Akizungumza
na paparazi wetu juzi kwa njia ya simu moja kwa moja kutokea nchini
humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo) alisema muda huo yeye alikuwa nje
ya Hospitali ya St. Helen Joseph ambako mwili wa marehemu ulikuwa
umehifadhiwa kwenye Mochwari ya Hillbrow.
M2 The P akiwa amelazwa HospitaliNI SUMU
Alisema muuguzi mmoja aliyekuwa akimtibu mshirika wa marehemu, Mgaza Pembe a.k.a M2 The P aliyenusurika, alimwambia wawili hao walionekana kuingiwa na kitu cha hatari na kibaya sana mwilini jambo lililowashtua hata madaktari wenyewe.
Mtanzania huyo alidai kuwa hata kama kweli wawili hao walichanganya vileo kama watu wanavyodai, basi ule mchanganyiko ndiyo uliotengeneza sumu mwilini akisisitiza kuwa hilo halina shaka kwa mujibu wa muuguzi huyo.
“Unajua kuna watu wanapenda kuchanganya pombe kali kwa hiyo kuna wanaodai wawili hao walichanganya ‘unga’, bangi na pombe kali.



.jpg)


.jpg)


