Friday, November 14, 2014

NDEGE YA KIJESHI YAANGUKA

Ndege ya kijeshi yaanguka nchini Nigeria.Ndege hiyo ni ya pili kuanguka.
Helikopta ya kijeshi ya Nigeria imeanguka katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo , ikiwa ni helikopta ya pili kupata ajali kwa muda wa chini ya wiki mbili .
Ajali ya hivi karibuni imetokea viungani mwa mji wa Yola, mji mkuu wa jimbo la Adamawa ambako kwa sasa jeshi linahangaika kukabiliana na uasi wa wanamgambo wa Jihad.
Kuna taarifa kutoka jimbo hilo kuwa wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwasukuma wanajeshi nje ya mji muhimu uliopo karibu na mpaka wa Cameroon . Wanafunzi katika chuo kikuu cha Modibbo Adama kilichopo katika mji wa Yola wanasema walisikia Helikopta ikianguka karibu na chuo chao .
Baada ya kuanguka ikafuatiwa na mfulurizo wa milipuko , kwani inaaminiwa kuwa ilikuwa inasafirisha silaha na zana nyingine za kijeshi kwa wanajeshi wanaopigana Boko Haram. Haijawa wazi ikiwa mtu yeyote aliekuwa ndani ya ndege hiyo amenusurika na kifo .
Ndege ya kijeshi yaanguka nchini Nigeria
Baada ya kusikia kelele , baadhi ya wanafunzi walianza kukimbia wakihofia kuwa wapiganaji wa jihad walikuwa wakiwashambulia Hii ni helikopta ya pili ya kijeshi kuanguka katika mji wa Yola wiki hii.
Wakati huo huo katika eneo la kaskazini kuna taarifa kuwa mji wa Mubi hauko tena mikononi mwa Boko Haram baada ya askari na vikosi vya usalama vya eneo hilo, wakiwemo wawindaji kuurejesha tena.
Lakini katika sehemu hii ya kaskazini ya jimbo la Adamawa bado hali ni mbaya na watu wamekuwa wakiukimbia mji huo ambao makundi ya Jihad yamekuwa yakijaribu kuuteka. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 14, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MWANAMKE MZAZI ABAKWA HOSPITALINI


Mwanamke nchini Pakistan
Polisi nchini Pakistan wanawashikilia wanaume watatu kwa kosa la utumizi dawa za kulevya na ubakaji kwa mgonjwa aliyefuata matibabu katika hospitali ya serikali.
Mwanamke huyo, ambaye alijifungua hivi karibuni,alikwenda katika eneo la Burewala Mashariki ya jimbo la Punjab,iliko hospitali hiyo na alikwenda hapo akiwa na mumewe pamoja na mtoto wao mchanga kwa uchunguzi wa kitabibu.
Mume wa mwanamke huyo alimwacha mkewe kitambo kifupi tu na aliporejea eneo alipokuwa ,hakumkuta ila mtoto na begi la mwanamke huyo vimetelekezwa.
Saa kadhaa baadaye,alimpata mkewe akiwa amelala katika chumba chenye kiza ,kilichomo katika hospitali hiyo na kuthibitika kuwa amebakwa .
baada ya fahamu kumrejea mwanamke huyo alisema kwanza alichomwa sindano na wanaume hao watatu kisha wakaanza kumbaka kwa zamu.Wanaume wote hao ni wanafanya hospitalini hapo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

UINGEREZA YAANDAA SHERIA KUDHIBITI IS


Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron

Uingereza inaandaa sheria kupambana na ugaidi, kuzuia ongezeko la Waingereza wanaokwenda kupigana nchini Syria na Iraq.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameelezea kwa mara ya kwanza sheria hiyo inayopendekezwa yenye lengo la kuzuia ongezeko la Waingereza wenye itikadi kali wanaokwenda katika nchi hizo.
Waziri mkuu wa Uingereza ametangaza pendekezo la muswada huo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye bunge la Australia mjini Canberra.
Katika sheria hiyo, amesema polisi wamepewa uwezo mpya kuweza kukamata hati za kusafiria za wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wapya walioandikishwa na kundi la Islamic State, ambao wanajaribu kuondoka nchini humo.
''... Uwezo mpya waliopewa polisi katika bandari kukamata hati za kusafiria, kuwazuia washukiwa kusafiri na kuzuia raia wa Uingereza wanaorejea nchini humo isipokuwa tu wamefuata masharti yetu. Sheria mpya kuyazuia mashirika ya ndege ambayo hayata tii hatua zetu za kuwachunguza wasafiri, kuingia nchini Uingereza. Alisema Cameron.
Sheria hiyo inayopendekezwa pia itayatoza faini mashirika ya ndege ambayo hayatachukua hatua zaidi kuchunguza orodha ya abiria inayowabeba.
Serikali ya Uingereza inatarajia mswada huo utapitishwa kuwa sheria ifikapo mwishoni mwa Januari mwakani. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Thursday, November 13, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS NOVEMBA 13, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MWANAMKE AFUNGWA JELA KWA KUFADHILI ISIS


