Timu
pekee iliyobakia kwenye mashindano ya shirikisho la mpira wa miguu
barani Afrika kutoka Tanzania, Yanga, imeendelea kuweka matumaini hai ya
kusonga mbele baada ya kuiangushia kipigo kikali timu ya Platnum ya
Zimbabwe kwa mabao 5-1.
Mchezo huo wa raundi ya kwanza ya vilabu vinavyoshiriki Kombe la Shirikisho la CAF, ulifanyika Jumapili jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa kufungana mabao 2-1.
Kipindi cha Pili ndicho kilichokuwa kiama chya Platnum baada ya kuruhusu mabao matatu zaidi.
Wafungaji
wa timu ya Yanga ni Mrisho Ngasa aliyefunga magoli mawili, Haruna
Niyonzima, Salum Telela, na Amisi Tambwe walifunga bao moja kila mmoja.
Kwa matokeo hayo Yanga imejenga mazingira ya kusonga mbele. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.