Mwanajeshi
wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), ambaye jina lake limehifadhiwa
anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kuwaua kwa kuwapiga risasi
vijana wawili na kisha kuwajeruhi vibaya wengine wawili walipokuwa
katika shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya. Tukio hilo lilitokea
majira ya saa sita na robo usiku wa kuamkia jana, katika eneo la Pugu
Kinyamwezi, Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Mwandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha
Minangi (pichani) alisema tukio hilo lilitokea baada kundi la vijana
waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya kuzingira gari la mwanajeshi huyo
aliyekuwa akielekea nyumbani kwake Pugu Kinyamwezi, akitokea katikati ya
Jiji kwa shughuli zake.
Alisema
mwanajeshi huyo alikuwa na gari aina ya Toyota Rava 4 na baada ya kufika
katika eneo hilo alizingirwa na kundi la vijana hao waliokuwa
wakisherehekea mwaka mpya na ndipo aliamua kutoa bastola yake na
kufyatua risasi ambapo iliwapata vijana hao na kufa papo hapo na
kujeruhi wengine.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Aliwataja
waliokufa katika tukio hilo kuwa ni Ibrahim Mohamed(16) mkazi wa Pugu
Kinyamwezi, Abubakari Hassan(14) naye mkazi wa Pugu Kinyamwezi.
Aliwataja
waliojeruhiwa kuwa ni Rupano Wanga(17) mkazi wa Pugu Makange na Kassim
Abdul (16), mwanafunzi wa shule ya sekondari Tandika.
Minangi alisema polisi walifanikiwa kumkamata mwanajeshi huyo na kumweka
rumande katika kituo cha polisi cha Stakishari usiku huohuo.
Alisema vijana hao waliojeruhiwa walipelekwa Hospitali ya Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Wakati
huohuo, wakazi wa Kiwalani, Wilayani Temeke walipata wakati mgumu baada
ya kutokea kwa kundi la vibaka waliokuwa wakipora simu, fedha na
kutembeza mapanga kwa wakazi hao.
Kwa
mujibu wa baadhi ya wakazi wa maeeno hayo, kundi hilo lilikuwa
likizungukia kila nyumba na katika nyumba za starehe na kila aliyekutwa
nje walichukua simu yake, fedha na wengie kupigwa mapanga.
No comments:
Post a Comment