Hospitali ya CCBRT imeguswa na kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ya kutafuta miguu bandia kwaajili ya watu wenye uhitaji kwa kuwapatia matibabu wagonjwa 35 waliokatwa miguu kutokana na ugonjwa wa kisukari.
Miguu hiyo ya kisasa ina thamani ya zaidi ya Shilling Million 157 ambapo kati ya wagonjwa 35 waliokuwa wakitembelea magongo kwa muda mrefu baada ya kukatwa miguu, 21 wameshawekewa Miguu Bandia na sasa wanaendelea na shuguli zao baada ya kuwa wazima.
Makonda amesema lengo la kampeni hiyo ni kusaidia wanaotumia magongo kupata miguu ya bandia ya kisasa ili waweze kuendelea na shughuli zao ujenzi wa Taifa na kuhudumia familia.
Ameishukuru Hospital ya CCBRT kwa kuunga mkono kampeni hiyo pamoja E FM radio na TV E walioojitolea kuhamasisha jamii kuchangia miguu bandia.
Katika hatua nyingine Makonda amepatiwa kiasi cha Shillingi Million 10,000,000 kutoka kampuni ya ujenzi ya Spectum design ambapo Mkurugenzi wake Arch. Jimmy Mkenda amesema lengo la kutoa mchango huo ni baada ya kuguswa na kampeni hiyo inayolenga kuwasaidia waliokata tamaa baada ya kupoteza miguu.
Aidha Makonda amesema kuwa atazungumza na taasisi zinazotoa Bima ya Afya ili waongeze kipengele cha matibabu na kutoa miguu bandia kwa watu waliopoteza miguu kwa ajali au ugonjwa.
Amehamasisha jamii kuchangia kampeni hiyo kupitia CRDB account namba 0150299713500 au kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa au E FM Radio kisha kuwasilisha mchango wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa walemavu Hospital ya CCBRT Brenda Msangi amewaasa wananchi kuchangia kampeni hiyo huku akieleza kuwa wataendelea kushirikiana na Mkuu wa Mkoa.
No comments:
Post a Comment