Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akibariki matoleo yakiotolewa na Umoja wa Wanawake wa katoriki(WAWATA), wakati wa Ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam jana.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki
la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema waumini
hawana budi kusoma vizuri na kuelewa Katiba Inayopendekezwa ili wakati
ukifika, wafanbye uamuzi kwa hiari na utashi wao wakati wa kupiga Kura
ya Maoni.
Ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku mbili baada ya
Jukwaa la Wakristo kutoa tamko linalowataka waumini kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura, kushiriki kikamilifu kwenye
shughuli zote za elimu ya Katiba Inayopendekezwa na kupiga kura ya
“hapana” kuikataa Katiba Inayopendekezwa.
Lakini jana, Kardinali Pengo alisema kuisoma na
kuielewa katiba hiyo ndiyo wajibu wa msingi ambao Wakristo wanao kwa
sasa ili kupiga kura inayostahili wakati ukifika. Kuhusu maaskofu
kuagiza waumini waikatae Katiba Inayopendekezwa, Kardinali Pengo alisema
wao wakiwa viongozi wa watu, hawana mamlaka wala uwezo huo, bali wenye
uwezo ni wananchi wenyewe. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Hata hivyo, Kardinali Pengo alitaka tamko hilo
lisambazwe kwenye parokia na vigango vyote vya Jimbo Kuu la Dar es
Salaam ili waumini wasomewe, wauelewe kwanza, ili hatimaye waweze
kufanya uamuzi sahihi wakielewa ni nini wanachokitakiwa kukifanya.
Changamoto za familia
Katika hatua nyingine, Kardinali Pengo pia
alizungumzia changamoto za wanandoa, ikiwamo tabia ya kuchepukia nje ya
ndoa ambayo alisema inasababisha amani kutoweka ndani ya familia.
Akizungumza katika ibada ya Kwaresima kwa Wanawake
Wakatoliki Tanzania (Wawata) jana, Kardinali Pengo alisema akina mama
wengi kwa sasa, hususan katika ndoa wamekuwa wakisaliti ndoa na baadaye
kuwatupia lawama watoto wao juu ya tabia walizoanzisha wenyewe.
Katika mahubiri yake aliyoyatoa katika Kanisa la
Mt. Joseph Dar es Salaam, mbali na changamoto sugu za kifamilia,
Kardinali Pengo alijikita katika kuangalia aina sita za malezi kwa
watoto na athari za utandawazi kwenye jamii.
“Wapo wanawake ambao kwa sasa wanaendekeza
michepuko kwenye familia na wamekuwa hawana hofu ya Mungu wakati wote.
Kuna wengine ambao wanavaa mavazi ya mabinti wakisema wanakwenda na
wakati,” alisema.
“Wanawakemea watoto wao wakati wao wanaendekeza tabia chafu, wakiulizwa wanasema eti wao wameshakuwa watu wazima.”
Katika sehemu ya mafundisho yake, mbali na
kupungua uaminifu, Kardinali Pengo alizitaja changamoto nyingine
alizosema kuwa zimeendelea kuumiza familia ambazo ni tofauti za kiimani,
kipato, elimu, kulea watoto nje ya ndoa, kushindwa kudhibiti maadili ya
watoto, ushirikina na ufisadi.
Alisema changamoto hizo zinatafuna familia nyingi kwa sasa.
”Familia inayokuwa inaendeshwa kwa imani tofauti za kidini ni changamoto kubwa sana, amani inapungua ndani ya familia kwa hivyo tunahitaji kuwa makini na changamoto hizo,” alisema Kardinali Pengo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
”Familia inayokuwa inaendeshwa kwa imani tofauti za kidini ni changamoto kubwa sana, amani inapungua ndani ya familia kwa hivyo tunahitaji kuwa makini na changamoto hizo,” alisema Kardinali Pengo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment