Chelsea
itaanza utetezi wa taji la ligi ya Uingereza wakati itakapoikaribisha
nyumbani Swansea katika wikiendi ya tarehe 8-9 mwezi Agosti.
Manchester
City iliomaliza pointi nane nyuma ya Chelsea itaelekea West Bromwich
huku Manchester United ikikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old
Trafford.
Arsenal itaialika West Ham
,Liverpool ikienda Stoke,Newcastle itakabiliana na Southampton huku
Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.
Bournemouth iliopandishwa daraja,Watford na Norwich zitakabiliana na Aston Villa,Everton na Crystal Palace mtawalia.
No comments:
Post a Comment