Friday, October 11, 2013

ICC: MAWAKILI WA KENYATTA WATAKA KESI IFUTWE


uhurukenyatta_b6263.jpg
Mawakili wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, wameitaka mahakama ya kimataifa ya jinai kusimamisha mashtaka ya Rais huyo kabla ya kesi yake kuanza mwezi ujao.
Wanasheria hao wamesema mashahidi wa utetezi wamekuwa wakitishwa, na kwamba wanao ushahidi wa kutosha kuthibitisha ukiukwaji wa taratibu za mahakama hiyo.
Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto, wanatuhumiwa kuchochea wimbi la vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Takriban watu1,200 walifariki na wengine laki sita kuachwa bila makao wakati wa ghasia hizo.
Kesi dhidi ya Kenyatta inatarajiwa kuanza tarehe 12 mwezi Novemba.
Naibu Rais pia yuko mbele ya mahakama hiyo na yeye ndiye afisaa mkuu wa kwanza wa serikali kufikishwa mbele ya mahakama ya ICC.
Mawakili wa Kenyatta waliwasilisha nyaraka za kurasa 38 siku ya Alhamisi kwenye mahakama hiyo wakiitaka kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Nyaraka hizo zilisema kuwa upande wa utetezi una ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa mahakama imekua ikiendelea kukiuka taratibu zake.
Pia zilisema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa mashahidi wa upande wa mashitaka na mwengine mmoja walihusishwa na njama ya kutaka kuhujumu sheria.
Mawakili wa uetetzi aidha walituhumu upande wa mashitaka kwa kuwasilisha kesi ambayo ni ya kifisadi na sio ya haki dhidi ya Rais Kenyatta.
Upande wa mashitaka sasa unatarajiwa kujibu madai hayo na mahakama ya ICC huenda ikaamuru jopo la kusikilizwa kwa madai hayo kuyathibitisha.

"TUMETOKA KUFUNGONI NA HAMASA KUBWA".......... MWANANCHI

MwananchiKurudiClip_1a8e4.jpg
Hata hivyo, huu hakika sio wakati wa kumtafuta mchawi, kwa maana ya kutaka kujua nani hasa serikalini alitoa amri ya kulifungia gazeti hili kwa sababu ambazo sisi tunaona hazikuwa na chembe ya mashiko. Tulishangazwa kuona amri hiyo ya Serikali ikitolewa wakati mkuu wa nchi, Rais Jakaya Kikwete akiwa nje ya nchi, tena akiwa katika majukumu mazito ambayo dunia nzima ilikuwa ikiyafuatilia kwa shauku na umakini mkubwa.
Kulifungia gazeti wakati huo hatuoni kama ilikuwa kwa masilahi ya taifa kwa sababu hatua hiyo iliichafua taswira ya nchi yetu na bila shaka Rais Kikwete alijikuta katika wakati mgumu kila alipoulizwa kuhusu hatua hiyo iliyochukuliwa na Serikali yake.
Ni habari zipi zilizolipeleka gazeti hili kifungoni? Habari ya kwanza ilikuwa juu ya waraka kuhusu mishahara mipya ya watumishi wa Serikali ambayo tuliithibitisha pasipo kuacha shaka yoyote kutoka katika vyanzo vyetu vya habari vya kuaminika katika mamlaka za juu serikalini.

HOTUBA ZA BABA WA TAIFA SASA KUPATIKANA KIGANJANI

11_d1a97.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiki akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupata hotuba za Marehemu baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika kwenye hotel ya Double Tree jana. Ili kuweza kupata hotuba za maneno na picha za video unatakiwa kutuma neno Hotuba kwenda namba 15678, pia unaweza kupata huduma hiyo kwa kutumia www.simu.tv/nyerere mobile tv. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Push Media Mobile Freddie Manento
22_c78fe.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Media Mobile, Freddie Manento (katikati) akifafanua jambo kuhusiana na mpango wa kumuenzi marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kupata hotuba zake mbali mbali kwa njia ya simu ya mkononi. Kushoto ni msaidizi maalum wa mkurugenzi mtendaji wa Taasisi mwalimu Nyerere, Gallus Abedi na kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku.
33_5bf0a.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Media Mobile, Freddie Manento (kushoto) na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku wakibadilisha mkataba mara baada ya kusainiwa katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya kupata hotuba za Marehemu baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika kwenye hotel ya Double Tree. Huduma hiyo inamwezesha mwananchi kupata hotuba mbali mbali mbali za marehemu Baba wa Taifa kwa kutuma neno Hotuba kwenda namba 15678. Pia unaweza kupata huduma hiyo kwa kutumiawww.simu.tv/nyerere mobile tv.

