INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili
mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo
wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.
Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi
jijini Dar es Salaam ameingia katika dimbwi la AIBU baada ya kunaswa
akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.
Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti
huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili)
katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye
alikuwa safarini.
Chanzo chetu cha habari kilipiga simu chumba cha
habari na kueleza juu ya tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo
chumbani kwake tena akiwa kwenye sare za shule.