzania katika kugombania nafasi ya kucheza fainali za CHAN mwakani nchini Rwanda, ndio nchi iliyo juu katika viwango vya FIFA kwa nchi za Afrika ya Mashariki.
Kushuka kwa Tanzania kunatokana na kufungwa na Uganda 4-1 katika michuano ya CHAN na kufungwa na Misri 3-0 katika mechi ya kwanza ya kugombania kufuzu kucheza fainali za AFCON.
Kenya imepanda nafasi saba na sasa ni ya 116 katika viwango hivyo ya Dunia. Rwanda ipo nafasi ya 78, ikipanda nafasi 16 wakati Sudan ikiwa nafasi ya 90, ikipanda nafasi 18. Burkina Faso (72), Botswana (120) na Comoros (187).
Algeria ndio timu inayoongoza katika viwango vya FIFA kwa Afrika ikiwa nafasi ya 19. Timu ya Agentina, licha ya kufungwa na Chile katika fainali za Copa America, imepanda na kuwa timu ya kwanza katika viwango va FIFA, ikiitoa Ujerumani. Tano bora za viwango vya FIFA ni Argentina, Germany, Belgium, Colombia na Uholanzi.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.