Kampuni kubwa ya kutengeza magari nchini Marekani imeagiza magari milioni 1.4 yarejeshwe kutokana na hitilafu ya usukani.
Takriban magari milioni 1.1 yaliyoundwa kwa
mtindo wa kispoti yaliyokuwa yameuzwa Marekani Kaskazini yametakiwa
kurejeshwa kwani huenda yana hitilafu kwenye usukani.Vilevile magari mengine 200,000 yenye muundo wa Taurus yaliyoundwa kati ya mwaka wa 2010 na 2014 huenda yakakumbwa na tatizo ya kushika kutu kwa haraka.
Matukio kama hayo yaliyofanyika majuzi huenda yakaifanya kampuni hiyo kuvunja rekodi ya kutaka magari mengi zaidi yarejeshwe katika kipindi cha mwaka mmoja.
Dosari hiyo imehusishwa na vifo 13, ingawa wasanifu wa Marekani wanaamini kuwa idadi hiyo itaongezeka.
Pindi tangazo hilo lilipofanywa, kampuni za kutengeneza magari hayo pamoja na wasanifu wa Marekani wameongeza juhudi za kurejesha magari ambayo yanapatikana kuwa na dosari. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment