1 — Mechi zote za Kombe la Dunia 1930 nchini Uruguay zilichezwa kwenye jiji moja: Montevideo.
2 — Beki wa Sweden, Jan Olsson, alikuwa akivaa jezi namba 2, beki huyo ndiye aliyemdhibiti vilivyo nyota wa Uholanzi, Johan Cruyff aliyekuwa akisifika kwa aina yake ya ugeukaji na kuwatoroka mabeki “Cruyff Turn” kwenye fainali za mwaka 1974, Ujerumani Magharibi.
3 — Gwiji wa Brazil, Pele ni mchezaji pekee aliyetwaa makombe matatu ya dunia akiwa anacheza mwaka: 1958, 1962 na 1970.
4 — Idadi ya wachezaji waliofunga mabao matatu katika mechi mbili za Kombe la Dunia: Mhungary Sandor Kocsis (zote mwaka 1954), Mfaransa, Just Fontaine (1958), Mjerumani, Gerd Muller (1970) na Gabriel Batistuta (moja 1994 na moja 1998).
5 — Mshambuliaji wa Russia, Oleg Salenko ndiye anayeshikilria rekodi ya kufunga mabao matano katika mechi moja ya Kombe la Dunia, wakati Russia waliposhinda 6-1 dhidi ya Cameroon fainali za 1994 nchini Marekani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz