Wednesday, March 27, 2013

ROSE NDAUKA: KAJALA AJIPANGE KUTIMIZA NDOTO ZAKE


Habari na saluti5
NYOTA wa filamu, Rose Ndauka amemzungumzia msanii mwenzie wa filamu, Kajala Masanja aliyeponea chupuchupu kwenda jela miaka mitano na kusema kuwa, anachoamini ni kwamba sasa Kajala atajipanga na kuyafanya maisha yake yaende kama alivyokusudia hatimaye kutimiza ndoto zake.Saluti5 ilizungumza na Rose ili kupata maoni yake juu ya kuachiwa huru kwa Kajala aliyekuwa jela kwa muda mrefu, ambapo alisema kuwa kikubwa ni kushukuru mungu kwa kuweza kwake kurudi tena uraini, lakini pia sasa ni wakati wa kuzijenga upya ndoto zake.
“Binafsi, siwezi kujua kwa sasa Kajala mwenyewe amepanga kitu gani juu ya maisha yake, lakini ninaamini atafanya yale anayayowaza katika akili yake, hususan kuhusiana na kuendeleza mipango yake ya kimaisha,” alisema Rose.

UGONJWA UTOKANAO NA KUWEKA LAPTOP MAPAJANI HUU HAPA

HATARII...UGONJWA UTOKANAO na KUWEKA  LAPTOP MAPAJANI MWAKO PINDI UTUMIAPO.Huu ndo ugonjwa utokanao na kuweka laptop mapajani.Kwa faida ya afya zetu thechoice inawakumbusha kuepuka kutumia laptop kwa mtindo huo na yakupasa kutumia mbinu mbadala ili kuweza kulinda afya zetu.

DEREVA ALIYEMGONGA TRAFIKI ENEO LA BAMAGA AFIKISHWA MAHAKAMANI







Akiteta jambo na Issa Mnally  ndani ya mahakama kabla ya hakimu kuwasili. 

  Waandishi wa habari wakimpiga picha (Simbo) wakati akiingia mahakamani

JK: afunga rasmi mafunzo ya JKT ya muda mfupi kwa wabunge RUVU JKT

8E9U3088Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo  yaliyofanyika kwa wiki tatu.(Picha na Freddy Maro)

8E9U3018
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.

RAIS KIKWETE AKAGUA MIRADI YA UZALISHAJI JKT RUVU

8E9U3121Mwakilishi wa Wabunge waliomaliza mafunzo maalumu ya muda mfupi ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)katika kambi ya RUVU Ester Bulaya akikabidhi risala kwa niaba ya wenzake kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana.8E9U3133Wabunge waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mris8E9U3151Wabunge waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho kikwete wakati wa gwaride maalumu la kumaliza mafunzo hayo huko kambi ya RUVU leo.8E9U3177Wabunge walihudhuria mafunzo ya muda mfupi Ruvu JKT wakionesha walijifunza kwa

Tuesday, March 26, 2013

SANAMU YA KANUMBA KUWEKWA BAGAMOYO, SOMA STORY HAPA

Steven-Kanumba
Of course Steven Kanumba had so much fans kwenye hii tasnia ya filamu za Bongo and he could defenetely take ‘Bongomovie’ somewhere far na ndio maana anakumbukwa kutokana na ku-inspire wengi.
Taarifa zisizokuwa rasmi kitaani kwasasa ni kwamba kwenye maazimisho ya mwaka mmoja wa kifo cha the late steven kanumba mwaka huu huenda ikatengezwa sanamu yenye sura yake na kuwekwa kwenye mji wa kihistoria wa bagamoyo Mkoani Pwani.

Muigizaji Stevene Kanumba alifariki mwezi April mwaka jana 2012 nyumbani kwake Sinza Vatkan dar es salaam akiwa na umri wa miaka 28 baada ya majibizano na mpenzi wake Elizabeth Michael ‘lulu’ ambae pia ni muigizaji.

MCHORO WA KUMUUA ASKOFU MOKIWA


MCHORO uliosanifiwa na watu ambao inaaminika walitaka kumuua Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,  Dk. Valentino Mokiwa ni hatari.

 
Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,  Dk. Valentino Mokiwa.
Taarifa za kila upande, zinathibitisha kwamba mchoro huo ulisanifiwa kitaalam na kwamba kilichomwokoa Mokiwa ni Mungu.
Imebainika kuwa kingine kilichonusuru maisha ya Mokiwa ni muundo wa nyumba yake, kwani baada ya majambazi kumshambulia kwa mapanga mlinzi wake, iliwawia vigumu kuifikia nyumba ambayo kiongozi huyo wa kiroho alikuwemo.

MCHORO WENYEWE
Uchunguzi unaonesha kwamba uvamizi nyumbani kwa Mokiwa, Mbezi kwa Yusuf, Dar es Salaam, Machi 9, mwaka huu haukuwa wa bahati mbaya kwani uliandaliwa mapema.
Pikipiki ambayo namba zake hazikunakiliwa, inatajwa kuhusika na upangaji wa uvamizi huo kwani siku ya tukio ilikaribia nyumba ya Mokiwa takriban mara tatu.

WANAFUNZI 10,000 WALIOKATA RUFAA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE-2012 WAMEFELI TENA

Wakati tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012 ikiendelea na kazi, imebainika kuwa wanafunzi waliokata rufaa kutaka mitihani yao isahihishwe upya wamefeli zaidi baada ya
kusahihishiwa.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa, wanafunzi waliokata rufaa wamefeli zaidi na hata walioongezewa alama matokeo hayakubadilisha madaraja waliyopata awali.Habari zinaeleza kuwa, wanafunzi waliokata rufaa NECTA kutaka mitihani yao isahihishwe upya ni takribani 10,000 na kwamba baraza bado limetoa muda zaidi kwa wengine wanaotaka kukata rufaa.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya NECTA viliieleza NIPASHE kuwa mitihani kwa wanafunzi waliokata rufaa ilianza kusahihishwa Machi 12 na kuhitimishwa Machi 15, mwaka huu na kwamba wengi wamefeli zaidi.“Baada ya wanafunzi kadhaa kukata rufaa, NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika masomo yote na kuanza kufanya kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya kwa umakini, kilichowashangaza walimu hao ni kuona kiwango cha kufeli kimeongezeka,” alisema ofisa mmoja wa NECTA ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa maelezo kuwa siyo msemaji wa baraza hilo.

ABOMOLEWA NYUMBA NA KUCHOMEWA VYOMBO VYA NDANI AKIDHANIWA MSHIRIKINA ILEMI MBEYA

Wananchi wenye hasira kali wakibomoa nyumba ya mama Atupele Kalile akidhaniwa kuwa mchawi maeneo ya ilemi Mbeya
Wengine wameshaingia ndani na kuanza kutoa vyombo nje tayari kwa kuvichoma
Mtoto wa mama Atupele akijaribu kuokoa vitu vya mama yake visichomwe moto na wanakijiji
Vyombo vinazidi kutolewa ndani ilivichomwe moto
Wamefyeka shamba lake lote la mahindi
Wengine wanapongezana kwa kazi waliofanya
Kushoto mama Atupele Kalile anaedhaniwa kuwa ni mshirikina akiwa na mtoto wake
MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Atupele Kalile (60) mkazi wa Mtaa wa Masewe Kata ya Ilemi Jijini Mbeya amenusurika kifo baada ya wananchi wa Mtaa huo kutaka kumpiga kisha kubomoa nyumba yake wakimtuhumu kwa ushirikina.
  
Wananchi hao kumtuhumu Mwanamke huyo kuhusika na upotevu wa motto mwenye umriwa miaka mitatu(3) (Judith Chengula) aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Februai 22, Mwaka huu.
  
Kwa mujibu wa wakazi hao walisema Mtoto huyo alipotea majira ya saa 11 jioni baada ya kupoteana na dada yake  Anitha Mgaya wakiwa wametokea kanisani ambapo hadi sasa mototo huyo hakuweza kupatikana licha ya juhudi kubwa za wakazi hao kumtafuta bila Jitihada. 
Walisema katika vikao kadhaa vilivyoitishwa mtaani hapo kwa ajili ya kutafuta mbinu za kupatikana kwa mtotolakini Mwanamke huyo hakuonesha ushirikiano jambo ambalo lilizua hofu miongoni mwa wakazi hao hali iliyopelekea kuhisiwa kuhusika na tukio hilo.
  
Walisema katika kikao kilichofanyika Machi 23 Mwaka huu majira ya Asubuhi mtaani hapo wananchi hao waliendelea kusisitiza kuwa Mwanamke huyo achukuliwe hatua kwa kuwa ndiye anayehusika na upotevu wa motto ambapo iliamriwa kwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi.
  