BARTON : FERGUSON ALIKUWA HANA UWEZO WA KUPANGA HATA KONI


joey-barton_2698492b_331ce.jpg
Kiungo mtukutu wa Queens Park Rangers Joey Barton ameibuka tena kwenye vichwa vya vyombo vya habari baada ya kudai kocha wa zamani wa Manchester Utd Sir Alex Ferguso hakuwa na uwezo wa kufundisha,
Barton alidai nchini England mameneja wanathaminiwa sana kuliko makocha.
'Sina maana ya kutomuheshimu Sir Alex Ferguson - alikuwa meneja mkubwa lakini hakuwa na uwezo wa kufundisha,
sidhani kama alikuwa na uwezo wa kupanga hata koni. Kuna tofauti kubwa kati ya kocha na meneja'.
Barton pia amesema hakubaliani na wazo la kuundwa kwa tume ya kutafuta njia bora ya kuendeleza soka nchini England.
Akizungumza katika kilele cha mkutano wa Viongozi wa vilabu (Leaders in Sports ) uliofanyika kwenye uwanja wa Stamford Bridge , alisema: 'Timu ya taifa ya England ni mbovu na haiwezi kufanya vizuri hata kama itafuzu fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil.

Thursday, October 10, 2013

SAKATA LA MADAWA YA LAMGEUKIA NEY WA MITEGO.... MAAFISA WA USALAMA WAANZA KUCHUNGUZA NYENDO ZAKE


Rapper Nay Wa Mitego amesema amekuwa akisumbuliwa mno na maafisa usalama pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wanaomdhania kuwa anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kitu ambacho amekuwa akikanusha kwamba sio kweli. Akiongea na Bongo leo kwa njia simu Nay amesema anasikitishwa kupokea taarifa zinazodai kuwa anajihusisha na biashara hiyo haramu, kitu ambacho hakifanyi kwakuwa anategemea shughuli zake za muziki zinazomlipa vizuri.
“Watu wamekuwa wakishangaa sifanyi show hata mwaka mzima lakini maisha yanaenda namiliki gari ndio maana wanaongea mengi huku media na maafisa usalama wananichunguza kila siku,” alisema Nay.
 
Msanii huyo wa Salam Zao amesema yupo kwenye maongezi na kampuni ya simu ili imfanye kama balozi wake.
“Nasubiria mambo yangu yaende poa, nimeingia mkataba wa kuwa balozi wa mtandao wa simu hapa nchini bado muda wake kuuweka wazi kwasababu tupo kwenye makubaliano zaidi na pia ikifika muda nataka kuanika vyanzo vyangu vyote vya mapato, ” alisema.

KENYA: HAKUNA RAIS AMEWAHI KUFIKA ICC


Amina Mohammed amesema kwa kuwa Kenyatta ni rais hali inabadilika kuhusu ICC
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed amesema kuwa hakuna rais hata mmoja aliye mamlakani amewahi kufikishwa mbele ya mahakama ya ICC. Taarifa hii bila shaka imetafsiriwa na wengi kuwa mpango wa Kenya kutokubali Rais Uhuru Kenyatta kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC mwezi ujao.
Duru zinseama kuwa kuwa hofu kuwa huenda Kenyatta akakosa kufika mahakamani kama alivyoamrishwa na mahakama.
Waziri Amina amesema kuwa Rais Kenyatta yuko tayari kushirikiana na mahakama ya ICC lakini kwa kuwa yeye ni rais hali imebadilika. Kenyatta anatakikana na mahakama ya ICC kuhusiana na uhalifu dhidi ya bindamu katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/2008
Bi Abdalla aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku tatu kabla ya mkutano wa Muungano wa Afrika kujadili uhusiano wa Afrika na mahakama ya ICC.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 10, 2013

