Naibu rais wa Kenya Mh. William Ruto ameonya kuwa ndoa za jinsia moja ni haramu na kuwa hazitawahi kuruhusiwa nchini humo.
Ruto amechukua msimamo huo mkali siku chache tu kabla ya ziara wa Marekani Barrack Obama nchini Kenya.
Mahakama ya juu nchini Marekani majuzi ilihalalisha ndoa za jinsia moja kote nchini humo.
''Kwa kweli uhusiano na ndoa ya jinsia moja kwa hakika inakiuka mpango wa mwenyezi Mungu, Mungu hakuwaumba mwanaume na mwanamke ili mwanaume amuoe mwanaume mwenzake wala mwanamke amuoe mwanamke mwenzake'' alisema bwana Ruto alipowahutubia waumini wa kanisa moja jijini Nairobi.
''Tumesikia majuzi wamarekani wamehalalisha ndoa ya jinsia moja na mambo hayo machafu.
''Nataka niwahakikishie kama kiongozi mkristo kuwa mimi ninapinga uchafu huo na nitailinda Kenya, Nitasimamia ukweli na mafundisho ya dini yangu''
Aliwataka wakristo na waislamu waungane kupinga shinikizo la aina yeyote ya kuhalalisho ndoa ya jinsia moja nchini Kenya.
''Hata wajaribu vipi ama watumie ushawishi wa nadharia hatutabadilisha msimamo wetu ''
''Tunamuamini mwenyezi mungu, na hili ni taifa linalomtukuza Mungu na litaendelea kufanya hivyo'' alisema bwana Ruto
Tayari muungano wa viongozi wa madhehebu mbalimbali nchini Kenya chini ya muavuli wa shirika la haki la Wakatholiki na vuguvugu la Wakristu wamepanga maandamano mjini Nairobi wakipinga mapenzi ya jinsia moja.
No comments:
Post a Comment