Walisema baada ya kufika nyumbani kwake na kufanya upekuzi walikuta vitu vinavyohisiwa kuwa vinahusika na ushirikina ambavyo ni vitovu vya watoto wachanga watatu ambapo Mwanamke huyo baada ya kuulizwa alishindwa kutolea ufafanuzi hali iliyosababisha wananchi kupandwa na hasira na kuanza kumpiga.

WABUNGE ZITTO, AZAN WAMALIZA MAFUNZO YAO YA JKT KAMBI YA MGAMBO 835KJ LEO


Mbunge wa Kigoma CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo wakemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 835KJ kilichopo Mkoani Tanga.

Pichani juu ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha chini akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake  Iddi Azan, Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.
Aidha Zitto Kabwe amesema anafuraha iliyo pitiliza kumaliza mafunzo hayo na ameweka historia ya kubwa katika maisha yake hii leo. Anapasha zaidi katika wakati wa Zoezi la kulenga shabaha alifanikiwa kulenga risasi 3 akiwa amelala, 3 akiwa amepiga magoti na 1 akiwa amesimama. NA FATHER KIDEVU

UAMSHO WASOMEWA KESI UPYA

Na Salma Said Zanzibar
KESI ya jinai inayowakabili viongozi wa Dini wa Jumuiya ya Uwamsho na Mihadhara imeanza kusomwa upya jana katika mahakama Kuu ya Zanzibar.

Kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2012 ilisomwa mbele ya Jaji Fatma Hamid Mahmoud na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Bw. Ramadhan Nassib, ambae aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Farid Hadi (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52) mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47)
mkaazi wa Makadara na Azan Khalid (48) mkaazi wa Mfenesini mkoa wa Mjini wa Magharibi Unguja.
Wengine ni Suleiman Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe na Abdallah Said (48) mkaazi wa Misufini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Washitakiwa wote kwa pamoja walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kuharibu mali, Uchochezi, Ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la ttatu ni kula njama ya kufanya kosa huku kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne Azan Khalid ambae anadaiwa kufanya vitendo
vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa Amani.
Makosa yote hayo yandaiawa kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 katika maeneo tofauti ambapo washitakiwa hao walipotakiwa kujibu tuhuma zao walizikana.
Mara baada ya kuwasomea mashtaka yao hayo Mwenesdha Mashtaka wa Serikali Bw. Nassib alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo tayari umeshakamilika lakini hata hivyo aliiomba mahakama hiyo kufanya subra ya kuweza kuamuwa maamuzi yoyote kutokana na upande huo wa mashtaka kukata rufaa kitendo ambacho alisema kwamba iwapo mahakama hiyo  itaendelea na kesi hiyo kunaweza mahakama ya rufaa ikatoa maamuzi ambayo yataweza kuathiri maamuzi ya mahakama hiyo.
Kwa upande wa mawakili wa watetezi uliokuwa ukiongozwa na Bw. Taufik Salum uliiomba mahakama hiyo kuwapatia dhamana washitakiwa wake haohasa ikiangaliwa kuwa tayari washitakiwa hao wameshakaa ndani kwa muda mrefu.
“Mhe Jaji tumefurahi kuona kwamba kwa mara ya kwanza upande wa mashtaka unatamka kuwa upelelezi umekamilika lakini isiwe sababu ya kuendelea kubakia rumande wateja wetu kwa vile muda wa kukaa kwako umekuwa mwingi na kupelekea haki yao ya msingi ya dhamana kunyimwa”,
alisema Bw. Salum.
Hata hivyo Jaji Mahmoud alisema kuwa atayachukuwa maombi ya pande yote mbili na kuyapitia kwa umakini ili baadae aweze kutoa maamuzi yaliyosahihi kutokana na kuwa ni mgeni wa kesi hiyo na jalada lake amelipokea kwa muda mchache ambao haukpata nafasi ya kuipitia.
“Nayachukuwa maombi yote mawili nitayatafakari kwa kina na kuja kutoa maamuzi unaofaa”, alisema.
Hata hivyo Jaji huyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 27 mwaka huu.

HABARI KUHUSU KUVUNJIKA KWA KUNDI LA P. SQUARE...!!!

P-Square1-460x396
Kumekuwa na uvumi kuhusu wasanii wanaoliunda kundi la muziki la PSquare kutengana kiasi cha mashabiki wao kubaki wameduwaa.
Hata hivyo Peter na Paul Okoye wameweka wazi kuwa huwa wanaingia kwenye mitafaruku hadi kufikia hatua ya kupigana makonde huku kila mmoja akitishia kutengana lakini wakadai kwamba kama ni kutengana ambae angeweza kuwatenganisha ni mama yao pekee.

Wawili hao wamesema kuwa mama yao aliwalea na kuwaonyesha upendo na mapenzi na kama ingetokea kuwa siku moja itatokea PSquare watatengana basi yatakuwa ni maamuzi ya wazi na kama mmoja wao ataamua kustaafu muziki basi haimaanishi kuwa wataacha kusaidiana.

Tanzania yaahidiwa misaada bila masharti

Rais Xi Jinping wa China ameahidi kuendelea kuipiga jeki Afrika ili kukabiliana na changamoto za kimaendeleo, huku akisema kuwa suala la utoaji misaada yenye masharti magumu siyo ajenda ya Serikali yake. Jinping akitumia jukwaa la Tanzania kutambulisha sera yake kwa nchi za Afrika alisema kwamba bara hilo limepiga hatua kubwa kimaendeleo na kwamba nchi yake itaimarisha uhusiano uliopo kwa manufaa ya pande zote mbili.
Alisisitiza kwamba ushirikiano wenye tija ni ule unaozingatia “majadiliano na maridhiano” na kwamba Serikali yake imetenga kiasi cha Dola za Marekani 20 bilioni kufadhilia miradi mbalimbali ya maendeleo Afrika.
“China haitakuwa tayari kutoa masharti kwa taifa lolote… Tunataka kutoa fursa zinazofanana,” alisema Rais, ambaye alishika rasmi wadhifa huo Machi 14, mwaka huu. Alisema China haitaingilia masuala ya ndani ya nchi, huku akisisitiza kwamba shabaha ya nchi yake ni kuendelea kupalilia ushirikiano mwema uliodumu kwa miongo kadhaa na siyo kujihusisha na migogoro.
Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanadai kuwa, kauli ya kiongozi hiyo ni kama ujumbe wa onyo kwa baadhi ya nchi za Magharibi ambazo zinalalamikiwa kuendesha sera zinazominya ustawi wa Afrika.
Mhadhiri katika Chuo cha Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa (CFR), Dk Ahmed Mtengwa alisema: “Ni hotuba inayofungua njia kwa Afrika..., amezungumzia ushirikiano unaolingana yaani `win win situation’ (kila upande ufaidike), hivyo kwangu ninayaona matumaini.”Rais Jinping, aliyekuwa katika ziara ya siku mbili nchini na juzi usiku alisaini mikataba 17 inayohusu sekta za kilimo, afya na miundombinu.
Mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani ni kati ya miradi mikubwa iliyomo kwenye makubaliano hayo na ujenzi wake utafanywa na Kampuni ya Merchants Holding ya China na utakwenda sanjari na ujenzi wa barabara inayounganisha bandari hiyo.
Pia katika bandari hiyo itaunganishwa na Reli ya Kati na na ile ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) ili kurahisisha usafiri wa mizigo ndani na nje ya nchi. Mikataba mingine itahusiana na uboreshaji wa sekta ya viwanda, kilimo hasa kile cha tumbaku ikiwamo kuwatafutia soko wakulima kutoka Mikoa ya Tabora na Ruvuma ili waweze kuuza zao hilo katika soko la China pamoja na kulipatia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zana za kufanyia kazi.
Rais huyo, ambaye Tanzania ndiyo nchi ya kwanza barani Afrika kuitembelea, alizindua na kukabidhi rasmi Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere kilichoko jijini Dar es Salaam ambalo ni jengo la ghorofa tatu na lenye kumbi nne za mikutano zenye uwezo wa kuchukua watu 1,800 kwa wakati mmoja.
Ujenzi wa kituo hicho uligharimu Dola za Marekani 29.7 milioni zilizotolewa na Serikali ya China kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Rais huyo alisifu ushirikiano wa muda mrefu baina ya taifa lake na Tanzania na kusisitiza kuwa nchi hizo zitaendelea kusaidiana kama sehemu ya kuenzi misingi iliyowekwa na waasisi wa mataifa haya mawili, Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tse Tung.
Rais Jinping aliondoka jana jioni kwenda Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa tano wa Wakuu wa Nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi ikiwamo Brazil, Urusi, India, China na Afrika ya Kusini (BRICS).

