Wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba wakipitisha Rasimu ya Kanuni za kuendesha Bunge hilo, suala la
aina ya kura kwa ajili ya kuamua masuala mbalimbali, limekwama na
litaamuliwa na wabunge baada ya kuanza kwa vikao rasmi vya Bunge hilo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa
mvutano wa takriban wiki nne kuhusu rasimu, hasa kifungu cha 37 na 38
kinachoeleza aina ya kura kati ya wazi na ya siri.
Hata hivyo, wajumbe wawili wa Bunge
hilo, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Felix Mkosamali wa NCCR-
Mageuzi walisusia kupitisha azimio la kukubali Kanuni za Bunge hilo,
wakidai kusalitiwa katika uamuzi huo na wenzao walioko kwenye Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wajumbe na viongozi mbalimbali wa
vyama vyenye ushawishi bungeni, kwa pamoja waliridhia na kulegeza
misimamo yao ili upatikane mwafaka wa kutengeneza Katiba Mpya ndani ya
wakati. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Wakizungumza kwa nyakati tofauti ndani
na nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, viongozi hao walisema masilahi
ya Watanzania katika mchakato wa Katiba ni ya muhimu kuliko masilahi
binafsi ya makundi.
Kinana asema
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,
Abdulrahaman Kinana alisema pamoja na malumbano makali yanayoendelea
katika Bunge la Katiba, anaamini sasa Katiba itapatikana.
Akizungumza katika mahojiano maalumu
na gazeti hili jana mjini Dodoma, Kinana alisema haoni tatizo katika
malumbano hayo na kwamba anaamini yanatokana na mitazamo tofauti ya
makundi wanayotoka wajumbe. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment