Saturday, June 01, 2013

DAKTARI AKIRI NGWEA KAFA KWA KUNYWESHWA SUMU, ADAI KUWA ALITOKWA NA DAMU NYINGI SANA PUANI WAKATI AKIKATA ROHO..!!

KIFO cha msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’, kinaendelea kuibua mapya ambapo sasa sumu imetajwa kuhusika.
Akizungumza na paparazi wetu juzi kwa njia ya simu moja kwa moja kutokea nchini humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo) alisema muda huo yeye alikuwa nje ya Hospitali ya St. Helen Joseph ambako mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa kwenye Mochwari ya Hillbrow.

M2 The P akiwa amelazwa Hospitali
Mbongo huyo alisema alifanikiwa kuutazama mwili wa marehemu Ngwea ambapo ulionesha kuwa wakati wa kukata roho damu nyingi zilimtoka kupitia puani na mdomoni kiasi cha kuwashangaza wauguzi.
 

NI SUMU
Alisema muuguzi mmoja aliyekuwa akimtibu mshirika wa marehemu, Mgaza Pembe a.k.a M2 The P aliyenusurika, alimwambia wawili hao walionekana kuingiwa na kitu cha hatari na kibaya sana mwilini jambo lililowashtua hata madaktari wenyewe.


Alisema muuguzi huyo alimweleza kuwa kitu walichokula au kulishwa kiliwadhuru sana ndani ya miili yao na kusababisha mishipa ya damu kwa Mangwea kupasuka hovyo kwa kuwa moyo ulizidiwa na presha ya msukumo wa damu.
Mtanzania huyo alidai kuwa hata kama kweli wawili hao walichanganya vileo kama watu wanavyodai, basi ule mchanganyiko ndiyo uliotengeneza sumu mwilini akisisitiza kuwa hilo halina shaka kwa mujibu wa muuguzi huyo.
“Unajua kuna watu wanapenda kuchanganya pombe kali kwa hiyo kuna wanaodai wawili hao walichanganya ‘unga’, bangi na pombe kali.

Mchanganyiko huo tu wenyewe ni sumu tosha mwilini kwa binadamu yeyote yule.
“Wataalam wanajua, ukichanganya pombe kali unapata upungufu wa oksijeni katika damu hivyo unaupa moyo kazi ya ziada ya ‘kupampu’ damu kwa kuwa presha inakuwa kubwa. Kwa hiyo kinachotokea ni kupasuka kwa mishipa mikubwa ya damu, ndiyo maana damu zilitoka puani na kinywani kwa wingi.
“Kwa kuchanganya vileo hivyo unatengeneza sumu ambayo husababisha shambulio kubwa la damu na mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi.
“Sasa usipowahishwa hospitali ili kuchomwa sindano ya limao, kifo kinakuwa njenje.
“Kwa vyovyote walikula au walilishwa sumu, daktari anasema mwili wa Ngwea umeharibika sana kwa ndani.
 “Kile siyo kipigo, hakuna jeraha lolote la kupigwa, ile ni sumu,” kilidai chanzo hicho cha kuaminika.

SAA CHACHE KABLA YA KIFO
Habari za kina kutoka kwa mmoja wa watu waliokuwa nao kabla ya kukutwa na tukio hilo zilieleza kwamba kabla ya kwenda kulala, Ngwea na mwenzake, walikutana na baadhi ya Watanzania waishio Sauzi na kupiga stori kwenye baa moja huku wakitaja majina ya wasanii wa Bongo Fleva waliotangulia mbele ya haki.
Ilidaiwa kuwa kila jina la msanii marehemu lilipotajwa Ngwea alikuwa akitamka ‘OMG’ (Ooh! My God) yaani Ooh! Mungu Wangu, bila kujua kitakachomkuta baadaye.

MADAI MENGINE, MAISHA YA SAUZI
Kuna madai mengine kwamba baadhi ya Wabongo waishio Sauzi huwa wana maisha ya kutegana hasa wakijua Mtanzania mwenzao kaenda kule akiwa na ‘mkwanja’ mrefu.
“Tatizo lingine ni kwamba kama walifanyiziwa na mtu huo uwezekano ni mkubwa sana kwani huku jamaa wakikushtukia tu kuwa una mkwanja, kwanza wanakuwa karibu sana na wewe ‘then’ ukikaa vibaya lazima wakutoe uhai.
“Inawezekana akina Ngwea walifanyiziwa kwa kulishwa sumu kwa sababu walikuwa wameshapiga mkwanja tayari kwa kurejea Bongo,” alisema Mbongo huyo.

MCHUNGAJI ALIKIONA KIFO CHAKE MAPEMA!
Mwezi Machi mwaka huu, kupitia gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa la Machi 22-28, 2013 liliandika ukurasa wa mbele habari yenye kichwa; ‘MASTAA WAWILI KUFA MWAKA HUU’ ambapo mchungaji maarufu jijini Dar alisema mwaka 2013  ameona katika maono yake vifo vya wasanii wawili wa Bongo.
Katika habari hiyo, mchungaji huyo alitahadharisha mapema kuwa wasanii wamrudie Mungu kwani upepo siyo mzuri kwao.
Mchungaji huyo alieleza: “Mwaka huu ulipoanza, Januari 2, Sajuki (Juma Kilowoko) aliaga dunia katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa lakini nimepewa maono na Mungu kwamba wasanii wengine wawili watakufa mwaka huu.
“Katika hayo maono niliona wasanii wenyewe, mmoja wa kike, mwingine wa kiume. Wa kike ni msanii wa filamu, wa kiume anaimba hizi nyimbo za kisasa za Bongo Fleva.
“Huyo wa Bongo Fleva siyo mkongwe sana kama wale waanzilishi wa fani hiyo lakini anajulikana sana na mashabiki wengi. Nyimbo zake zinajulikana pia.
“Huyu wa kike yeye ni mkongwe kidogo, halafu ni mweusi, zamani aliwahi kuwika sana lakini kwa siku za hivi karibuni amepoapoa.”

MANENO YAKE YALIJAA UTABIRI
Watu wa karibu waliokuwa wakichati na Ngwea kupitia mitandao ya kijamii walisema siku za mwisho wa uhai wake, marehemu alipenda kutumia maneno yenye kumtaja Mungu, Yesu au viashiria vingine vinavyofanana  na hivyo.

TURUDI KWENYE TUKIO
Habari zilieleza kuwa baada ya majibu ya kilichomuua Ngwea kujulikana, mwili wa staa huyo utaagwa kesho jijini Dar ambapo msiba upo kwa kaka yake Mbezi Beach na baadaye mwili utasafirishwa kwenda mkoani Morogoro eneo la Kihonda, nyumbani kwao.

NGWEA HAPA, BABA’AKE PALE
Habari kutoka msibani Morogoro zimeeleza kwamba marahemu Ngwea atazikwa jirani kabisa na kaburi alilozikwa marehemu baba yake, mzee Kenneth Mangwea. Huo ni ushauri wa familia yake.

HALI YA M2 THE P
Kwa upande wake, M2 The P, hadi gazeti linakwenda mitamboni alikuwa akiendelea na matibabu huko Sauzi huku hali yake ikisemekana inaendelea kuimarika.
Ngwea alizaliwa Novemba 16, 1982 huko mkoani Mbeya (asili yake ni Mkoa wa Ruvuma) akiwa mtoto wa mwisho katika familia yao. Hajaacha mke wala mtoto.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...