TAARIFA KWA UMMA
Mamlaka
ya Bandari Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii
pamoja na vyombo vingine vya Dola, tarehe 2 Januari 2014 majira ya saa
tatu asubuhi kwenye Bandari ya Dar es Salaam, imekamata meno 81 ya tembo
yenye uzito wa kilo 303 sawa na tembo 41. Aidha, magamba 120 ya
kakakuona na mazao ya bahari nayo yamekamtwa.
Hii
ni baada ya Askari wa Bandari kutilia shaka mizigo iliyokuwa kwenye
gari ikiingizwa bandarini. Meno ya tembo yaliyokamatwa bado ni mapya
ikiwa na maana tembo hao wameuawa katika kipindi kizichozidi mwezi mmoja
uliopita.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Wizara
inasikitishwa sana na vitendo hivi viovu vya ujangili ambavyo vimetokea
ndani ya muda mfupi. Tayari watuhumiwa wawili wanashikiliwa na Polisi
kufuatia tukio hilo. Majina yao yanahifadhiwa kwa lengo la kutovuruga
upelelezi.
Serikali
inasisitiza tena kwamba imejizatiti kupambana na vitendo vya ujangili
katika mapori yote na maeneo yote ya mipaka ya nchi yetu. Pia, Serikali
inapanua wigo wa upelelezi kuhakikisha wote waliohusika wanapatikana na
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Imetolewa na:
Chikambi K. Rumisha
Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Januari 2, 2014
Chikambi K. Rumisha
Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Januari 2, 2014
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment