Dar es Salaam/Mwanza. Rais Jakaya Kikwete
ameshauriwa kunusuru mchakato wa kupata Katiba Mpya ili usisimame kwa
kuvua koti la Uenyekiti wa CCM na kubaki na Urais ili awaeleze wananchi
nini cha kufanya kupata Katiba Mpya.
Ushauri huo umetolewa na viongozi mbalimbali wa
vyama vya siasa na wasomi walioshiriki katika mdahalo wa Katiba
uliofanyika jijini Dar es Salaam na Mwanza jana. Walisema kuwa Rais ana
wajibu kuunusuru mchakato huo kwa kuwa yeye ndiye aliyeuvuruga kwa
hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge Maalumu la Katiba iliyoonekana kuelemea
upande wa chama chake CCM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete amekuwa
kigeugeu juu ya Muundo wa Serikali za Muungano kama zilizopendekezwa
kwenye Rasimu ya Kwanza na ya Pili ya Katiba.
Alisema kuwa Rais Kikwete alionyesha wazi
kukubaliana na Muundo wa Serikali tatu, kwani kabla Rasimu ya Pili ya
Katiba haijapelekwa kwenye Bunge Malaumu la Katiba ili kujadiliwa,
alisaini kuonyesha kuwa amekubaliana na yaliyopendekezwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz