Watafiti nchini Australia wanadai kwamba dawa inayotumiwa kuongeza nguvu za kiume VIAGRA husababisha upofu baada ya mda mrefu.
Kulingana
na Watafiti hao kutoka Australia, kiungo fulani katika dawa hiyo
inayotumiwa kukabiliana na ukosefu wa nguvu za kiume,huathiri uwezo wa
kuona miongoni mwa wanaume ambao wana ugonjwa wa macho.
Kulingana
na gazeti la Nation nchini kenya,Madaktari nchini Australia wamebaini
kwamba kiungo fulani katika dawa hiyo kinaweza kusababisha upofu
miongoni mwa wanaume wenye tatizo la ugonjwa wa macho.
Vilevile inadaiwa kuwa dawa hiyo pia inaweza kuwaathiri watumiaji ambao wanaona vizuri.
Utafiti huo uliofanywa katika panya,ulibaini kwamba hata watu wasio na ugonjwa wa macho wanaweza kuathirika. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC