Sunday, June 08, 2014

ANGALIA PICHA ZA HARUSI YA MBUNGE JOSHUA NASSARI ILIVYOFANA



2_31d12.jpg
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Samwel Nassari jana amefunga ndoa na Anande Nko kwenye Kanisa la Pentekoste lililopo Kilinga, Arumeru jijini Arusha ikifuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hoteli ya Ngurdoto.
Sherehe hiyo ilianza saa 7:00 mchana  ambapo watu wote walialikwa wakiwemo ndugu, marafiki, jamaa na wananchi wote wa Arumeru Mashariki ambao wamepiga 'mpunga' wa kutosha na vinywaji hadi kila mtu akaondoka akisema 'Nassari ameacha historia'. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
CHANZO: Mitandao ya Kijamii.

RAIS MPYA WA MISRI KUAPISHWA

Raia wanaomuunga mkono Abdel Fatah al sisi
Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Misri, Cairo kabla ya kufanyika kwa sherehe ya kumuapisha rasmi rais mpya wa taifa hilo Abdel Fatah el Sisi.
Rais huyo mteule atakula kiapo chake cha kuchukua mamlaka katika mahakama kuu ya kikatiba mjini Cairo.
Alishinda uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita kwa wingi wa kura ijapokuwa idadi ya waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo ilikuwa chini ya asilimia 50.
Uchaguzi huo unajiri miezi michache tu baada ya kiongozi huyo kumpindua madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Mkuu huyo wa jeshi wa zamani ameanzisha msako dhidi ya wanaompinga mbali na kukipiga marufuku chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

Saturday, June 07, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 07, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUAGIZA MAITI IKATWE MIGUU...!!!


Mwandalizi mmoja wa mazishi nchini Afrika Kusini, anayedaiwa kuwaagiza wafanyakazi wake kuikata miguu ya maiti moja aliyodai kuwa ndefu sana alifikishwa mahakamani Ijumaa.
Ronel Mostert anayemiliki chumba cha kuhifadhi maiti ambacho pia huendesha shughuli za mazishi, alitoa amri hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa maiti hiyo ingetosha katika jeneza. Anakabiliwa na kosa la kumkata miguu maiti.
Mfanyakazi mmoja aliimbia mahakama kuwa Ronel alimuagiza kuchukua kifaa kimoja cha kukata ili kuikata miguu hiyo ya marehemu na kwamba jambo hilo limekuwa likimsumbua sana kimawazo.
Mwili marehemu ulifukuliwa ili kusaidia katika uchunguzi wa polisi.Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC

MADEREVA WA UMMA WAGOMA BRAZIL

Mgomo wa wafanyakazi hao umesababisha uhaba wa magari ya usafiri
Maafisa wa polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika siku ya pili ya mgomo wa wafanyikazi wa sekta ya uchukuzi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa usafiri wa uma katika mji wa Sao Paulo.
Takriban nusu ya vituo vya treni vilifungwa na kusababisha msongamano mkubwa wa watu katika barabara za mji huo mkubwa ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe la dunia kuanzia alhamisi ijayo.
Wafanyakazi hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi.
Awamu nyengine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo utaendelea kwa mda usiojulikana. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC

MWEGANE YEYA WA MBEYA CITY AAHIDI MAKUBWA TAIFA STARS, AMSHUKURU MUNGU KWA KUITWA NA MART NOOIJ


Mwagane-Yeya.pngnnnnnnnnnnnnnnNa Baraka Mpenja, Dar es salaam
MSHAMBULIAJI hatari wa Mbeya City fc, Mwegane Yeya amefurahishwa na kitendo cha kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij.
Akizungumza na mtandao huu, Mwegane amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kupata nafasi hiyo kwasababu Tanzania ina wachezaji wengi wenye viwango vya hali ya juu, lakini amechaguliwa yeye.
“Hii ni nafasi nyingine muhimu kwangu. Niliwahi kuitwa katika kikosi cha Young Future Taifa Stars na Kim Poulsen, lakini sikufanya vizuri kwasababu nilikuwa majeruhi. Naamini kwasasa nitaitumia vizuri nafasi hii”. Alisema Mwegane ambaye ni hatari kwa kufunga magoli ya kichwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, June 06, 2014

WARIOBA AZISHUKIA UKAWA NA CCM


Katika Bunge hilo, wajumbe wengi wa CCM walimshambulia Warioba na tume yake wakidai kuwa Rasimu ya Pili ya Katiba haikuzingatia maoni ya wananchi na Mabaraza ya Katiba. PICHA|MAKTABA 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashauri wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na CCM kuacha kuzunguka mikoani kufanya mikutano inayoeleza misimamo yao kuhusu mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa haina tija kwa taifa.
Ameonya kuwa mikutano hiyo inajenga mwelekeo mbaya kwa taifa na kuhatarisha mchakato wa Katiba na kuzitaka pande hizo kumaliza tofauti zao.
Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Warioba alisema: “Kwa mustakabali mwema wa taifa, ni muhimu makundi haya ‘ya-resolve’ (yamalize), matatizo yaliyopo kabla ya Agosti, ili Bunge Maalumu la Katiba likirejea, wote washiriki na kukamilisha mchakato wa kupata Katiba Mpya. Hili ni kwa masilahi ya taifa.”
Kauli ya Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu, imekuja huku makundi ya Ukawa linaloundwa na wabunge wengi wa upinzani na viongozi wa CCM wakiendelea kung’ang’ania misimamo yao kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Wakati CCM ikipinga mapendekezo ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu uliomo kwenye Rasimu, Ukawa unaunga mkono mapendekezo hayo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TIGO, AIRTEL NA ZANTEL ZAUNGANISHA HUDUMA




Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo, Diego Gutierrez (Kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Muhula wakitia saini ya makubaliano jijini Dar es Salaam jana baina ya Tigo na DTBi ya kusaidia wajasiriamali kujifunza teknolojia ya digitali na mawasiliano. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Hassan Mshinda. Picha na Venance Nestory.


Kampuni za simu za mkononi za Tigo, Airtel na Zantel zimeunganisha huduma zao za kutoa, kutuma na kuweka fedha na sasa mteja anaweza kutuma fedha kutoka mtandao mmoja kupitia mwingine.

Taarifa ya pamoja na kampuni hizo iliyotolewa jana, ilisema kuwa wote wanaotumia huduma za kifedha za mitandao hiyo, wataweza kutumiana fedha kupitia simu zao za mikononi pasi na tatizo baada ya kampuni hizo kuunganisha huduma zao.

Huduma hiyo inayotarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu, itawafanya wateja wa mitandao hiyo kutumiana na kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao tofauti na ilivyokuwa awali. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 06, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MTAWA WA KANISA KATOLIKI ASHINDA KATIKA SHINDANO LA KUIMBA...!!!

Mtawa wa Italia anyakua ushindi
Mtawa mmoja kutoka Italia ambaye alipata umaarufu katika mtandao wa kijamii ameshinda shindano la kuimba nchini humo. Mtawa huyo, Sister Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika televisheni kushiriki shindano la The Voice.
Scuccia aliyeonekana amevalia mavazi yake ya utawa na msalaba shingoni, alijawa na furaha na kumshukuru Mungu kwa kumfikisha katika ushindi huo. Mtindo wake wa wimbo wa Alicia Keys, kwa jina 'No One', umetizamwa zaidi ya mara milioni 50 katika mtandao wa You Tube tangu auimbe.
Mtawa huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema kuwa aliamua kushiriki mashindano hayo kufuata ushauri wa Papa mtakatifu Francis, kuwa kanisa liwakaribie zaidi watu wa kawaida. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC Swahili

DRC YAILAUMU RWANDA KWA KUWALINDA M23




DRC yailaumu Rwanda kuwalinda M23
Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeikashifu serikali ya Rwanda kwa kuwalinda wapiganaji wanaotuhumiwa kwa kusababisha mauaji ya halaiki chini ya nembo ya wapiganaji wa M23.
Afisa mmoja wa Serikali ya DRC ameiambia BBC kuwa imekuwa vigumu kwa serikali yake kuwahoji zaidi ya wapiganaji 500 ambao wamekita kambi nchini Rwanda licha yao kutuma ombi la kufanya hivyo yapata miezi saba iliyopita . Zaidi ya watu 800,000 walitoroka makwao haswa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo wakati wa mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe.

Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo na kusema kuwa imeshirikiana na serikali ya DRC. Kundi hilo la M23 lichukua silaha mashariki mwa DRC kuanzia Aprili 2012, liliaumu serikali ya Kinshasa kwa kuwabagua jamii ya watutsi na pia kupuuza makubaliano ya awali ya kusitisha mapigano. Kundi hilo hata hivyo lilishindwa katika mapigano yaliyoongozwa na jeshi la Umoja wa mataifa likisaidiwa na majeshi ya serikali ya Congo mnamo November 2013. Wapiganaji hao walitorokea Rwanda na Uganda.