Chanzo - Mwananchi

NGUMI ZITAPIGWA BUNGENI: NDESAMBURO

MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, (CHADEMA), amewataka Watanzania watarajie mapanbano makubwa zaidi bungeni, hata ikibidi ngumi kupigwa, ili kuleta ustaarabu na kutetea haki ya kidemokrasia katika chombo hicho cha kutunga sheria.
Ndesamburo ambaye amekuwa bungeni tangu mwaka 2000, alisema hayo jana katika mahojiano mafupi na gazeti hili, ofisini kwake Moshi Mjini.
Alisema nyakati zimebadilika na wabunge wa mwaka 2013 si sawa na wa mwaka 2000; kwani hawa wa sasa hawako tayari kuona kanuni zinavunjwa waziwazi.
Ndesamburo alikuwa akizungumzia kauli ya Spika wa Bunge, Anna Makinda, na Naibu wake, Job Ndugai, ambao wanadai kuwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ni vinara wa fujo bungeni.
Alisema siasa za sasa ni za vijana, si za wazee kama ilivyokuwa huko nyuma na kwamba wazee wanapaswa kuelewa kuwa nyakati zimebadilika.
Alisema kwamba katika siasa za kuelekea mwaka 2015, CHADEMA ina nafasi kubwa ya kushinda ili kuwaletea Watanzania maendeleo waliyokosa kwa miaka zaidi ya 50.
Alisema: “Lazima tujifunze kubadilika, hizi ndizo siasa za wakati huu. Watu wasidhani vijana hawa wa CHADEMA, hata vijana wa CCM… maana yake kitu kimoja ambacho nimekiona, kama tunajaribu kufikiria sasa, watu wasidhani ni CHADEMA… lakini kule ndani mpaka vijana wa CCM wanafanya vurugu. Ukitazama ile filamu iliyoletwa na TBC ilionyesha CHADEMA tu haikuonyesha upande wa CCM walioshangilia, haikuonesha kabisa; jambo ambalo si sahihi.
“Kwa hiyo watu wajifunze kwenda na wakati. Zamani Bunge lilikuwa limetawaliwa na wazee. Sasa kuna vijana. Vijana ni tofauti na wazee. Lazima wazee waanze kujua vijana wanataka nini. Sheria na kanuni zinazoendesha Bunge, vijana wanazijua, zinapovunjwa ni rahisi kuelewa. Zamani hakuna aliyekuwa anajali hilo.
“Hizi fujo ni demokrasia. Bunge linashika hamasa, limekuwa zuri. Wala wasione haya. Hii ni mwanzo tu, tutaona mengi hata ngumi zitapigwa mle ndani. Ndiyo ustaarabu, hilo ndilo Bunge. Unaponyimwa haki yako, unataka mtu afanyeje?”
Katika Bunge la Februari, Bunge lilitawaliwa na fujo, baada ya Spika wa Bunge, Anna Makinda, na Naibu Spika, Job Ndugai, kuliendesha Bunge kinyume cha kanuni na kusababisha kuzomewa na wabunge wa upinzani waliodai Spika na naibu wake wanapinda kanuni.
Mjadala mkali ulianza wakati wa kujadili hoja binafsi za mbunge wa Ubungo, John Mnyika, mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, na Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, James Mbatia. Uongozi wa Bunge uliahirisha shughuli za Bunge mara kadhaa baada ya hali ya kutoelewana na ubishi mkali kutokea ndani ya Bunge.
Akizungumzia hali hiyo, Makinda alinukuliwa akisema, “Hata hivyo, imelazimu kuahirisha mijadala ya hoja binafsi kutokana na tabia iliyojitokeza ya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wabunge na hivyo kuamua kwa makusudi kuanzisha vurugu na hivyo kulifanya Bunge lianze kupoteza heshima yake ya kibunge.”
Alisema hoja binafsi za wabunge zinaongozwa na kanuni za Bunge kuanzia kanuni ya 53 hadi 58, na kanuni za majadiliano zinaongozwa na kanuni kuanzia 59 hadi 71 ambazo kwa ujumla wake zikifuatwa kama inavyotakiwa vurugu haiwezi kutokea bungeni.
Makinda ambaye alionekana kuzungumza kwa jazba, alisema katika mkutano huu imeonyesha waziwazi baadhi ya wabunge kwa makusudi na kwa nia ya kupotosha wananchi wanatumia vibaya kanuni hizo na wakati mwingine kuwadanganya wananchi ambao kwa bahati mbaya kanuni hizi hawazifahamu.
Ubabe huo wa Spika na naibu wake ulisababisha kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2010, wabunge wa vyama vya upinzani kuungana kumsusa Spika na Naibu Spika, wakipinga hatua yake ya kupindisha hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani.
Wabunge wa vyama vya upinzani waliotoka kupinga ubabe wa Spika kinyume cha kanuni ni wa vyama vya CHADEMA, CUF, UDP, TLP na NCCR-Mageuzi ambao waliungana kwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kupinga hatua ya Ndugai kuwaburuza katika kupitisha hoja ya Mbatia.
Hoja hiyo binafsi iliyoainisha udhaifu katika mfumo wa elimu nchini, iliwasilishwa na kuibua mjadala mzito bungeni, huku kambi ya upinzani ikikubali hoja ya Mbatia kutaka kuunda kamati teule wakati wabunge wa CCM wakipinga, hoja iliyosababisha hadi sasa Wazairi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda tume inayotafuja tatizo la kufeli kwa wanafunzi wa mwaka 2012.
SOURCE TANZANIA DAIMA

