Rais Joyce Banda wa Malawi akipungia wafuasi wake waliokusanyika huko Lilongwe wakati wa uzinduzi wa kampeni yake.
Mahakama
kuu inapanga Ijumaa kutoa maamuzi kama iwapo matokeo ya uchaguzi
yatangazwe hadharani au kura zihesabiwe tena. Matokeo ya awali
yamemuweka Bi. Banda nyuma ya mpinzani wake Peter Mutharika.
Bi.Banda anasema uchaguzi ulijaa ubadhirifu, ikiwemo pamoja na wizi wa kura na watu kupiga kura zaidi ya mara moja.
Ameliambia
shirika la habari la reuters kwamba atakubali maamuzi ya mahakama kuu,
akifahamu fika kuwa amejaribu kutetea haki za wamalawi kwa kuhakikisha
kuwa kiongozi anachaguliwa kwa haki na utaratibu wa heshima. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Bi.Banda
ameamuru uchaguzi mpya uitishwe katika kipindi cha siku 90 na kusema
hatakuwa mgombea. Lakini mahakama kuu imebatilisha maamuzi yake pale
chama kikuu cha upinzani kilipowasilisha malalamiko.
CHANZO:VOA