Wednesday, December 04, 2013
UN: KUTUMIA NDEGE ZISIZO NA RUBANI DRC
Majeshi ya Umoja wa Mataifa katika
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yameanza kutumia ndege zisizo na rubani
kuchunguza harakati za waasi katika mipaka na Rwanda na Uganda.
Hii ni mara ya kwanza kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa kutumia ndege za aina hiyo.
Ndege
mbili za kwanza zilirushwa kutoka mji wa mashariki wa Goma ambao mwaka
jana ulikaliwa kwa muda mfupi na waaasi wa kundi la M23.
Ndege mbili za kwanza zinaundwa na shirika la Italia la Selex ES.
Jeshi la Umoja wa mataifa katika
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ndio kubwa kupita yote duniani na
lilichangia kwa kiasi kikubwa mwezi uliopita ushindi dhidi ya waasi wa
kundi la M23;lakini bado kuna makundi mengine kadhaa ya wanamgambo
nchini humo.
Kikosi kipya kilichoimarishwa nguvu
cha Umoja wa Mataifa kilitumia ndege za helikopta kulisaidia jeshi la
Congo dhidi ya waasi hao wa M23.
Eneo tajiri la madini la mashariki mwa
Congo limekumbwa na vita kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita lakini
kushindwa kwa M23 kumeleta matumaini fulani ya kupatikana utulivu zaidi
kwa eneo hilo.
DK MIGIRO APONGEZWA NA WENGI KWA KUTEULIWA NA RAIS KUWA MBUNGE
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa
Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye
ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa
kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,
Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania

Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.
Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.PICHA
NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Tuesday, December 03, 2013
MBOWE, DK SLAA WAPIGWA MARUFUKU KUKANYAGA ARDHI YA MWANZA ...!!!
Mwanza, Tanzania. Gazeti la RAI leo katika ukurasa wake wa kwanza
limeandika kwamba Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Katibu
Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa amepigwa marufuku kukanyaga jijini
Mwanza ambako chama hicho kimepanga kwenda kuwahutubia wananchi.
Mbali na kupigwa marufuku, viongozi wa Chadema wamepewa masharti ya
kufanya kila linalowezekana kumrejesha madarakani aliekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa madaraka.
Viongozi wa Chadema wametakiwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku nne kuanzia jana.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya Chadema, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele wakati akizungumza na waandishi wa habari.

WAATHIRIKA WA VVU MAKETE WASUSA KUNYWA DAWA ZA ARV
Mkuu
wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akihutubia kwenye maadhimisho ya
siku ya UKIMWI duniani katika kata ya Mbalatse wilaya ya Makete
Wakazi wa Mbalatse wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Makete akitoa hotuba yake
BOKO HARAM WASHAMBULIA NGOME YA JESHI
Wapiganaji wa Boko Haram
Wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia ngome ya Jeshi Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria na kuharibu helkopta mbili maafisa wa serikali
wamesema.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mamia ya wapiganaji wameshambulia
maeneo kadhaa katika mji wa Maiduguri kuanzia mapema asubuhi siku ya
jumatatu.
Amri ya kutotembea ovyo ya saa 24 imetangazwa katika jimbo la Maiduguri.
Na uwanja wa ndege unaotumiwa na wananchi umefungwa kwa muda.
Mwandishi wa habari wa BBC anasema shambulio hilo lililopangwa ni
shambulio kubwa ambalo limerudisha nyumba juhudi za Jeshi la Nigeria.
Maelfu ya watu wameuwawa nchini Nigeria na wapiganaji hao tangu mwaka
2009 wakati Boko Haram walipoanza mashambulizi ya kutaka kusimika
utawala unaoegemea sharia ya kiislamu.
CHADEMA KIGOMA WATOA TAMKO KUHUSU ZIARA YA DR SLAA NA TISHIO LA USALAMA....!!!
Hii ni taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Dec 2 2013 likiwa ni tamko la kikao cha mkoa Chadema Kigoma.
Ni kuhusu Kikao
kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na
Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma
5/12/2013 ambapo
atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya
miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano
ufanyike makao Makuu ya Jimb lengo likiwa ni kuangalia uhai wa chama.
Mambo makuu na muhimu yalizingatiwa ambapo usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.
Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo
i.Mkoa
uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu
kwa mkoa wetu ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uweze
kwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu
ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu
yetu hata kama yanamaumivu ….katiba ifuatwe katika kutatua tatizo –
Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya
k/kuu ambayo dhahiri yalilenga Zitto – Kisiasa.
ii. Mkoa
ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya
viongozi wa majimbo ya mkoa kwamba hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa
kiongozi Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na
wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.
iii. Kwa
hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6
kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara
yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake
Kitaifa.
iv. Hivyo
Mkoa kupitia kikao hicho ikaonekana ni bora kuzuia kuliko kutibu,
tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana
mitazamo ni HATARI katika hali hiyo, mkoa ulijiridhisha usalama
hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo
salama tu.
v. HOFU/TAHADHARI - Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.
Mkoa
hautokwepa lawama na uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini
ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao
Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa
upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa
Taifa.
LENGO KUU: NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA
ALHAJ. JAFARI KASISIKO MSAFIRI WAMALWA
M/KITI MKOA 01/DEC.2013 KATIBU MKOA
Monday, December 02, 2013
MKUU WA MKOA WA MOROGORO MH. JOEL BENDERA NA NAIBU WAZIRI MEDEYE WATUNUKIWA PHD YA HESHIMA
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa
Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu
ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea
matatizo ya Haki za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, (
kulia) mara baada ya kumtunukisha Shahada ya Uzamivu ya Heshima ( PhD)
katika Masuala ya Falsafa ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Califonia State
Christian kilichopo nchini Marekani, kwa mamlaka aliyopewa na Bodi cha
Chuo Kikuu hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akivishwa kofia ya udaktari wa Heshima .
Naibu
Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dk Joel Goodluck Ole
Medeye ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa
Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina
wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki za Binadamu
Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, ( kulia).kati kati kati ni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalongeris.
TABIA ZA MSICHANA ANAYEKUPENDA KIMAPENZI LAKINI HAWEZI KUSEMA
1. Atakutega kupata attention yako. Hufanya mambo ambayo yatamfanya
kuona kama unampenda au lah! Mf wa mambo hayo ni kujifanya anaumwa na
kuangalia respond yako kwake ni kiasi gani unamjali na kiasi gani
utahangaika kwa ajili yake au
2. Haoni aibu kugusa sehemu yako ya mwili. Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomosa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahisishia kazi ya kuwa na wewe
3. Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli
4. Wivu.
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi.
5 anakumbuka siku zako muhimu. Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatowez kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifaulu mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza
6. Eye contact anapenda kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaelewa ni kiais gani anakupenda kupitia vile ambavyo anakuangalia.
Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda si wote wana ujasiri wa kuwatazama wapenzi wao.
7. Hupenda kukaa mmuda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe.
8. Yupo tayari kuangamiza. Kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Utaona vipi huyo msichana alivyo kwako na wa wengine. Yaani yupo tayari yeye akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwamba hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine.
9. Anachukulia matatizo yako kama ni yake. Unapomueleza kuwa ana tatizo anajali tatizo lako kama vile ni lake na hujisikia vibaya sana na kuhuzunika na atafanya lolote ili aweze kukusaidia utoke katika hilo tatizo.
10. Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakuambia anakupenda. Kwa kuwa anakupenda endapo ikatokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose

UZINDUZI WA AZAM TV HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA...!!!
Mambo yalikuwa kama hivi kwenye uzinduzi wa Azam TV jijini Dar..
Mtangazaji wa Televisheni ya Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akiwa kwenye
Red Carpet kabla ya mahojiano na Mkurugeni wa Kajunason Blog Cathbert
Angelo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa METL na Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji
alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Azam TV.
Pichani akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi
Mwambulambo.
HUYU NDIYE JOSEPH OMOG KOCHA MPYA AZAM FC
Kocha mpya wa Azam FC Joseph Omog akiwa na Mwenyekiti wa timu hiyo Ndugu Said Mohammed.
WANAWAKE WENGINE WANASWA NA DAWA ZA KULEVYA KIA ...!!!
Jeshi la Polisi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (Kia), linawashikilia wanawake wawili ambao ni
wafanyabiashara wa kigeni kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha kilo 12.7
za dawa za kulevya maarufu kama 'unga'.
Hilo ni tukio la pili katika muda usiozidi siku saba kwa raia wa kigeni kukamatwa na dawa hizo katika uwanja huo, ikiwa ni wiki mbili tangu Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe, atishie kuwafukuza kazi maofisa wa idara za usalama watakaobainika kujihusisha na biashara hiyo kupitishwa katika uwanja huo.
Watuhumiwa hao waliokamatwa ni jana alfajiri katika uwanja huo ni Josiane Dede Creppy (25), raia wa Togo na Grace Teta (34), raia wa Liberia ambao kwa nyakati tofauti, mmoja akijiandaa kuelekea jijini Accra, Ghana na mwingine nchini Afrika Kusini.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, aliiambia NIPASHE jana kwamba mtuhumiwa Grace alikamatwa akiwa na kilo 10.5 za dawa hizo wakati akisafiri kwa ndege ya Shirika la Precision Air kutoka KIA kwenda Captown nchini Afrika Kusini kupitia Nairobi, Kenya.
“Huyu alikamatwa na unga unaoaminika kuwa ni dawa za kulevya alfajiri ya saa 10:45 akitumia hati ya kusafiria yenye namba 1039080 ikimuonyesha ni mfanyabiashara na raia wa Liberia. Josiane alikamatwa saa 8:50 alfajiri akiwa na kilo 2.2 za dawa hiyo akiwa anataka kuondoka na ndege ya Shirika la Ethiopia kelekea Ghana,” alisema Kamanda Boaz

Sunday, December 01, 2013
CHADEMA YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA
UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA
Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya
Ndugu Ali Omari. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua
na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA,
tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;
Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu
ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila
Mkumbo, chama kimeshafunga mjadala kwenye vyombo vya habari kwa
kuheshimu na kuzingatia taratibu za kikatiba za ndani ya chama
kuendelea.
Pili kuhusu suala la restructuring ya
Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi
wafuatao, kuwa ni wapya;
1.Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika
3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.
Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.

Subscribe to:
Posts (Atom)