Baadhi ya vijana waliohudhuria mkutano huo |
Lipumba wa CUF akisisitiza jambo |
Mchungaji Msigwa wa Chadema |
Danda Juju wa NCCR-Mageuzi
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz |
Frank Nyalusi (Diwani wa Kata ya Mivinjeni |
Profesa
Lipumba aliuliza swali hilo mara tu baada ya kupanda jukwaani katika
uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa kuhutubia mkutano wa Ukawa uliolenga
kufafanua mchakato mzima wa katiba ulivyo hivisasa na kutafuta ushawishi
wa wananchi kupinga kile kinachoendelea katika bunge hilo.
“Vijana
mnaonekana kama wazee kwasababu ya hali ngumu ya maisha na leo
mnahujumiwa kupata Katiba mpya itakayoletea matumaini kwa watanzania
wote; itakayozungumzia haki za msingi, haki za kupata elimu, afya, kazi
na zingine” alisema
Alisema
uamuzi wao wa kuanzisha Ukawa ulikuja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
kuteka nyara mchakato mzima kwa kutupilia mbali mapendekezo ya wananchi
kupitia rasimu ya pili ya Katiba na kuingiza mambo yao kwasababu ya
wingi wao katika bunge hilo.
Awali
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema)
alisema hawatarudi katika bunge hilo mpaka pale wabunge wa bunge hilo
watakapokuubali kuijadili Rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba
iliyowasilishwa bungeni hapo badala ya mapendekezo mapya kutoka kwa CCM.
“Mapambano ya kudai katiba sio ya watu wanaojificha, sio ya watu waoga,
ni ya watu walio tayari kujitoa kwa gharama yoyote ile,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Mchungaji Msigwa alisema kama Zanzibar wana nchi yao na hakuna mtu
aliyepiga kelele kwa maamuzi hayo kwanini Tanganyika isiwe na nchi yake.
Alisema
muungano wanaoutaka Ukawa ni ule wa serikali tatu uliopendekezwa na
wananchi kwa kupitia maoni yao waliyotoa kwa tume hiyo.
Profesa
Lipumba alisema suala la Katiba sio suala la mzaha kama linavyofanywa na
wabunge wa CCM kwasababu linazungumzia haki za msingi za watanzania.
Alisema
CCM na wabunge wake wamekuwa wakipinga mapendekezo ya serikali tatu
yaliyotolewa na tume hiyo kwa kisingizio cha gharama jambo ambalo halina
utafiti wa kutosha.
Alisema:
“tatizo la nchi hii sio serikali tatu, tatizo la nchi hii ni matumizi
mabaya ya fedha za umma, rushwa, ufisadi, misamaha holela ya kodi na
ukubwa wa serikali.
Alisema
hayo yote yakifanyiwa kazi kama ambavyo wabunge wapinzani wamekuwa
wakipiga kelele bungeni, kisingizio cha kwamba serikali tatu zitaongeza
gharama hakitakuwepo.
Alisema
rasimu ya Katiba iliyosainiwa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya
kujadiliwa na bunge hilo kabla ya kupelekwa kwa wananchi ina mambo mengi
yanayolenga kuboresha ustawi wa taifa hili lakini inapingwa na baadhi
ya wanaCCM kwa nguvu za mafisadi.
“Ndugu
zangu tunazunguka nchi nzima kuwaeleza watanzania jinsi mchakato
ulivyohujumiwa na wanavyotakiwa kujipanga kukataa hila hizo; ni lazima
tuwe macho, nchi imekamatwa na mafisadi na wala rushwa ambao hawataki
mianya hiyo izibwe kwa kupitia katiba mpya,” alisema.
Alisema
rasimu hiyo inazungumzia uadilifu ambao ni changamoto kubwa kwa baadhi
ya viongozi tulionao, inazungumza kupunguza madaraka ya Rais, ukubwa
serikali na umuhimu wa wabunge kutokuwa mawaziri, mambo ambayo
hayakubaliki na wengi wa CCM.
Awali
Sheikh Rajab Kitimba wa Shura ya Imam alisema wameamua kuingia katika
kundi la Ukawa ili kusaidia kumaliza kilio cha wananchi.
“Ni sawa
na kufanya ibada za kijamii, ibada nje ya nyumba za ibada, kwasababu
huko ndiko kwenye asilimia 75 ya watu wa dini mbalimbali wenye msiba
tunaotaka kuumaliza kupitia ukawa,” alisema.
Alishangaa sababu ya tume ya Warioba kupewa ridhaa na kutumia fedha
nyingi za walipa kodi kwa kazi ambayo mwisho wa siku inakataliwa na
wachache.
“Zanzibar, Tanganyika na serikali ya shirikisho ndio mpango mzima; Ukawa
ni matumaini yetu na nyinyi mkiiunga mkono kazi ya kupata katiba ya
wananchi badala ya ile ya wachache itakuwa nyepesi, tukatae hila, na
ghiriba zinazopinga maoni ya wananchi,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Danda
Juju wa NCCR-Mageuzi alisema pamoja na mchakato huo kuhujumiwa bado
watanzania wana uwezo wa kukataa na hatimaye kupata katiba wanayoitaka. (CHANZO: BONGO LEAKSBLOG)
No comments:
Post a Comment