James Horner, enzi za uhai wake.
James Horner mtunzi nguli wa eneo maarufu kwa watu maarufu la Hollywood ambaye aliandika na kushinda katika tuzo za Oscar juu ya filamu maarufu ulimwenguni ya Titanic, amefariki dunia mjini California kutokana na ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka 61.
James alipata mafunzo ya urushaji wa ndege, inaarifiwa alikuwa peke yake wakati alipopata ajali hiyo, na ndege binafsi ndogo ambayo alipata nayo ajali eneo la Kusini mwa Santa Barbara mwanzoni mwa wiki hii.
Mwandishi huyu na mtunzi wa tungo mbali mbali ametia mkono wake katika kazi tatu tofauti za filamu za msanii James Cameron, pamoja na filamu ya A Beautiful Mind, Braveheart, Troy na ile ya Apollo 13.