Amal alimuo9mba rafiki yake kumpelekea mumewe anayepigana nchini Syria pauni 15,800

Mwanamke mmoja nchini Uingereza aliyeshitakiwa kwa kumfadhili mumewe aliyejiunga na vita nchini Syria, amefungwa jela kwa zaidi ya miaka miwili.
Amal El-Wahabi, mwenye umri wa miaka 28, alijaribu kumhadaa rafiki yake kumbebea pauni 15,800 hadi nchini Uturuki ambako mumewe angeweza kuzichukulia.
Jaji aliyetoa uamuzi katika kesi hiyo, Nicholas Hilliard, alimwambia El Wahabai kuwa alifahamu vyema kwamba mumewe Aine Davis alikuwa anapigana nchini Syria na kwa hivyo alikuwa anamsaidia katika harakati zake.
Davis, ambaye alikuwa mlanguzi wa dawa za kulevya pamoja na kushtakiwa kwa kosa la kumiliki silaha, aliondoka Uingereza mwaka 2013 kwenda Syria kupigana na kundi la Isis. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SHELL YADAIWA ILIPUUZA ONYO NIGERIA


Mafuta yaliyovuija yaliathiri mazingira na kusababisha watu kuapoteza kazi.

Mawakili wanaoiwakilisha jamii ya watu walioathiriwa na uchafuzi wa mazingira anasema wakuu wa kampuni ya mafuta ya Shell walijulishwa mapema kuhusu kuchakaa kwa mabomba yake ya mafuta.
Hii ilikuwa kabla ya kutokea kwa visa vya kumwagika mafuta mara mbili hivyo kuchafua pakubwa eneo hilo Lagoniland Kusini mwa Nigeria mwaka 2008.
Shell inakana kwamba ilikuwa na taariifa kuwa mabomba hayo yalihatarisha usalama.
Shell inadai mabomba hayo yalipasuliwa na wezi wa mafuta lakini mawakili hao wamejibu kwamba mabomba hayo yalikwa duni na yalimwaga mafuta hata kwenye ziwa la eneo hilo ambako sasa uvuvi haufanyiki tena. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Wednesday, November 12, 2014

MATUMIZI YA KONDOM YAPUNGUA NCHINI...!!!




Imeelezwa kuwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), yanaweza kuongezeka nchini hasa kwa vijana kutokana na kubainika kupungua kwa kasi ya matumizi ya mipira (kondomu).

Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Florens Turuka katika mkutano wa sita wa kutathmini maambukizi ya VVU nchini.

Dk Turuka alisema maambukizi mapya yameendelea kuwapo kwa sababu vijana hawatumii kondomu kujikinga.

“Matumizi ya kondomu katika jamii yamepungua na kuwafanya watu wengi hasa vijana kupata maambukizi na zaidi ni kutokana na mwamko mdogo kuhusu umuhimu wa kondomu kama kinga ya Ukimwi,” alisema. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SITTI MTEMVU KUVUA TAJI LA MISS TEMEKE NA MISS CHANG’OMBE


HAIJAKAA sawasawa! Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji la Miss Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu umri wake, wadau wamemwangushia uwajibikaji  mwingine wakimtaka avue mataji mengine mawili.
 
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu.
Baadhi ya wadau wa sanaa waliozungumza na Risasi Mchanganyiko Jumatatu iliyopita jijini Dar walisema kama kweli Sitti ana dhamira safi ya kukwepa kusakamwa basi ni bora kwake akavua na mataji ya Miss Chang’ombe na Miss Temeke ambayo ndiyo yaliyompa tiketi ya kwenda kambi ya Miss Tanzania na kushinda. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 12, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WAUMINI WAMZUIA ASKOFU MKUU ASIINGIE OFISINI KWAKE...!!!




  Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania, Alinikisa Cheyo


Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania, Alinikisa Cheyo amezuiwa na waumini wa kanisa hilo kuingia katika ofisi yake iliyopo Jakaranda, Mbeya kwa saa 18.
Cheyo, ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, alifungiwa mlango na waumini wa kanisa hilo Usharika wa Jakaranda kumzuia asiingie mpaka atakapoitisha mkutano na kumrudisha Mchungaji Nosigwe Buya ambaye alimhamisha.
Akizungumzia hatua hiyo mbele ya waumini wengine, Mchungaji wa usharika huo, Jamson Mwilugumo alisema walifunga mlango huo kushinikiza Askofu Cheyo abadili msimamo wa kumwondoa Mchungaji Buya na kumrejeshea wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya jimbo hilo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HII NDIO SAA GHALI ZAIDI DUNIANI

Saa ghali zaidi duniani iko Uswiss
Saa ghali zaidi duniani imenunuliwa mnadani huko Geneva,Uswiss kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 21.3.
Saa hiyo imetengenezwa kwa kutumia karati ishirini na moja za dhahabu na ina uzito wa nusu kilo,saa hiyo iliyoundwa kwa mbwembwe ilitengenezwa mahsusi kwa ajili ya mtoto wa mfanya biashara,Henry Graves mnamo mwaka 1930.
Na ilimchukua miaka nane kwa watengeneza saa maarufu wa Uswis kuikamilisha hiyo saa ghali ambaye ni Patek Philippe.
Saa hiyo ilinunuliwa siku mbili tu baada ya mmiliki wa mwisho kufariki dunia kutoka falme za kiarabu Saud Bin Mohammed Al-Thani.
Mmiliki huyo alikuwa na madeni mengi ambayo yangemgharimu nyumba yake kuuzwa na hivyo akaikabidhi saa hiyo kwenye nyumba ya mnada ya Sothebys. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WATU WATATU WACHINJWA KISA MAONI WALIYOTOA KWENYE MITANDAO

Mjini Derna, kundi la Is limeshika hatamu
Wanaharakati watatu wa kisiasa nchini Libya wamechinjwa baada ya kuandika katika mitandao ya kijamii juu ya maisha chini ya utawala wa dola ya kiislam.Miili yao ilipatikana mapema wiki hii mashariki mwa mji wa Derna karibu na Benghazi.
Tukio hilo lilianzia kwa wanaharakati hao kutekwa mapema mwezi huu.Mji huo wa Derna uko chini ya mamlaka ya kikundi cha dola ya kiislam tangu mwaka 2012 ambacho kimekiri kuwa sehemu ya kundi la is.
Mnamo mwezi August mwaka huu katika video ilooneshwa katika mitandao ya kijamii ilionesha mwanamume mmoja akipigwa risasi na kufa hadharani katika viwanja vya mpira mjini Derna.
Siku za hivi karibuni kuna picha iloachiliwa mitandaoni ikionesha kikundi cha kijamii kinachojiita mahakama ya kiislam. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

CAF YAIENGUA MOROCCO AFCON 2015

moroc
Timu ya Taifa ya Morocco imeondolewa katika michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2015, kutokana na maamuzi ya nchi hiyo kujitoa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo yaliyotarajiwa kuanza Januari mwakani, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limethibitisha leo baada ya kukutana jijini Cairo, Misri jana.


Nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika ilifikia maamuzi ya kujitoa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya Bara la Afrika kwa kuonesha hofu ya kuenea kwa Ebola, ugonjwa ambao umelipuka Magharibi mwa Afrika. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Tuesday, November 11, 2014

POLISI YAWATAWANYA WAFUASI WA MBOWE KWA MABOMU


Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), Freeman Mbowe 

Wafuasi wa (Chadema) wilayani Mpanda jana jioni walilazimika kutafuta vichochoro vya kukimbilia baada ya polisi kusambaratisha kwa mabomu ya machozi, maandamano ya kumsindikiza Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe baada ya mkutano.

Patashika hiyo ilitokea baada ya mkutano wa Mbowe kumalizika na wafuasi wake kutaka kumsindikiza hotelini, jambo ambalo polisi hawakulikubali.

Baada ya wananchi hao kuanza maandamano hayo, polisi walifyatua mabomu takriban 15 yaliyowafanya wafuasi wote kutawanyika na kusababisha taharuki miongoni mwa wakazi wa mji huo. Dakika chache baada ya tukio hilo, umeme ulikatika mji mzima.

Tofauti na maeneo mengine aliyofanya ziara zake kama Tabora, Sikonge na Igunga ambayo wafuasi walikuwa wakimsindikiza, polisi wa Mpanda walijipanga ipasavyo tangu mapema kuhakikisha hali hiyo haitokei. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...