Timu
ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa kuvuka hatua ya kwanza
ya michuano ya kuwania kucheza michuano ya kombe la mataifa huru ya
Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani.
Stars leo ilikuwa inacheza Zimbwabwe kwenye mchezo wa marudiano baada
ya kuwafunga Zimbwabwe 1- 0 uwanja wa taifa wiki moja iliyopita, kwenye
mchezo huo Stars imefanikiwa kufuzu baada ya kulazimisha sare ya 2-2.
Zimbwabwe walianza kufunga dakika ya 24, kabla ya Stars kusawazisha dakika kadhaa baadae kupitia Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 28.
Muda mchache baadae Thomas Ulimwengu aliongezea Tanzania bao la pili
dakika ya 46, kabla ya dakika 10 baadae Zimbwabwe kusawazisha na
kufanya matokeo 2-2.
Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki 2-2, na sasa
Tanzania wanaingia hatua ya pili ambapo watacheza na Msumbiji. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz