Wednesday, October 30, 2013

WEMA SEPETU AFUNGUKA JINSI BABA YAKE ALIVYOTESEKA MPAKA MAUTI ILIPOMCHUKUA

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akielezea kuhusu msiba wa baba yake mzazi Balozi Abraham Isaac Sepetu alipoongea na GLOBAL TV. Balozi Sepetu alifariki asubuhi ya Jumapili Oktoba 27, 2013 katika hospitali ya TMJ jijini Dar na mwili wake jana nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar es Salaam tayari kwa mazishi yatakayofanyika leoVisiwani Zanzibar.

Tuesday, October 29, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 29, 2013

.
.
.

ASKARI ALIYEUAWA DRC ALIKUWA MBIONI KUFUNGA NDOA DESEMBA



Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), aliyeuawa kwa kupigwa risasi kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani, katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (Monusco), Luteni Rajab Ahmed Mlima, alikuwa katika hatua za mwisho za kufunga ndoa.

Askari huyo aliuawa katika  uwanja wa mapambano na vikosi vya wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23, katika Milima ya Gavana, karibu na Goma, DRC- Congo wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani

Akizungumza na gazeti hili, kaka wa marehemu Dk Aziz Mlima, alisema kuwa ndugu yake alikuwa tayari amekamilisha mipango yote na kilichokuwa kikisubiriwa ni siku ya kufunga ndoa hiyo.

“ Alikuwa yuko mbioni kufunga ndoa, lakini kwa sasa sitapenda kutaja jina la mchumba wake kwa kuwahayupo hapa lakini naye ni askari,” alisema Dk Mlima.

MWIGAMBA AZIDI KUANIKA MADUDU YA CHADEMA


*Awaonya wanaomwita msaliti
*Dk. Slaa aibua mapya

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, aliyesimamishwa uongozi asema atakichafua chama hicho kama ataendelea kuitwa msaliti.

Hatua hiyo, imekuja baada ya Mwigamba kukiri hadharani kusambaza waraka unaowatuhumu viongozi wa chama hicho katika mtandao wa Jamii Forum (JF), akitumia jina la Maskini Mkulima. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mwigamba aliwaonya viongozi wa Chadema wanaomwita msaliti. 
 
Alisema kama wanataka awe msaliti, yupo tayari kumwaga mambo yote hadharani, tena kwa ushahidi usio na shaka hata kidogo.

Mwigamba, aliyejiunga na Chadema mwaka 2004, akiwa mwanachama wa kawaida, alisema akiwa makao makuu mjini Dar es Salaam kama mhasibu mkuu wa chama, ndipo alipoanza kutambua udhaifu mkubwa wa kiuongozi ndani ya chama chake.

“Niliondoka pale makao makuu kwa mizengwe, kiongozi mmoja mkubwa kabisa alinifukuza kazi kwa kunipigia simu, tena baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa Fedha,Anthony Komu akiwa nje ya Dar es Salaam na kumwagiza anifukuze,” alisema Mwigamba.

WAZIRI AANGUA KILIO MAHAKAMANI



ALIYEKUWA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Arcado Ntagazwa, jana alijikuta akiangua kilio ndani ya kizimba, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutamka yeye na wenzake wawili wameachiwa huru.
Ntagazwa alitokwa na machozi, mbele ya Hakimu Mkazi, Geni Dudu, alipokuwa akisoma hukumu katika kesi ya kujipatia tisheti 5,000 na kofia 5,000 za kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mwaka 2009 kwa njia ya udanganyifu.

“Ukiangalia ushahidi hapakuwa na udanganyifu katika kuagiza kuchapwa kwa tisheti na kofia, waliamini wangeweza kulipa fedha hizi, ukiangalia uhalisia wa tisheti hazikuwa za kibishara… zilikuwa za kugawa bure kwa wananchi, zilikuwa kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa kupiga vita rushwa na ufisadi, zilikuwa kama mabango.

“Ni kweli washtakiwa walihujumiwa na kushindwa kulipia gharama za uchapishaji, tayari nina shaka hiyo inatosha sana kuwaona washtakiwa si wakosaji, shaka hata ikiwa ndogo kiasi gani manufaa yanakuwa kwa washtakiwa.

“Kutokana na ushahidi na vielelezo vilivyopo mahakamani, naona washtakiwa hawana kosa, wako huru, mlalamikaji akafungie kesi ya madai ili aweze kupata haki yake,” alisema Hakimu Dudu na kutamka washtakiwa wako huru.

Ntagazwa, alianza kujifuta machozi yaliyokuwa yakibubujika akiwa kizimbani na hata baada ya kushuka kizimbani aliendelea kububujikwa na machozi, huku akitembea taratibu mno kuelekea nje ya jengo la mahakama.

Hakimu Dudu kabla hajafikia uamuzi wa kuwaachia huru washtakiwa, alisema katika ushahidi hapakuwa na ubishi washtakiwa walichapisha tisheti na kofia, ushahidi huo unasapotiwa na vielelezo kwamba kampuni mbili zilikubaliana kuingia mkataba huo.

Alisema upande wa Jamhuri ulileta mashahidi watano mahakamani kuthibitisha mashtaka hayo na kuomba katika majumuisho ya mwisho, kwamba washtakiwa watiwe hatiani kwani waliweza kuthibitisha makosa yao bila kuacha shaka.

YANGA, MGAMBO JKT KUVAANA TAIFA LEO

Yanga-Mgambo_d3a44.jpg
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Bara leo itashuka katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kupambana na Mgambo JKT katika mchezo wa raundi ya kumi na moja ya ligi hiyo.
Yanga inaingia uwanjani leo ikiwa na pointi 19 ilizopata katika mechi 10 ilizocheza huku ikiwa nafasi ya nne. Azam inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 23 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 20 huku zote zikiwa zimecheza mechi 10. Mbeya City ni ya tatu ikiwa na pointi 20 katika mechi 10.
Kwa upande wao, Mgambo wanaingai uwanjani wakiwa na pointi tano walizopata katika mechi 10. Timu hiyo inaburuza mkia katika ligi hiyo.
Kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo kutakuwa mchezo utakaozikutanisha timu mwenyeji za mkoa huo ambazo ni Mbeya City na Tanzania Prisons. Rhino Rangers na JKT Ruvu zitacheza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.


Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaanza Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Novemba Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu kwenye uwanja huo huo.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Monday, October 28, 2013

AZAM YAINYUKA SIMBA 2-1, YAKAMATA USUKANI WA LIGI

Timu ya Soka ya Azam FC leo imefanikiwa kuiondoa Simba katika usukani wa Ligi Kuu soka Tanzania bara baada ya kuichapa goli 2-1 katika mchezo wa 11 wa timu hizo kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara. magoli ya Azam yalifungwa na Kipre Chetche  huku la Simba likifungwa na Ramadhan Singano 'Messi'.

Pos. Logo Club P W D L GF GA GD Pts
1 Azam FC Azam FC 11 6 5 0 17 7 10 23
2 Simba SC Simba SC 11 5 5 1 21 10 11 20
3 Mbeya City FC 10 5 5 0 13 7 6 20
4 Young Africans FC Young Africans SC 10 5 4 1 21 11 10 19
5 Mtibwa Sugar FC Mtibwa Sugar FC 10 4 4 2 16 11 5 16
6 Ruvu Shooting Stars 11 4 4 3 13 10 3 16
7 Kagera Sugar FC Kagera Sugar FC 11 4 4 3 12 10 2 16
8 Coastal Union SC 10 2 6 2 6 5 1 12
9 JKT Ruvu Stars JKT Ruvu Stars 10 4 0 6 9 11 -2 12
10 Ashanti United 11 2 4 5 10 18 -8 10
11 Tanzania Prisons 10 1 5 4 6 13 -7 8
12 Rhino Rangers 10 1 4 5 8 15 -7 7
13 JKT Oljoro FC 11 1 4 6 7 16 -9 7
14 JKT Mgambo JKT Mgambo 10 1 2 7 3 18 -15 5

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA MJANE NA FAMILIA YA BALOZI ISAAC SEPETU LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Mama Salma Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam. . Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 28, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.

SIRI ZA CHADEMA ALIZOZIANIKA MWENYEKITI WA CHADEMA ARUSHA, SAMSON MWIGAMBA

MWIGAMBA
Jina la ‘Maskini Mkulima’ lilijiunga na mtandao wa jamiiforums mnamo Desemba 27, 2011 na mpaka jana inaonyesha alikuwa ametuma zaidi ya Post 27 ikiwamo hii iliyokuwa na kicha cha habari: Wito kwa wana CHADEMA wote.
   
Makala hiyo ambayo ndiyo imefanikisha kumbaini ilitumwa Jamiiforums Oktoba 19 Mwaka huu chini ya kichwa cha habari cha ‘Wito kwa wana CHADEMA wote!’, inaeleza haya;

Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama.
 Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.

Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari.

Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika.

Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.

JAMAL MALINZI AMEIBUKA MSHINDI WA URAIS TFF...!!!

JAMAL Emil Malinzi, usiku huu ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupata kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa kupata kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani kura 52 na Imani Madega sita.
1_3cebe.jpg
Huyu ndiye Rais wenu mpya TFF; Rais aliyemaliza muda wake TFF, Leodegar Tenga kushoto akimtambulisha Jamal Malinzi kuliakuwa Rais mpya wa shirikisho hilo usiku nwa kuamkia leo ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam
Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa zamani wa Simba SC Wilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, Omar Abdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne.
Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54.

Kanda ya 11 Geoffrey Nyange 'Kaburu' amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya 10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata nne na Stewart Nasima 58.
Kanda ya tisa Othman Kambi aliyepata kura 84 yeye amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati James
Mhagama aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda aliyepata kura 11 na Kanda ya nane, Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52.
Kanda ya Tano, Ahmed Iddi Mgoyi aliyepata kura 92 amemshinda Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34, wakati Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa. Eley Mbise amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai.
Mbasha Matutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61, wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati kura 11, Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 na Kanda namba moja, Karilo Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.

TORRES AITEKETEZA MAN CITY DAKIKA YA MWISHO KABISA, CHELSEA YASHINDA 2-1

BAO la dakika ya 90 na ushei la Fernando Torres limeipa ushindi wa 2-1 Chelsea dhidi ya Manchester City Uwanja wa Stamford Bridge, London usiku huu katika Ligi Kuu ya England.
article-2477820-1905CCBA00000578-880_634x407_daa1f.jpg
Awali, Torres alitoa krosi nzuri kwa Schurrle akaifugia bao la kwanza Chelsea dakika ya 32, lakini Aguero akaisawazishia City dakika ya 48.
article-2477820-1905CB3A00000578-502_634x514_ad69f.jpg

Saturday, October 26, 2013

DIAMOND ATOA SIRI 5 ZA KUMRUDIA WEMA


MKALI wa songi linalotamba runingani na redioni ndani na nje ya Bongo la Number One, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kuanika siri tano za kurudiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Wiki mbili zilizopita, wakiwa Hong Kong, China, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii viliripoti kurudiana kwa Diamond na Wema waliomwagana takriban mwaka mmoja uliopita ambapo staa huyo wa Bongo Fleva aliibuka na kukanusha vikali akidai kuwa picha zinazomwonesha yuko na Wema ni za Filamu ya Temptations.
Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa dakika ishirini katika mahojiano maalum jijini Dar mara tu baada ya kutua kutoka China Jumatano iliyopita, Diamond alikiri kufaidi penzi la Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.

JK AIKATIA TAMAA CCM


2_f799f_1391b.jpg
• ASEMA IMEPOTEZA MATUMAINI KWA WATANZANIA(na Danson Kaijage, Dodoma Tanzania Daima)
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ameonyesha wasiwasi wa chama hicho kushindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 iwapo watendaji wake wataendelea na vitendo vya rushwa.
Alisema kuwa kwa sasa chama hicho kikongwe kimepoteza matumaini kwa Watanzania kutokana na vitendo ambavyo siyo vya kiungwana vinavyofanywa na watendaji.
Kwa kusisitiza, Kikwete alisema hata kama CCM itashinda uchaguzi wa 2015, kama tabia walizonazo watumishi na viongozi ndani ya chama hazitabadilika, ni wazi kuwa hakitapita kwenye uchaguzi wa 2020.
Rais Kikwete alitoa onyo hilo mjini hapa juzi usiku, alipokuwa akifunga mafunzo maalumu ya siku nne kwa makatibu na wenyeviti wa wilaya na mikoa wa chama hicho nchini nzima.
"Kama hatutabadilika katika suala la rushwa, mwaka 2015 tutakuwa na wakati mgumu sana, na kama mwaka huo tutafanikiwa kuishika serikali, basi mwaka 2020 hatutarudi tena madarakani.
"Najua rushwa ipo na mnaendelea kupokea sh laki mbili za 'airtime' (muda wa mawasiliano), ndugu zangu hatutafika, ama wengine watavuka na wengine kukwama," alisema.
Alisema tatizo la rushwa kwa viongozi wa chama hicho linazidi kuwa kubwa kila siku hali ambayo inawapotezea imani wananchi ambao ndio wapiga kura wao.

MAALIM SEIF ATANGAZA KUWANIA URAIS 2015

Seif20hamad201 2f850MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema atagombea urais hadi nguvu zitakapomuishia katika maisha yake.
Mbali na hilo amesema kuwa ataendelea kutetea nafasi yake ya ukatibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaoanza Novemba Mosi mwaka huu.
Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alielezea miaka mitatu ya utendaji wa SMZ katika awamu ya saba ya uongozi wa Serikali hiyo.
"Nitastaafu pale nitakapoishiwa nguvu, wengine wanaona Maalim ni kizingiti, aondoke, nasema siondoki ng'o. Nitaendelea kuwatumikia Wazanzibari na ndiyo ahadi yangu kwao, nasema nikiwa mzima nitagombea urais na ukatibu mkuu wa chama changu.
"Mchakato wa uchaguzi CUF tayari umeanza na utafanyika katika matawi yote Novemba mwaka huu, na uchaguzi mkuu utafanyika mwakani pamoja na mkutano mkuu kati ya Mei na Juni mwakani na Inshaallah nitagombea tena," alisema Maalim Seif.
Akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa na Serikali hiyo ya pamoja inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na Chama cha Wananchi (CUF), alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali hiyo, moja ya mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kupandisha bei ya karafuu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...