DRC yailaumu Rwanda kuwalinda M23
Katika mji wa Ngoma, mashariki mwa Rwanda mwandishi wetu alikumbana na wapiganaji hao ana kwa ana katika kambi nje ya mji. Wengi wao wanasema kuwa wamechoshwa na ngoja ngoja hiyo ambayo imedumu kwa kipindi kirefu sasa na wanasema kuwa wangependa kuomba hifadhi nchini Rwanda, kwani wanahofia kurejea ndani ya Congo.
 Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Serikali ya Congo imetangaza kuwa itawapa msamaha wapiganaji hao. Tulipoingia ndani ya kambi hiyo ,hali na taswira ilikuwa tulivu na shwari. Kulikuwa na hema kubwa nyeupe, majengo kadha mbali na bustani iliyolindwa na nadhifu. Wapiganaji hao wanalala sita katika chumba kimoja .

Thursday, June 05, 2014

G7 WAKUTANA BRUSSELS BILA URUSI

mkutano wa G7
Viongozi wa mataifa tajiri ya magharibi wanaokutana mjini Brussels wamesema kuwa wako tayari kuweka vikwazo zaidi kwa Urusi iwapo itaendelea kuvuruga amani mashariki mwa Ukrain. Taarifa ya pamoja ya mataifa ya G7 imesema kuwa Mambo yanayofanywa na Urusi nchini Ukrain hayawezi kubalika kamwe na lazima yakomeshwe.
Huu ndio mkutano wa kwanza wa viongozi hao tangu waifukuze Urusi kama mwanachama.
Urusi ilibumburushwa kutoka G7 kwa kosa lake kubwa zaidi, kuinyakua Crimea kutoka Ukrain. Viongozi wa mataifa hayo ya G7 wanakutana sasa kwa mara ya kwanza tangu wakati huo.
Ukrain vita vimechacha
Lakini huku wakikutana mapigano yamechacha kati ya serikali ya Ukrain na majeshi yanayo unga mkono Urusi mashariki mwa Ukrain. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Urusi imeendelea kukana kuhusika na mapigano hayo. Miongoni mwa mikutano iliyopangwa Alhamisi hii, waziri mkuu wa Uingereza Davin Cameron atakutana na rais Obama mjini Brussels, ambapo kwa upana zaidi watazungumzia Urusi. Kisha baada ya mkutano huo, David Cameron ataelekea Paris Ufaransa kwa mkutano wa faragha na rais wa Urusi Vladmir Putin.

D-Day barani Uropa

Katika wiki hii mataifa ya Uropa yamekuwa yakiadhimisha siku ya kuikomboa bara Uropa kutoka utawala wa ki Nazzi katika vita vya pili vya dunia miaka 70 iliyopita. Huku hayo yakitokea, juhudi za kidiplomasia zimeshika kasi miongoni mwa mataifa ya magharibi kumaliza uhasama kati yao na Urusi.
G7 wamepongeza uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Ukrain na wameirai Urusi kumpokea na kushirikiana na rais mpya wa Ukrain Petro Poroshenko. Pia wameonya kuwa hawatasita kuiwekea Urusi vikwazo zaidi iwapo itakataa kusaidia kurejesha uthabiti Ukrain. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa miaka 17 ambapo G7 inakutana bila Urusi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JUNI 05, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Wednesday, June 04, 2014

ANGALIA MSAFARA WA RAIS WA KENYA UNAVYOKUWA BAADA YA KUPEWA KITISHO CHA KUUAWA NA AL- SHABAAB

Screen Shot 2014-06-04 at 9.53.41 AM 
Imefaamika kuwa baada ya kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab cha Somalia kutoa onyo kwamba mashambulizi yake yanayofata yatawahusu viongozi wa Kenya, imebidi system ya ulinzi wa rais kwenye msafara ibadilike.
Mabadiliko yalianza kuonekana toka mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye sherehe za 51 za kujitawala ambapo badala ya Rais kutumia gari aina ya Land rover iliyo wazi iliyokua pia ikitumika na marais wa awali, rais aliiingia kwenye uwanja wa michezo wa Nyayo na gari aina ya Land cruiser iliyo na vioo visivyo penya risasi.
Screen Shot 2014-06-04 at 9.53.52 AM 
Hiyo Land Cruiser ililoongozwa na gari lenye mitambo iliyo na uwezo wa kugundua bomu kwa zaidi ya kilomita 10, nyuma kabisa kulikua na gari lililo na uwezo wa kuhimili risasi na bomu au kilipuzi cha aina yoyote na inasemekana kwamba gari hilo huwa linatumika endapo msafara wa Rais umeshambuliwa kwa haraka Rais na wakuu wengine wanaondolewa na gari hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 04, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...