Umoja wa
watendaji wakuu wa kampuni wa CEO RoundTable (CEOrt) umeandaa mdahalo wa
kuzungumzia mbio za urais utakaowahusisha viongozi wa vyama vya
upinzani, Profesa Ibrahim Lipumba, Dk Willibrod Slaa, Zitto Kabwe na
Emmanuel Makaidi, lakini Chadema imesema itakuwa tayari kwa midahalo
baada ya mchakato wa ndani kukamilika.
Kauli hiyo ya Chadema inaweza kuwa kikwazo kingine
kwa CEOrt kuendesha midahalo hiyo baada ya wa kwanza uliokuwa uhusishe
makada 10 wa CCM wanaoomba ridhaa ya chama hicho kuwania urais,
kushindwa kufanyika kutokana na viongozi wa sekretarieti kutoa kauli
tofauti siku moja kabla.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
Kiongozi wa CEO, Ali Mufuruki alisema jana kuwa Dk
Slaa, Profesa Lipumba, Makaidi na Zitto, ambaye ni kiongozi mkuu wa
ACT-Wazalendo, wamethibitisha kushiriki kwenye mdahalo huo utakaofanyika
kesho kuanzia saa 1:00 jioni jijini Dar es Salaam.
Lakini Dk Slaa aliiambia Mwananchi jana kuwa
Chadema itakuwa tayari kushiriki kwenye midahalo baada ya kumaliza
mchakato wa kupata mgombea wake na kukamilisha Ilani ya Uchaguzi, mambo
ambayo alisema hupitishwa na vikao vya juu.
“Kamanda, sijui kama ni kongamano au mdahalo: 1.
Chadema inaendeshwa kwa katiba, kanuni na taratibu zake. Hadi siku ya
leo taratibu zetu hazijafikia kupata aspirants (watangazania),” alisema
katibu huyo mkuu wa Chadema katika ujumbe wake mfupi wa simu.
“2. Kama kuna waliopata aspirants, Chadema bado
mchakato wetu unaendelea. 3. Midahalo inafanywa kwa msingi wa ilani.
Chadema ilani yetu haijafika bado mbele ya vikao vya maamuzi, yaani
Baraza Kuu na Mkutano Mkuu. Hivyo tukienda mdahalo tutakuwa
tunazungumzia ilani ipi?
“Hivyo tuko tayari kwa midahalo yote baada ya mchakato wetu wa ndani kukamilika.”
Mufuruku alikuwa ametuma taarifa hiyo kwenye
ukurasa wake wa facebook na alipopigiwa simu na Mwananchi, alithibitisha
kuwapo kwa mdahalo huo ambao alisema utaonyeshwa moja kwa moja na vituo
vya televisheni, redio na intaneti.
Kuhusu ushiriki wa Zitto, ambaye atagombea ubunge
wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mufuruki alisema CEOrt imemualika kwa kuwa ni
kiongozi wa chama ambacho kinaweza kusimamisha mgombea wa urais.
“Kushiriki si lazima uwe unachukua fomu za
kugombea urais. Yeye ni kiongozi wa chama ana mawazo yanayoweza kutoa
mchango kwenye mdahalo,” alisema Mufuruki.
CEOrt imepanga kufanya midahalo kadhaa mwezi huu
na Juni 25 itaendesha mdahalo utakaoshirikisha wagombea kutoka CCM baada
ya kada mmoja tu, Balozi Amina Salum Ali, kujitokeza kwenye mdahalo wa
kwanza na hivyo kusababisha uahirishwe.
