Wananchi wametakiwa
kupuuza kauli alizodai kuwa za wapinzani za kuwataka wasishiriki kupiga
kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika Desemba,
mwaka huu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo juzi alipozungumza na wakazi wa Nchingwea mkoani Lindi.
Alisema ni marufuku kwa vyama vya upinzani kuzuia wananchi kupiga kura na kumchagua kiongozi wanayempenda
“Tumepata taarifa kuna wapinzani wameanza
kuwatisha wananchi wasiende kupiga kura siku ya Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa,” alidai Nape.
“Hizi ni salamu kwa wapinzani wenye mpango huo kuwa hatutawaacha, lazima tutawashughulikia.”
Alisema kupiga kura ni haki ya kila mwananchi,
hivyo kitendo cha kuzuia watu ni sawa na kubaka demokrasia, jambo ambalo
CCM haitalivumilia.
Nape alisema CCM imejipanga vizuri na kwamba ina uhakika wa kushinda kwa kishindo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz