Kwa ufupi
Hayo aliyasema jana katika Ibada maalumu ya
kumsimika rasmi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu
Mathias Mulumba lililopo Mjini Songea ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya
waumini, viongozi wa chama na Serikali, viongozi wa madhehebu ya dini
pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne
Makinda.
Songea. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la
Songea, Damian Dallu amesema Katiba Mpya itapatikana iwapo wajumbe wa
Bunge la Katiba watakuwa na maadili ya kiroho kwa kufuata maagizo ya
Mwenyezi Mungu bila kupindisha ukweli wa mchakato wa maoni ya Katiba.
Amesema kupotosha ukweli wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba unaweza kuipeleka nchi kubaya.
Hayo aliyasema jana katika Ibada maalumu ya
kumsimika rasmi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu
Mathias Mulumba lililopo Mjini Songea ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya
waumini, viongozi wa chama na Serikali, viongozi wa madhehebu ya dini
pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne
Makinda. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz