MAJASUSI wa shirikisho la ujasusi la nchini Marekani wamefika jijini Arusha kusaidiana na wapelelezi wa nchini Tanzania katika uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa bomu kwa waumini wa kanisa katoliki na Balozi wa Vatican nchini siku ya jumapili.
Magesa alitoa taarifa hiyo wakati akitoa taarifa ya Mkoa kwa waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipozuru eneo la tukio na kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali na kuwapa pole.
Wakati maafisa hao wakifika jijini humo tayari vyombo vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 10 miongoni mwao wakiwemo watu wanne kutoka Saudia Arabia ambao waliwasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) siku moja kabla ya tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa watu hao walikamatwa muda mfupi wakiondokanchini kupitia mpaka wa Namanga kuelekea nchini Kenya baada ya tukio kutokea.
Hata hivyo taarifa hiyo haikuweza kutoa ufafanuzi zaidi na kwamba taarifa zaidi juu ya upepelezi zitatolewa kadri muda na wakati utakavyoruhusu.
No comments:
Post a Comment