Wednesday, November 27, 2013

CECAFA CHALLENGE CUP 2013 KUANZA RASMI LEO, STAR v ZAMBIA…TAKWIMU ZA TIMU ZOTE




Na Baraka Mbolembole


Timu ya Taifa ya Kenya ' Harambee Stars', leo itakata ' utepe' wa
michuano ya Mataifa ya ukanda wa CECAFA, kwa kucheza na timu ya Taifa ya Ethiopia. Wenyeji hao wa michuano ya sasa na makamu bingwa wa taji hilo, wanapewa nafasi kubwa ya kuvuka kundi A, mbele ya Ethiopia,
Zanzibar, na Sudan Kusini.

Mabingwa watetezi, Uganda wao wapo kundi C, pamoja na Rwanda, Sudan, na Eritrea katika kundi linalotarajiwa kuwa gumu zaidi katika michuano hiyo. Moi Kasarani na Nyayo Stadium, ni viwanja viwili vilivyopo
katika jiji la Nairobi, Kisumu Stadium, Mombasa, na Machakos ni idadi
ya viwanja vitano ambavyo vitazipokea timu 12. Mapema leo mchana wawakilishi wengine wa Tanzania, timu ya Zanzibar Heroes itacheza na  Sudan Kusini katika mchezop wa kwanza kabisa mwaka huu.
  KILIMANJARO STARS vs ZAMBIATimu ya Taifa ya Tanzania Bara itaanza kibarua chake cha kwanza siku ya kesho, Alhamis kwa kucheza na timu ' alikwa' ya Zambia katika mchezop unaosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa soka. Zambia, mabingwa wa michuano ya Mataifa ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika, COSAFA, iliifunga Kilimanjaro Stars katika mchezo wa mwisho kukutana katika michuano hii, walipoalikwa kwa michuano iliyofanyika, Dar es Salaam, 2010.
Mbele ya Rais wa Jamhurio ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Stars ilipoteza kwa kulala bao 1-0 siku ya ufunguzi.

Monday, November 25, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 25, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.

BALAA TENA SIMBA SC…BASI LAO LA YUTONG LAKAMATWA, KISA MADENI ...!!!

BASI_LA_SIMBA_85a15.jpg
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
BASI kubwa la klabu ya Simba aina ya Yutong, walilopewa na wadhamini wao, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) linashikiliwa na kampuni ya MEM kutokana na deni la zaidi ya Sh. Milioni 40.
Basi hilo lenye thamani ya Sh. Milioni 200 linashikiliwa kwa siku ya pili sasa, linaweza kupigwa mnada baada ya siku 14, iwapo Simba SC itashindwa deni hilo.
Hali hiyo inatokea wakati klabu inakababiliwa na mgogoro mkubwa baina ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji na Mweyekiti wao, Alhaj Ismail Aden Rage, Mbunge.
Rage hakupokea simu alipopigiwa jioni hii ili kuzungumzia suala hilo na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Evodius Mtawala simu yake haikupatikana kabisa.
Jumanne wiki hii Kamati ya Utendaji ya Simba SC ilitangaza kumsimamisha Rage katika kikao chake cha Jumatatu usiku kwa sababu anaendesha klabu kwa kufanya maamuzi yake mwenyewe bila kushirikisha kamati ikiwemo kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (a).
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang'are 'Kinesi' alisema sababu nyingine ni Rage kuahirisha mkutano Mkuu maalum wa katiba ulioidhinishwa na mkutano mkuu bila kuishirikisha kamati.

Sunday, November 24, 2013

LOWASSA AIELEZEA ILANI IJAYO YA CCM


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akiwahutubia wakazi wa Kigamboni.
******
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa amewaomba wanachama wa CCM kushawishi suala la elimu bure na bora liwe ajenda ya kwanza katika Ilani ijayo ya uchaguzi ya Chama hicho.
Akiwahutubia wananchi wa kata ya Kigamboni ambako alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kukabidhiwa madawati shule za msingi za kata hiyo, Mh Lowassa amesema kwa maoni yake anapendekeza suala hilo liwe ajenda ya kwanza katika Ilani ya uchaguzi ya ccm.
"Wana CCM wenzangu naomba tushawishi suala la elimu bure kwa wanafunzi wote wa shule tena elimu bora liwe la kwanza katika ilani ijayo ya uchaguzi" alisema Lowassa na kushangaliwa na mamia ya wananchi wa kata hiyo.
Alisema kuwa ana ndoto hiyo kuwa siku moja elimu itakuwa bure tena elimu iliyo bora, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kujenga usawa wa matabaka kwa taifa letu.
Lowassa ambaye ni miongoni mwa wana CCMinakosemekana yuko katika mbio za kuwania urais uchaguzi ujayo, alisema kuwa kutokana na hali nzuri ya uchumi hivi sasa suala hilo linawezekana.
"Wakati Mzee Mkapa anaingia alikuta madeni mengi sana Serikali yake ikafanya juhudi kulipa na kuanza kukopesheka, Rais Kikwete yeye ameunyanyua uchumi kwa kuimarisha miundo mbinu na sasa hali ni nzuri kabisa, hebu sasa tuelekeze nguvu katika elimu"alisema na kuongeza iwe kipaumbele cha sasa.

RAGE AGOMA KUITISHA MKUTANO WA DHARURA - ATISHIA KUJIUZULU AMTEUA WAMBURA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI

Hatimaye mkutano wa Mwenyekiti aliyesimamishwa Simba, Ismail Aden Rage na waandishi wa habari umefanyika leo mchana kama alivyohaidi jana.

Katika mkutano huo Rage amegoma kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama kama alivyoagizwa na Rais wa shirikisho la soka nchini Bwana Jamal Maliniz mapema jana.

Akizungumza na waandishi wa habari Rage amesema kwamba haoni sababu za kuitisha mkutano mkuu na endapo TFF na Malinzi wataendelea kumshinikiza kufanya hivyo basi atajiuzulu.

Katika hatua nyingine Rage amemteua mwanachama wa klabu hiyo Michael Wambura kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba.

Pia, amemteua Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 24, 2013

.
.
.

MAMA YAKE ZITTO KABWE AELEZEA SAKATA LA MWANAYE

Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.

“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.

Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. 
Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”

Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki. “Kwa sasa nataka mwanangu atulize akili.”

Shida Salum, mbali na kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, pia ni  mwasisi wa  Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata) na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo (Chawata)

SOMA KWA MAKINI ILE TAARIFA MAALUM YA CHADEMA KWA WATANZANIA JUU YA UAMUZI WA KAMATI KUU


Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu Maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama hicho ya kuwavua nyazifa Naibu Katibu Mkuu,Zitto Kabwe na  Mjumbe wa Kamati Kuu Kitila Mkumbo Katikati ni Mwanasheria wa chama hicho,Tundu Lissu na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa. PICHA | FIDELIS FELIX  
----
 TAARIFA KWA WATANZANIA JUU YA UAMUZI WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU KUWAVUA NYADHIFA ZA UONGOZI NAIBU KATIBU MKUU, MH. ZITTO ZUBERI KABWE NA WENZAKE 
 
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,

         Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuanzia asubuhi ya siku ya Jumatano ya tarehe 20 Novemba, 2013 hadi alfajiri ya leo Ijumaa tarehe 22 Novemba, 2013 imetafakari na kujadili kwa kina taarifa mbali mbali juu ya hali ya kisiasa ndani na nje ya Chama chetu ambayo kwa muda mrefu imegubikwa na tuhuma kubwa na nzito dhidi ya Chama chetu na viongozi wake wakuu, yaani Mwenyekiti wa Taifa, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (MB), na Katibu Mkuu, Dk. Wilbrod Peter Slaa. Tuhuma hizi zilikuwa na malengo na athari ya kuwapaka matope na kuwachafua viongozi wakuu wa Chama na Chama chenyewe, kutengeneza mtandao wa siri ndani na nje ya Chama ambao hatimaye ungefanikisha sio tu lengo la kufanya mapinduzi nje ya utaratibu wa kikatiba wa Chama, bali pia ungekipasua Chama vipande vipande na hivyo kuua matumaini ya Watanzania juu ya uwezekano wa kufanya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na kijamii katika nchi yetu kwa kukiondoa madarakani Chama cha Mapinduzi (CCM).

          Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Uchunguzi wa Kamati Kuu umebaini kuwepo kwa mkakati mkubwa wa kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013.’ Mkakati huu uliandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’ ambacho vinara wake wakuu ni wanne, yaani Naibu Katibu Mkuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambaye kwenye waraka huo anajulikana pia kama ‘MM’ au ‘Mhusika Mkuu’; mjumbe wa Kamati Kuu na mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitilla Mkumbo ambaye kwenye waraka anajulikana pia kama M1; Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ambaye kwa sasa amesimamishwa uongozi, Bwana Samson Mwigamba na ambaye kwenye waraka anaitwa M3; na mtu mwingine ambaye hadi sasa jina lake halijajulikana lakini kwenye waraka anajulikana kama M2 na anatajwa kuwa yuko ‘ukingoni kupigwa nje’ katika mageuzi ya kiutendaji yanayoendelea katika Sekretariat ya Chama hapa Makao Makuu.

       Kwa mujibu wa waraka wenyewe, “Mkakati huu umeandaliwa kwa pamoja na M2 na M3 na kupitiwa na kurekebishwa na M1 ili upelekwe kwa MM kwa maoni ya mwisho na kuanza utekelezaji.” Mbele ya Kamati Kuu, Dk. Mkumbo alikiri kwamba MM au Mhusika Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe; M1 ni yeye mwenyewe Dk. Mkumbo na M3 ni Bwana Mwigamba. Dk. Mkumbo alikataa kata kata kumfahamu M2. Aidha, Dk. Mkumbo alikiri mbele ya Kamati Kuu kwamba yote yaliyoandikwa katika ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ yametoka kwenye ‘Mtandao wa Ushindi’ na hayajabadilishwa.

Thursday, November 21, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 24, 2013

.
.
.

HOFU YATANDA KAMATI KUU YA CHADEMA, KIKAO CHAFANYIKA CHINI YA ULINZI MKALI WA BLUE GUARD

 

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (katikati) akiwa na walinzi wake akiwasili katika Jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, jana kushiriki kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho. Picha na Michael Jamson 

********

Hali ya wasiwasi iligubika eneo  kinapofanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilichoanza Dar es Salaam jana.


Ulinzi mkali wa walinzi wa Chadema (Blue Guard), uliimarishwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza kinapofanyika kikao hicho ambacho kinatarajiwa kumalizika leo, huku kukiwa na maagizo yaliyoashiria kuwapo kwa mambo mazito.




Maazimio ya kikao hicho yanasubiriwa kwa hamu na wafuatiliaji wa mambo ya siasa nchini kwani kinafanyika katika kipindi ambacho chama hicho kikuu cha upinzani nchini kinapita katika misukosuko na hasa ya malumbano baina ya makamanda wake wa juu.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS NOVEMBA 21, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

MAZUNGUMZO YA NYUKLIA YA IRAN YAANZA

017216860_35400_0aad8.jpg
Catherine Ashton Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja (kushoto) na Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva baada ya kushindwa kufikiwa kwa makubaliano. (10.11.2013).
Mazungumzo magumu yanaanza leo kati ya Iran na mataifa makubwa kutafuta makubaliano kwa mpango wa nyuklia wa Iran ambayo pia yatawaridhisha wanasiasa wa msimamo mkali huko Marekani, Israel na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mazungumzo hayo yanafanyika Geneva wakati kukiwa na hali ya mvutano inayoongezeka Mashariki ya Kati ambapo waziri wa mambo ya nje wa Iran akiishutumu Israel kwa kujaribu kuvuruga mchakato huo kufuatia mirupuko miwili ya mabomu iliouwa takriban watu 23 nje ya ubalozi wa Iran mjini Beirut hapo jana.Wizara ya mambo ya nje ya Iran imeilaumu Israel na mamluki wake kwa kuhusika na miripuko hiyo.
Israel imekanusha madai hayo na Waziri Mkuu wake Benjamin Netanyahu leo hii anatarajiwa kuendeleza kampeni yake dhidi ya kufikia makubaliano ya nyuklia na Iran wakati atakapokutana na Rais Vladimir Putin wa Urusi mjini Moscow.

WAZIRI NCHIMBI, MWAKYEMBE WAFANYA KIKAO NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA ZAO JIJINI DAR

bc_b7ac1.jpg
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto-meza kuu) akizungumza na Watendaji Wakuu wa wizara yake pamoja na wa Wizara ya Uchukuzi katika Kikao cha utendaji kazi cha kuimarisha uhusiano kati ya wizara hizo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam. Kulia (meza kuu) ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
cd_03534.jpg
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe (kulia-meza kuu) akizungumza na Watendaji Wakuu wa wizara yake pamoja na wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Kikao cha utendaji kazi cha kuimarisha uhusiano kati ya wizara hizo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam. Kushoto (meza kuu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
ab_64f21.jpg
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na Watendaji Wakuu wa wizara yake pamoja na wa Wizara ya Uchukuzi (hawapo pichani) katika Kikao cha utendaji kazi cha kuimarisha uhusiano kati ya wizara hizo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday, November 20, 2013

EMMANUEL ADEBAYOR AONESHA UTAJIRI WAKE, JUMBA LA KIFAHARI, MAGARI NA NDEGE

1
Mchezaji wa Tottenham Hotspur Emmanuel Adebayor ni mmoja kati ya wachezaji matajiri sana Africa na anamiliki nyumba kwao Togo,Ghana,UK na Marekani.

00
Adebayor mwenye miaka 29 ametoa picha zake zikionyesha magari yake ya kifahari, private jet na vitu vingine vingine.
,5
Enjoy picha 15 kutoka kwa Adebayor ambaye siku chache zilizopita alikuwa kwenye harusi ya Peter wa P Square pamoja na Diamond Platnums.

0

WATU ZAIDI YA 50 WAFUKIWA BAADA YA JENGO KUPOROMOKA AFRIKA KUSINI

131119173308 jengo laporomoka sa 304x171 bbc nocredit f5726
Watu wawili wamefariki na wengine takriban watu 50 kukwama kwenye vifusi baada ya paa ya jumba la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini.
Inaarifiwa watu 29 wameweza kuokolewa.
Taarifa zinazohusianaAfrika Kusini
Madaktari kutoka kampuni ya kibinafsi ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban.
"Shughuli hii itachukua mda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale waliokwama," alisema msemaji wa kampuni hiyo.
Hata hivyo ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.
Inaarifiwa watu wengine 26 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majereha mabaya.
CHANZO BBC SWAHILI

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...