Profesa Lipumba, ambaye amechukua fomu za kuomba
ridhaa ya CUF kupitishwa kugombea urais kwa mara ya tano iwapo jina lake
litapitishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliiambia
Mwananchi jana kuwa atashiriki kwenye mdahalo huo, kama ilivyo kwa
Makaidi ambaye amepitishwa na NLD kuwania nafasi hiyo.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD vimepanga kusimamisha mgombea
mmoja atakayeungwa mkono na vyama vyote, lakini kila chama kitalazimika
kupata mgombea wake ambaye jina lake litapelekwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kupitishwa kabla ya kuteua mmoja ambaye
atawakilisha vyama hivyo kwenye Uchaguzi Mkuu.
ridhaa ya chama hicho kuwania urais, kushindwa
kufanyika kutokana na viongozi wa sekretarieti kutoa kauli tofauti siku
moja kabla.
Kiongozi wa CEOrt, Ali Mufuruki alisema jana kuwa
Dk Slaa, Profesa Lipumba, Makaidi na Zitto, ambaye ni kiongozi mkuu wa
ACT-Wazalendo, wamethibitisha kushiriki kwenye mdahalo huo utakaofanyika
kesho kuanzia saa 1:00 jioni jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Dk Slaa aliliambia gazeti hili jana
kuwa, Chadema itakuwa tayari kushiriki kwenye midahalo baada ya kumaliza
mchakato wa kupata mgombea wake na kukamilisha ilani ya uchaguzi, mambo
ambayo alisema hupitishwa na vikao vya juu.
“Kamanda, sijui kama ni kongamano au mdahalo: 1.
Chadema inaendeshwa kwa katiba, kanuni na taratibu zake. Hadi siku ya
leo taratibu zetu hazijafikia kupata aspirants (watangazania),” alisema
katibu huyo mkuu wa Chadema katika ujumbe wake mfupi wa simu.
“2. Kama kuna waliopata aspirants (watiania),
Chadema bado mchakato wetu unaendelea. 3. Midahalo inafanywa kwa msingi
wa ilani. Chadema ilani yetu haijafika bado mbele ya vikao vya maamuzi,
yaani Baraza Kuu na Mkutano Mkuu. Hivyo tukienda mdahalo tutakuwa
tunazungumzia ilani ipi?
“Hivyo tuko tayari kwa midahalo yote baada ya mchakato wetu wa ndani kukamilika.”
Mufuruki alikuwa ametuma taarifa hiyo kwenye
ukurasa wake wa facebook na alipopigiwa simu na Mwananchi, alithibitisha
kuwapo kwa mdahalo huo ambao alisema utaonyeshwa moja kwa moja na vituo
vya televisheni, redio na intaneti.
Kuhusu ushiriki wa Zitto, ambaye atagombea ubunge
wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mufuruki alisema CEOrt imemualika kwa kuwa ni
kiongozi wa chama ambacho kinaweza kusimamisha mgombea wa urais.
“Kushiriki si lazima uwe unachukua fomu za
kugombea urais. Yeye ni kiongozi wa chama ana mawazo yanayoweza kutoa
mchango kwenye mdahalo,” alisema Mufuruki.
CEOrt imepanga kufanya midahalo kadhaa mwezi huu
na Juni 25 itaendesha mdahalo utakaoshirikisha wagombea kutoka CCM baada
ya kada mmoja, Balozi Amina Salum Ali, kujitokeza kwenye mdahalo wa
kwanza na hivyo kusababisha uahirishwe.
Profesa Lipumba, ambaye amechukua fomu za kuomba
ridhaa ya CUF kupitishwa kugombea urais kwa mara ya tano iwapo jina lake
litapitishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliiambia
Mwananchi jana kuwa atashiriki kwenye mdahalo huo, kama ilivyo kwa
Makaidi ambaye amepitishwa na NLD kuwania nafasi hiyo.
NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD vimepanga kusimamisha mgombea mmoja
atakayeungwa mkono na vyama vyote, lakini kila chama kitalazimika kupata
mgombea wake ambaye jina lake litapelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kwa ajili ya kupitishwa kabla ya kuteua mmoja ambaye atawakilisha
vyama hivyo kwenye Uchaguzi Mkuu.Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
No comments:
Post a Comment