Timu ya Taifa ya wanawake chini ya
miaka 20 (Tanzanite) imefuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya Kombe
la Dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada ya leo (Novemba 9
mwaka huu) kuibugiza Msumbiji mabao 5-1.
Mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo
iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini Maputo yalipatikana
kupitia kwa Sherida Boniface alipiga matatu (hat trick) wakati mengine
yalifungwa na Vumilia Maarifa na Donesia Minja.
Msafara wa Tanzanite ulioongozwa na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Kidao Wilfred utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) leo Jumapili (Novemba 10 mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa
ndege ya LAM.
Tanzanite inayofundishwa na Rogasian
Kaijage itacheza mechi ya raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini. Mechi
ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Desemba 6 na 8 mwaka
huu wakati ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba
20-22 mwaka huu.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)