Mahakama yaamuru matokeo ya urais Kenya yachunguzwe

Nairobi. Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya nchini Kenya imeagiza kuchunguzwa kwa fomu 34 za matokeo ya uchaguzi wa rais kutoka katika vituo vyote 34,400, vilivyotumika kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Machi 4, mwaka huu.
Kadhalika mahakama hiyo jana iliagiza kuhesabiwa upya kwa kura za urais katika vituo vya kupigia kura 22 kati ya elfu 33 vilivyolalamikiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Muungano wa Cord, Raila Odinga.
Katika malalamiko yake yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo kupinga Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Machi 4, Odinga alidai kuwa vituo hivyo 22 kura zilizopigwa zinazidi idadi ya wapigakura walioandikishwa.
Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya majaji wenzake watano, Jaji Smokin Wanjala alisema kwamba uhesabuji kura wa vituo hivyo utafanyika leo kuanzia saa 2.00 asubuhi kwa lengo la kubaini ukweli kuhusu madai hayo.

“Matokeo ya kura zitakazohesabiwa katika vituo hivyo 22 yawasilishwe katika mahakama hii Jumatano, saa 10.00 jioni,” alisema Jaji Wanjala.
Kikao hicho, ambacho Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande amealikwa kama mwangalizi, ni cha awali kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa rasmi keshokutwa (Alhamisi) na kuendelea kwa mfululizo hadi kufikia uamuzi ikiwa madhumuni yake.

Lengo ni kupitia madai yaliyowasilishwa mahakamani hapo na pande zote zinazohusika na kuamua mwenendo wa kesi utakavyofanyika.
Ukiachilia mbali kesi iliyofunguliwa na Odinga kupinga Kenyatta kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa tano tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa Kenya, kuna kesi nyingine ambayo imefunguliwa na muungano wa mashirika yasio ya kiserikali, `The African Centre for Open Governance’ (Africog).
Katika kesi hiyo inayorushwa moja kwa moja na vituo kadhaa vya televisheni nchini Kenya, Africog inahoji uhalali wa uchaguzi huo.
“Kesi yetu haihusiani na nani ameshinda au kushindwa bali jinsi umma ulivyoshindwa, tumepoteza ahadi ya uchaguzi uliowazi,” alisema Gladwell Otieno, Mkurugenzi Mtendaji wa Africog.
Kesi ya tatu ambayo imefunguliwa na wajumbe wa timu ya kampeni ya Kenyatta, mwanaharakati katika mitandao ya kijamii Dennis Itumbi na Moses Kuria wanaopinga uamuzi wa Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya kujumuisha kura zilizoharibika wakati wa kujumlisha kura za wagombea urais.
Katika uamuzi wake, mahakama iliamua kwamba kesi zote tatu zitaunganishwa kuwa moja, huku ile iliyowasilishwa na Odinga ikiwa ndiyo kinara wa kesi zote.
Pia mahakama iliamuru Muungano wa Vyama vya Siasa wa Cord na Jubilee kuteua mawakala 10 kila mmoja ambao watakula kiapo mahakamani hapo kabla ya kuanza kuhesabu upya kura hizo.
Katika uamuzi wake jana jioni, mahakama hiyo ilikubali ombi la Mwanasheria Mkuu wa Kenya, kushiriki katika kesi hiyo kama rafiki wa mahakama na siyo mdaiwa kama ilivyokuwa awali. Wakili wa Cord, George Oraro alikubali uamuzi huo licha ya kuupinga awali.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...