Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani jana.Picha na Ikulu
Kikwete alimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya wapiganaji wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na Jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini humo katika hafla iliyofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani jana. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange ni miongoni mwa mashuhuda katika hafla hiyo.
“Ninawatakia kila la kheri kwenye mapambano,” Amiri Jeshi Mkuu alimwambia kiongozi wa Batalioni ya Wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda nchini humo. Tanzania inaungana na Afrika Kusini na Malawi kufanya kuwapo kwa kikosi cha askari 3,100 huku Tanzania ikipeleka askari 850 kwa ajili ya kazi hiyo.
Vikosi vya awali vya Tanzania vimekwishatangulia nchini humo vikiongozwa na Jenerali James Mwakibolwa anayeongoza Brigedi hiyo chini ya UN, na tayari amewasili kwenye Mji wa Goma, ambao ndio Mji Mkuu wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini unaokaliwa na waasi wa M23 tangu Aprili 2012.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Monusco, vikosi vingine vya wapiganaji wa Tanzania na Afrika Kusini vitawasili wiki ijayo wakati Wanajeshi wa Malawi haijafahamika tarehe ya wao kuwasili.
Msemaji wa wapiganaji wa M23, Kanali, Vianney Kazarama alikaririwa akisema: “Tuko tayari kwa mapambano, wapiganaji wako kambini Rumangabo, wakifanya mazoezi makali ya kushambulia, kujilinda na mbinu za kukabiliana na adui pamoja na kucheza kung fu.
Msemaji wa wapiganaji wa M23, Kanali, Vianney Kazarama alikaririwa akisema: “Tuko tayari kwa mapambano, wapiganaji wako kambini Rumangabo, wakifanya mazoezi makali ya kushambulia, kujilinda na mbinu za kukabiliana na adui pamoja na kucheza kung fu.