MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe, amemvaa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na kusema kamwe
chama hicho hakiwezi kuvumilia usaliti wa aina yoyote.
Akizungumza mjini Mwanza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika
Viwanja vya Malimbe, alisema kwa namna yoyote ile hawatamfumbia macho
mtu yeyote anayekwenda kinyume cha katiba na taratibu za chama hicho.
Alisema
Chadema ambayo imejengwa kwa damu za Watanzania haiwezi kukubali kuona
mtu yeyote anatoboa ‘boti’ yake iendayo kasi katikati ya bahari wakati
huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa utakaofanyika mwakani.
Mbali na kumshukia Zitto pia amekirushia kombora Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusema kinatumia mbinu chafu kutaka kuiua Chadema kabla ya mwaka 2015. Alisema kamwe mbinu hizo hazitafanikiwa maana Chadema ipo kwa mpango wa Mungu.