Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana
alijikuta katika wakati mgumu wakati alipokuwa waziri wa kwanza
kuhusishwa na tuhuma za ufisadi wa kutumia vibaya madaraka yake na
lawama lukuki kuhusu kasoro za kiutendaji katika wizara anayoiongoza.
Mawaziri
wengine wamekuwa wakiwekwa kitimoto kutokana na tuhuma za utendaji mbovu
na udhaifu kwenye wizara zao, lakini hali ilikuwa tofauti jana wakati
Waziri Kivuli wa Ardhi, Halima Mdee aliposoma hotuba ya kurasa 77 ya
upinzani kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, huku kurasa 30 zikielekeza tuhuma kwa waziri huyo.
Miongoni
mwa tuhuma zilizotolewa dhidi ya waziri huyo ni pamoja na kujinufaisha
kupitia mgogoro wa ardhi katika eneo la Chasimba na kiwanda cha Saruji
cha Wazo Hill jijini Dar es Salaam.
Mdee,
ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alimhusisha waziri huyo na ufisadi katika
kazi ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa masuala ya ardhi, uliogharimu
Sh700 milioni. Tuhuma hizo zilimchanganya Waziri Tibaijuka kiasi kwamba
wakati akitoa majibu alijikuta akitoka nje ya mada na kumshambulia
Mdee, huku Spika Anne Makinda akimrudisha kila mara na kumtaka ajikite
kwenye hoja na kuacha kushambulia wapinzani.
Waziri Tibaijuka pia alidai hotuba ya upinzani ilijaa uongo na kumtaka Spika Makinda kumchukulia hatua Mdee. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Akisoma
maoni ya Kambi ya Upinzani bungeni jana, Mdee alisema utafiti huo
ulikuwa na timu ya watu 140 kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo, sekta
binafsi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alisema
waziri huyo anatuhumiwa kuingilia mchakato huo kwa kuingiza jamaa zake
na taasisi ambazo ana uhusiano nazo kama sehemu ya kikosi kazi cha
utafiti kwa jina la wataalamu washauri.
"Matokeo
yake, Idara ya Uchumi ya UDSM ilitumika kama chambo huku kiasi kikubwa
kikimrudia mwenyewe kwa mlango wa nyuma," alisema Mdee.
"Ilifika
hatua wataalamu walimsusia kazi waziri kutokana na kuwepo ujanja ujanja
katika masuala ya fedha, hivyo kumlazimu waziri kujifungia na wasaidizi
wake kukamilisha kazi iliyobaki."
Kadhalika
Mdee alimtuhumu Tibaijuka kwamba ana uhusiano na Taasisi ya Tanzania
Women Land Access Trust (TAWLAT) ambayo ililipwa kiasi cha Sh300 milioni
kutoka Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kutoa elimu na kuendesha
mazungumzo kwa diplomasia, kati ya viongozi na wananchi wa Chasimba
kuhusu mgogoro wa ardhi.
"Licha ya
kulipwa fedha hizo, TAWLAT haikufanya kazi yoyote ya uthamini katika
eneo la Chasimba, badala yake aliyekuwa mkurugenzi wa upimaji, mthamini
mkuu wa serikali pamoja na wataalamu wa wizara walikuja kuniomba
niwatulize wananchi waliokuwa wanawarushia mawe kwa kuwa hawakuwa na
imani na viongozi hao," alisema Mdee.
Mdee,
ambaye pia ni mbunge wa Kawe (Chadema), aliitaka Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuichunguza TAWLAT kuhusu ushiriki wake
aliosema una shaka katika kazi kadhaa za Wizara ya Ardhi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment