SIRI ZA CHADEMA ALIZOZIANIKA MWENYEKITI WA CHADEMA ARUSHA, SAMSON MWIGAMBA
|
MWIGAMBA |
Jina
la ‘Maskini Mkulima’ lilijiunga na mtandao wa jamiiforums mnamo Desemba
27, 2011 na mpaka jana inaonyesha alikuwa ametuma zaidi ya Post 27
ikiwamo hii iliyokuwa na kicha cha habari: Wito kwa wana CHADEMA wote.
Makala hiyo ambayo ndiyo imefanikisha kumbaini ilitumwa Jamiiforums
Oktoba 19 Mwaka huu chini ya kichwa cha habari cha ‘Wito kwa wana
CHADEMA wote!’, inaeleza haya;
Kufuatia malumbano
yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo
tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA
wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama.
Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa
wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr.
Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini
sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.
Naandika nikiwa
mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na
kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana
chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari.
Nimekuwa
mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya
chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika.
Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati
tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake
wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na
Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake. CHADEMA iliyopiga
kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya
vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM
kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC)
kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha
zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake
nini?
Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu
zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu
aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu
hizo?
Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza
wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri
sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na
kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu.
Hawakuwa
madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda
madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate
na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila
mwanachama.
Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa
katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya
kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha
miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili
cha miaka mitano baada ya hapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile
ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili.
Ili kuonyesha kwamba
walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani
kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili
walikaa kipindi kimoja kimoja tu.
Napenda pia kumpongeza
mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama.
Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha
kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani.
Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49.
Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba
agenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa
raslimali, katiba mpya,nk.
Lakini kuna matatizo yameanza
kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata
shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo
asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA.
Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie
wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa
na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao.
Leo nitaainisha mambo machache tu yanayohusiana na fedha za chama na
uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama
wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripoti za fedha
wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati
na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni
mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa
siku nyingine nitakapopata fursa:
1. Wakati tukifanya
mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia
kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya
miaka mitano mitano.
Lakini wakati katiba inachapwa chini ya
uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo
yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa
kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa
sasa.
Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini
kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili,
ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa
nayenye athari zisizomithirika kwa chama.
Ni muhimu
wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho
ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto
kupigania uenyekiti.
Kama kingekuwepo leo Mbowe alikuwa
anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo
kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi.
Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze
kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina
Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi
kuuruhusu si kwa Mbowe, bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa
mwenyekiti wa chama chetu.
2. Matumizi ya fedha za chama:
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya
kakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, katibu Mkuu na
Mkurugenzi wa Fedha.
Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na
mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi
na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum
kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha
bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha.
Watu watatu ndo
wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza
kuu cha mwezi January kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka
serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine
kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa
ipasavyo.
Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na
majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michango ya watu binafsi kama
Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani,
zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje.
Hapo sijataja fedha
zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya
Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha
hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.
3. Taarifa za fedha
Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote
kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi
ya fedha za chama.
Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina.
Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu niliowataja hapo juu na malengo ya
kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua
wao.
Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa
hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa
tumesimama.
4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama
Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada.
Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na
kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za
kuchangisha fedha kwa njia ya matukio.
Mawazo mazuri kama la
kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi
mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi
mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana.
Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa
Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama
wamejifunza chochote.
5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi
Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat.
Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa
kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa
wakuu,wamekubali kuzimwa.
Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete
nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama,
set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana.
Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo
ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi
tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari na
pikipiki zote za M4C.
Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni
80 ambazo mwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama
tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana.
Na
mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti
na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya katibu mkuu kama
mtendaji mkuu wa chama na kamati yake ya tenda. Huu si ufisadi ni nini?
6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa
taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vi
No comments:
Post a Comment