Monday, January 06, 2014
Saturday, January 04, 2014
HAWA HAPA NDIO WALIOPENDEKEZWA NA CHADEMA ILI WATEULIWE NA RAIS BUNGE LA KATIBA
Kamati Kuu CHADEMA leo kimewapendekeza Prof. Abdallah Safari, Mabere
Marando, Nasra Juma Baruan na Method Kimomogolo ili wateuliwe na Rais
Bunge la Katiba.
Professor Abdallah Safari ni mwanasheria nguli
wa chama hicho na pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani. Huku
Method Kimomogolo ni mwanasheria maarufu wa Chama hicho ambaye ameongoza
kesi nyingi zilizokwishafunguliwa dhidi ya Chadema na viongozi wake.
Wasifu wa Mabere Marando kila mtu anaujua kwani ni nguli aliyeongoza
Mageuzi Tanzania tokea kabla ya mfumo wa vyama vingi. Kwa sasa ni mjumbe
wa Kamati Kuu Chadema na ni mmoja wa wanasheria wake huku akiwa pia
Makamu Mkiti wa Chadema Kanda ya Pwani.
Rais anatarajiwa kuteua
majina mawili tu kutoka Chadema na kwa mujibu wa sheria ni sharti katika
wateuliwa hao mmoja atoke Zanzibar na pia lazima mmoja awe mwanamke.
TAZAMA JINSI MWILI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI, DK. WILLIAM MGIMWA ULIVYOWASILI NCHINI UKITOKEA AFRIKA KUSINI
Mwili
wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa umewasili nchini kwa
ndege ya shirika la Kenya (KQ) na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa
chama na Serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue pamoja na Mawaziri mbalimbali na Wabunge.
Ndege
iliyobeba mwili wa marehemu William Mgimwa ikiwasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar majira ya saa 7.45 mchana.
Gari maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kubeba mwili wa marehemu.
MOTO MKUBWA WAZUKA JANCO MOTEL JIJINI MBEYA JANA USIKU
Moto mkubwa umezuka katika hotel ya Janco forest mpya jijini Mbeya chanzo cha moto hakijajulikana mpaka tunaondoka katika tukio hilo |
Friday, January 03, 2014
"SARAFU YA TSH. 50,000 HAITATUMIKA KATIKA MANUNUZI" PROF. NDULU
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo
iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa
ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa
kulipia malipo ya aina yoyote.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
WACHINA WENGINE WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO 81 BANDARINI DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA UMMA
Mamlaka
ya Bandari Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii
pamoja na vyombo vingine vya Dola, tarehe 2 Januari 2014 majira ya saa
tatu asubuhi kwenye Bandari ya Dar es Salaam, imekamata meno 81 ya tembo
yenye uzito wa kilo 303 sawa na tembo 41. Aidha, magamba 120 ya
kakakuona na mazao ya bahari nayo yamekamtwa.
Hii
ni baada ya Askari wa Bandari kutilia shaka mizigo iliyokuwa kwenye
gari ikiingizwa bandarini. Meno ya tembo yaliyokamatwa bado ni mapya
ikiwa na maana tembo hao wameuawa katika kipindi kizichozidi mwezi mmoja
uliopita.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
DK.SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Hassan Khatib, (kulia) alipotembelea banda la Ofisi ya faragha Ikulu, wakati
wa Maonesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, yaliyofanyika jana
viwanja vya Beit el Ras, katika shamra shamra za sherehe za Mapinduzi
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
WARIOBA: SERIKALI TATU SI MZIGO
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, ametetea muundo wa serikali tatu kuwa hauna gharama, tofauti na inavyotafsiriwa na wengi. Mbali na kutetea gharama za uendeshaji wa serikali tatu, Jaji Warioba pia amewashukia wanaodhani mapendekezo ya muundo wa serikali tatu ni yake binafsi, kutokana na msimamo wa siku nyingi wa kiongozi huyo.
Akizungumza na Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Jaji Warioba alisema muundo wa serikali tatu umepunguza gharama za uendeshaji. Kwa mujibu wa Jaji Warioba, chini ya muundo huo hata Bunge linatarajiwa kuwa na wabunge 75 tu, hatua ambayo itapunguza gharama. Mwenyekiti huyo alisema kuwa gharama za uendeshaji wa Serikali ya Muungano zitakuwa katika Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mambo ya Nje huku katika maeneo yaliyobaki gharama zake zitakuwa zimepungua zaidi.
“Hivi kwa nini hili la muundo wa muungano tunajadili gharama wakati kila mwaka tunapoongeza mikoa, wilaya, tarafa, majimbo na vijiji gharama zinaongezeka wala hakuna anayezungumzia wala kuhoji? Hivyo hivyo kwa kuwa na serikali tatu, hakuna gharama, tena kimsingi tumepunguza gharama za migogoro ya mara kwa mara ya kushughulikia kero za Muungano,” alisema Jaji Warioba.
Thursday, January 02, 2014
MWANAJESHI AUA VIJANA WAWILI KWA BASTOLA
Mwanajeshi
wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), ambaye jina lake limehifadhiwa
anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kuwaua kwa kuwapiga risasi
vijana wawili na kisha kuwajeruhi vibaya wengine wawili walipokuwa
katika shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya. Tukio hilo lilitokea
majira ya saa sita na robo usiku wa kuamkia jana, katika eneo la Pugu
Kinyamwezi, Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Mwandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha
Minangi (pichani) alisema tukio hilo lilitokea baada kundi la vijana
waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya kuzingira gari la mwanajeshi huyo
aliyekuwa akielekea nyumbani kwake Pugu Kinyamwezi, akitokea katikati ya
Jiji kwa shughuli zake.
Alisema
mwanajeshi huyo alikuwa na gari aina ya Toyota Rava 4 na baada ya kufika
katika eneo hilo alizingirwa na kundi la vijana hao waliokuwa
wakisherehekea mwaka mpya na ndipo aliamua kutoa bastola yake na
kufyatua risasi ambapo iliwapata vijana hao na kufa papo hapo na
kujeruhi wengine.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
RAY C AFUNGUKA KUHUSU JACK CLIF... ASEMA WACHA AFE TU TENA ANYONGWE KABISA...!!!
Kutokana
na maswahibu makubwa yaliyompata Ray C juu ya madawa ya kulevya,
ameshindwa kujizuia kutokusema ya moyoni mwake juu ya mwanadada Jack Cliff aliyekamatwa na madawa ya kulevya nchini China. Kafunguka maneno
mengi sana na alionyesha ni jinsi gani alivyokuwa hamuonei huruma
mwanadada Jack mpaka kuamua kutamka bora anyongwe tu.
Soma alichokisema hapa
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
LOWASAA ATANGAZA KUANZA RASMI SAFARI YA NDOTO ZAKE...!!!
Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza kuanza rasmi kwa safari
aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo amesema itatimiza ndoto za
Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
Akizungumza
katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini, Lowassa
bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, aliwashukuru watu wote kutoka maeneo
mbalimbali nchini, ambao walimsindikiza katika ibada hiyo.
Lowassa alisema anaamini watu hao waliofika, wana uhakika wa ushindi katika safari hiyo kwa kumtegemea Mungu.
"Nimefarijika
sana leo kuwaona hapa marafiki zangu wengi. Ninapowatazama hadi machozi
yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na
ndoto yangu,'' alisema Lowassa na kupokelewa na sauti za shangwe
kanisani.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)