Watoto
walioathirika na Virusi vya Ukimwi watanufaika kutokana na uamuzi wa
mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani kuidhinisha dawa mpya ambazo
zinaweza kuchanganywa kwenye Chakula ili kuwarahisishia matumizi watoto
wanaoishi na virusi vya ukimwi.Shirika la Umoja wa Mataifa la
kushughulikia Ugonjwa wa Ukimwi ,UNAIDS na Shirika linalohudumia watoto
duniani, UNICEF yameeleza.
Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Michel
Sidibe' amesema kuwa dawa hizi ni mbadala wa zile ambazo zilikuwa
hazifurahiwi na watoto, zenye ladha mbaya.Dawa hizi zitawawezesha watoto
kuzidi kupata tiba nzuri na kuwafanya watoto wawe na afya, amesema
haikubaliki kuwa asilimia 24 pekee ya watoto walioathirika wapate dawa
za kupunguza makali.
Dawa hizi zimetengenezwa nchini India, zina
viambata vya Lopinavir na ritonavir ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye
chakula cha mtoto.Dawa hizi haziharibiwi na joto la chakula na zina
ladha nzuri kuliko zinazopatikana sasa, vidonge hivi vinafaa kwa
matibabu kwa watoto.
Hii ni hatua mpya katika mipango ya kuokoa
maisha ya Watoto waishio na virusi vya ukimwi, Mkurugenzi wa Mradi wa
Ukimwi wa UNICEF,Craig McClure amesema '' tunatarajia kuimarisha
upatikanaji wa matibabu kwa ajili ya watoto wengi zaidi na kuunga mkono
mpango wa kuwafikia watoto wasiopata huduma hii duniani kote''. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment