Wakati tume ya kuchunguza
matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012 ikiendelea na kazi,
imebainika kuwa wanafunzi waliokata rufaa kutaka mitihani yao
isahihishwe upya wamefeli zaidi baada ya
kusahihishiwa.Kwa mujibu wa
taarifa kutoka ndani ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa,
wanafunzi waliokata rufaa wamefeli zaidi na hata walioongezewa alama
matokeo hayakubadilisha madaraja waliyopata awali.Habari zinaeleza kuwa,
wanafunzi waliokata rufaa NECTA kutaka mitihani yao isahihishwe upya ni
takribani 10,000 na kwamba baraza bado limetoa muda zaidi kwa wengine
wanaotaka kukata rufaa.
Vyanzo vya habari kutoka ndani
ya NECTA viliieleza NIPASHE kuwa mitihani kwa wanafunzi waliokata rufaa
ilianza kusahihishwa Machi 12 na kuhitimishwa Machi 15, mwaka huu na
kwamba wengi wamefeli zaidi.“Baada ya wanafunzi kadhaa kukata rufaa,
NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika masomo yote na kuanza
kufanya kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya kwa umakini,
kilichowashangaza walimu hao ni kuona kiwango cha kufeli kimeongezeka,”
alisema ofisa mmoja wa NECTA ambaye aliomba jina lake lisiandikwe
gazetini kwa maelezo kuwa siyo msemaji wa baraza hilo.
Wakizungumza na NIPASHE,
baadhi ya walimu walisema walioshiriki kusahihisha mitihani hiyo
walisema kuwa maoni yaliyokuwa yanatolewa na baadhi ya watu kwamba
matokeo mabaya ya mtihani huo yalitokana na uchakachuaji, hayakuwa ya
kweli.Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na
NIPASHE jana alithibitisha kuwa mitihani ya wanafunzi waliokata rufaa
ilianza kusahihishwa Machi 12 mwaka huu.
Dk Ndalichako alisema hata
hivyo, hana taarifa kama matokeo ya wanafunzi hao yanaonyesha kuwa
wanafunzi wengi wamefeli zaidi kwa kuwa alikuwa safarini
kikazi.“Unavyozungumza na mimi nipo Arusha na wageni, sifahamu kama
baada ya kusahihishwa upya mtihani wa wanafunzi waliokata rufaa matokeo
yamekuwaje, nitafahamu baada ya kurejea Dar es Salaam Jumatano wiki
hii,” alisema Dk Ndalichako ambaye hata hivyo, hakutaja idadi ya
wanafunzi waliokata rufani.Dk Ndalichako alisema suala la kufeli zaidi
wanafunzi waliokata rufaa linawezekana kutokea kwa sababu kila mwaka
imekuwa ikijitokeza hali kama hiyo, hivyo ni jambo la kawaida
NIPASHE
No comments:
Post a Comment