DSC 0042 ad260
DSC 0033 484f1
DSC 0034 cbb76

VYOMBO VYA HABARI KUTOWAANDIKA WAZIRI MUKANGARA NA MWAMBENE


WanahabariClip_1f73f.jpg
Wadau wa habari nchini wametangaza msimamo wa kutotangaza wala kuandika habari zinazomhusu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari(Maelezo), Assah Mwambene kama sehemu ya kupinga mwenendo wa serikali wa kuvifungia vyombo vya habari.
Wadau hao kutoka taasisi mbalimbali za habari wamesema kuwa pamoja na kilio cha muda mrefu cha kuitaka serikali kufuta Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, lakini hakuna jambo lolote lililofanyika mbali ya kuendelea kuviandama vyombo hivyo.
Katika taarifa yao, wadau hao wamesema pia wamesikitishwa na tabia iliyoonyeshwa na Dk Mukangara na Mwambene kuchukua uamuzi wa kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania bila kuyasikiliza na kupotosha umma juu ya jambo hilo.
"Kwa msingi huo, wadau tumeamua kwamba tutasitisha kuandika, kutangaza na kupiga picha shughuli zozote zitakazowahusisha au kuratibiwa na Dk Mukangara na Mwambene hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. Adhabu hiyo inaanza mara moja kuanzia leo," imesema sehemu ya taarifa hiyo.

AFISA USALAMA ‘FEKI’ ANASWA MTEGONI

IMG 4926 e7e26

Kitambulisho cha Usalama wa Taifa, alichokuwa akitumia, Bw. Magige, kwenye majukumu aliyokuwa akijipangia

IMG 4927 1d844

Bw. Kennedy Magige, anayedaiwa kuwa Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa 'feki' akiwa hoi baada ya kunaswa na kupata kipigo kutoka kwa wananchi.
IMG 6228 779e5

Bw. Magige na mtuhumiwa mwenzake wakiwa kwenye gari la Polisi tayari kupelekwa kituoni

IMG 6245 13f0e

Gari aina ya Land Cruiser Prado, alilokuwa akitumia wakati wa shughuli zake za kila siku  

Watu wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya utapeli , huku mmoja akitumia kitambulisho kinachomtambulisha kuwa ni ofisa mwandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa, wametiwa mbaroni jijini Dar es Salaam.

BERGKAMP ATAKA KUREJEA ARSENAL KUPIGA KAZI

arsenal a88a5
GWIJI wa Arsenal, Dennis Bergkamp ameelezea nia yake ya kujiunga na dawati la makocha la timu ya Arsene Wenger.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 44 alunga mabao 87 katika miaka yake 11 ya kuchezea Arsenal na amesema klabu hiyo ina nafasi maalum moyoni mwake.
Robert Pires amekuwa akisaidia kuendesha mazoezi katika Uwanja wa Gunners, London Colney na Bergkamp, ambaye aliichezea timu hiyo kuanzia mwaka 1995 hadi2006, anaweza kuungana naye.
"Hisia alizonazo Johan Cruyff kwa Barcelona, nami ninazo hizo hizo kwa Arsenal," Bergkamp aliiambia Telegraph.
"Nikiwa Arsenal ilikuwa babu kubwa. Wakati wote nafurahia. Sijawahi kuwa na siku mbaya humo. Ipo katika fikra zangu wakati wote. Ni sehemu ya malengo yangu kurejea huko.
"Naona kama naweza kuwa sehemu ya makocha. Nafurahia hiyo kazi, hususan kufundisha vitu binafasi kwa washambuliaji,".
Bergkamp alijipatia sifa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka, ubunifu na maarifa ya kisoka alipokuwa Arsenal.
Mchezaji mpya ghali wa Arsenal, Mesut Ozil amekuwa akifananishwa na Mholanzi huyo, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi amesema kila mchezaji ni wa kipekee.
Sasa akiwa kocha Msaidizi wa Ajax, Bergkamp amevutiwa na mwanzo mzuri wa Arsenal msimu huu na kusema Ozil ni kipaji maalum.
"Pamoja na heshima zangu zote kwa wachezaji wengine wote wa Arsenal, nafikiri ni mmoja ambaye anaweza kutengeneza tofauti,"alisema.
"Wachezaji wengine ni wazuri katika kiungo. Lakini unahitaji mtu mmoja fulani wa kiwango cha juu ambaye anaweza kuhaha Uwanja mzima,". Chanzo: binzubeiry

CHICHARITO ATAJA SABABU KWA NINI ATAONDOKA MAN U

chicha fe087
MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amesema anaweza kuondoka Manchester United ili kusaka timu ambayo atapata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.


Mshambuliaji huyo anayefahamika kama Chicharito hapewi nafasi kubwa katika klabu ingawa mwezi uliopita aliifungia timu hiyo bao la ushindi katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One dhidi ya Liverpool na zaidi ya mechi hiyo alianza katika mechi nyingine moja tu, United ikifungwa nyumbani na West Brom.
Hernandez amesema kwamba wakati akiwa ana furaha kuchezea klabu kubwa kama hiyo, pia anataka nafasi zaidi za kucheza na anaamini anaweza kuwa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza iwe Old Trafford au katika klabu yoyote.
"Nasotea hiyo [kuanza katika mechi zaidi],"alisema Hernandez akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Mexico, Deportes Telemundo.

Wednesday, October 09, 2013

WAKUU WA KAMPUNI ZA SIMU KENYA WAHOJIWA


zJo-confino-talks-to-Bob-C-001_a088d.jpg
Polisi nchini Kenya wamewahoji maafisa wakuu watendaji wa kampuni za huduma za simu za rununu kuhusu usajili wa kadi za simu za mkononi zinazotumia huduma za kampuni hizo.
Hatua ya polisi imefuatia ripoti kuwa simu zenye kadi ambazo hazikuwa zimesajiliwa zilitumiwa na magaidi walioshambulia jumba la Westgate mjini Nairobi wiki mbili zilizopia.
Wanne hao walitishiwa kukamatwa mnamo siku ya Jumatatu baada ya maafisa wa serikali kuwatuhumu kwa kuuza kadi za simu ambazo hazijsajiliwa.
Hata hivyo walikana tuhuma hizo.
Mnamo mwaka 2010, serikali ya Kenya ilieleza kuwa sharti mmiliki wa simu kusajili kadi yake ya simu ya mkononi katika hatua ya serikali kuzuia visa vya uhalifu wa kutumia simu za mkononi. Hata hivyo sheria ilianza kutekelezwa mwaka jana.
Takriban watu 67 waliuawa kwenye mashambulizi hayo na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mashambulizi yaliyofanywa na kundi la kigaidi la al-Shabab .
Katika taarifa yao ya pamoja, maafisa hao wakuu wa kampuni za huduma za simu,Safaricom, Bharti Airtel, Orange Kenya na Yu Essar – walisema kuwa walitoa taarifa kwa polisi asubuhi ya leo.

WAPINZANI WASITISHA MAANDAMANO

zzzwapinzani_a58b3.jpg
Vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi vimeahirisha maandamano ambayo yalitakiwa kufanyika kesho (Alhamisi).
Vyama hivyo vilipanga kuandamana nchi nzima ili kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete asisaini muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuwa una kasoro nyingi ikiwamo Zanzibar kutoshirikishwa katika mchakato.
Viongozi wa vyama hivyo wamesitisha uamuzi huo baada ya Rais Kikwete kusema yuko tayari kufanya nao mazungumzo kujadili suala hilo.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema hayo Jumanne mara baada ya kukutana na viongozi wenzake katika Ofisi za NCCR-Mageuzi, Ilala Dar es Salaam.
Mbele ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Profesa Lipumba alisema viongozi wa vyama hivyo wametafakari na kuona ni busara kumsikiliza Rais Kikwete kwanza kabla ya kuamua kuendelea na uamuzi wao au la.
"Lengo la kuandaa maandamano ni kuhakikisha kwamba tunapata Katiba bora isiyo na kasoro, ndiyo maana tunaona kwa kuwa Rais ameonyesha nia ya kuzungumza na sisi tumeona ni bora tukakutana naye kwanza," alisema.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 09, 2013

DSC 0010 46ff2
DSC 0011 13794

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...