Jana ilikuwa siku ya hisia tofauti kwa watu wawili wanaotajwa kwenye kinyang’anyiro cha urais, Edward Lowassa na Lazaro Nyalandu baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kumsifu mmojawao na kumponda mwingine.
Akiwa Kondoa, Kinana alitumia muda mwingi kujibu
kilio cha wananchi wanaosumbuliwa na askari wa wanyamapori kwa kumponda
Waziri Nyalandu kuwa anazurura bila kushughulikia matatizo ya wananchi,
lakini saa chache baada ya kuwasili Monduli alimsifu Lowassa kuwa ni
kiongozi shupavu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Tayari Nyalandu ameshatangaza nia ya kugombea
urais, wakati Lowassa, mmoja wa wanachama wa CCM wanaotajwa sana kwenye
kinyang’anyiro hicho, hajatangaza uamuzi wake lakini anatumikia adhabu
ya chama chake kilichomfungia kujihusisha na harakati za uongozi pamoja
na makada wengine watano.
Baada ya msafara wa Kinana kuwasili Monduli na
kupokewa na viongozi wa chama hicho wa eneo, katibu huyo wa CCM, Kinana
alipata nafasi ya kuzungumza machache kabla ya kuanza safari ya kukagua
shughuli mbalimbali.
“Hatuna shaka na Monduli kwa kuwa yupo kiongozi
shupavu, ndugu yetu Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa (Halmashauri Kuu ya
CCM) Nec,” alisema Kinana akiwaelezea wananchi waliokuwapo eneo hilo.
“Wa Monduli mna kiongozi shupavu na mchapakazi. Hongera Bwana Lowassa.”
Baadaye, Lowassa aliwakaribisha akisema: “Mmefanya kazi kubwa sana ya kukijenga chama chetu. Nawashukuru sana, karibuni.”
Naye katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye alisema: “Nafurahi kuwa katika jimbo la mzee wangu, rafiki yangu
Edward Lowassa. Mapokezi mazuri, bila shaka Arusha mmeamka.”
Kinana amekuwa akitumia sehemu kubwa ya ziara yake
kushuhutumu viongozi wa Serikali na hasa mawaziri kwa kushindwa
kuwatatulia wananchi matatizo yao na ilifikia wakati aliwataja mawaziri
wanne aliowaita kuwa ni mizigo, tofauti na alivyofanya kwa waziri mkuu
huyo wa zamani.
Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Serikali
ya Awamu ya Nne na anajulikana kama mtu aliye tayari kufanya uamuzi
mgumu. Alilazimika kujiuzulu wadhifa huo mwaka 2008 baada ya kuibuka kwa
kashfa ya Richmond.
Kinana alikuwa mtu tofauti wakati akijibu kero za
wananchi mkoani Singida, ambako alimtaja moja kwa moja Waziri Nyalandu
kuwa hashughulikii matatizo ya wananchi na badala yake amekuwa
akizunguka bila msaada wowote.
Kinana alisema hayo juzi katika Kijiji cha
Ikengwa, Kata ya Kinyasi wilayani Kondoa baada ya wananchi wa kijiji
hicho kumchongea Nyalandu kwa Kinana kwamba wizara yake inawaua na
kuwaumiza bila ya hatia, hivyo wamechoka.
Wananchi hao walisema mateso wanayoyapata kutoka kwa askari wa
wanyamapori katika Pori la Mkungunero ni makubwa ambayo yanalenga
kuondoa uhai wa watu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Katibu wa CCM wa Kata ya Inyasi, Jusberi Jumanne
aliyesoma risala ya malalamiko hayo, alisema wanaishi ndani ya kijiji
chao na kufanya shughuli zao za kilimo, lakini kila wakati wanachomewa
nyumba, mazao yao kufyekwa na hata kuwasababishia ulemavu na vifo.
“Mheshimiwa katibu mkuu, hapa ni kijiji halali
kilichosajiliwa 1974 na kupewa hati 398, lakini hifadhi hiyo ilikuja
kuweka mipaka yao mwaka 2006, jambo hili sisi tunaona ni uonevu ambao
tunafanyiwa bila ya kushirikishwa na kuambiwa tuhame kwa nguvu na
hatujui mahali pa kwenda,” alisema.
Akijibu hoja hiyo Kinana alionekana kukerwa na
namna maisha ya watu wa maeneo hayo yasivyoshughulikiwa ili nao waishi
kama Watanzania wengine.
“Ni jambo la aibu kwa Waziri wa Maliasili na Utalii kusikia migogoro lakini yeye akawa kimya,”alisema Kinana.
“Nyalandu awaeleza Watanzania kama kuna mahali
amefanikiwa kumaliza kabisa migogoro walau 10 kwani amekuwa ni bingwa wa
maneno na matembezi.”
Kinana alisema ni lazima Nyalandu abebe msalaba
huo kwani roho za binadamu zina thamani… ni heri roho ya binadamu kuliko
mnyama ingawa alizuia wanyama wasiuawe.
“Hawa mawaziri lazima waje, na nina wasihi waje
haraka, yaani Waziri wa Maliasili na Utalii na mwenzake wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi,” alisema.
“Mfano ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye
anafanya kazi ya kuzunguka nchi nzima na maeneo mengine wakati mizunguko
yake haisaidii kuondoa matatizo ya wananchi.”
Kinana alitaka kamatakamata ya wananchi
isimamishwe kwanza hadi ufumbuzi kuhusu mipaka ya pori hilo
itakapoangaliwa upya. Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, Waziri Nyalandu
alisema anakubaliana na alichosema Kinana, lakini akataka watu wajjue
kuwa mgogoro huo ni wa muda mrefu.
“Mgogoro huo ni wa siku nyingi, hivyo busara
inahitajika sana kulinda watu, mali zao na maliasili. Niliunda kamati
ambayo yumo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na Manyara, Ma-RAS (maofisa utawala
wa mikoa) wao na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambayo imefanya
uchunguzi pamoja na kuongea na wananchi,” alisema.
“Kamati inatarajiwa kumaliza kazi wiki hii na
itanikabidhi kwa kuwa mimi ndiye niliyeiunda. Nimepanga kwamba ndani ya
hizi wiki mbili za Bunge, mimi na Waziri wa Ardhi tutatangaza suluhisho
la tatizo hili. Tutaenda pamoja Mkungunero kuongea na wananchi.”
Katika mkutano huo, Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Zabein Mhita
alisema kuwa katika kata hiyo na maeneo mengine kumekuwa na kelele
zinazotishia amani na tayari kwa baadhi ya watu wameshapoteza maisha.
Walimkabidhi Kinana maganda ya risasi pamoja na rundo la mabaki ya nguo zilizochomwa moto na askari wa wanyamapori. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment