MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe,
akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kakola, mahali
ambapo mgodi wa dhahabu wa Buzwagi unapatikana, Emmanuel Bombeda
anayetokana na chama hicho, wakati kiongozi huyo mkuu wa CHADEMA
alipokuwa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama hicho, baada ya
kuwasili mkoani Shinyanga, kwenye kikao cha Baraza la Uongozi Kanda ya
Ziwa Mashariki (Mara, Shinyanga na Simiyu). Mbowe anatarajiwa kufanya
mkutano wa hadhara Mjini Shinyanga, kufanya uzinduzi wa kanda hiyo.
Sunday, March 17, 2013
Saturday, March 16, 2013
HEBU ANGALIA WASANII TUNAOWAITA KIOO CHA JAMII
Kuna msemo
unasema wasanii kioo cha jamii je ni kweli?hili ni kava linalobeba kazi
za wasanii kwa hali kama hii bado tunadhubutu kusema wasanii ni kioo cha
jamii? Mimi naona waitwe waharibifu wa jamii kwa halii hii. Hapa watoto wanajifunza nini kwa kweli?
MWANA FA AITAKA SERIKALI IRUDISHE MFUMO WA ANALOGIA
Rapper
Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ambaye March 13 mwaka huu alisherehekea
siku yake ya kuzaliwa, ameiomba serikali kuwafikiria mara mbili mbili
wasanii na kuachia mifumo yote miwili ya digitali na analojia kwakuwa
mfumo wa digitali unawaumiza.
Akiongea
na gazeti la Habari Leo, FA amesema kwa sasa wasanii nchini wanaumizwa
na mfumo wa digitali kwakuwa wamekuwa wakitumia fedha nyingi katika
kutengeneza video, lakini zinaishia kutazamwa na watu wachache tu wenye
ving’amuzi.
“Waachie mifumo yote kwani kila mtu atakuwa na uamuzi wa kufanya, kutokana na ubora wa kazi,” alisema Mwana FA.
Alisisitiza
kuwa huenda akasubiri hata miezi miwili na zaidi, kama serikali
itakubali kuachia mifumo yote miwili wa digitali na analojia, na kama
hawatotaka, basi ataachia hivyo hivyo kwa kuwa hawezi kukaa nayo ndani.
CHECK OUT ALICHOKISEMA LULU KUHUSU MAREHEMU STEVEN CHARLES KANUMBA.
Leo kutoka akaunti ya Twitter ya msanii wa filamu(Boongomovie) amefunguka na
juu ya aliyekuwa mpenzi wake marehemu Steven Charles Kanumba ambae kifo cha
mraehemu kilichosababisha yeye kuingia gerezani
sasa hiki ndicho alicho kiandika kupitia ukurasa wake huo wa mtandao wa
kijamiaa Twitter
MASTAA WAANDAA MKESHA KUMUOMBEA KAJALA
Stori: Sifael Paul ZIkiwa zimebaki siku 8 tu kabla ya hukumu ya staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja kusomwa Machi 25, mwaka huu, inasemekana kuwa baadhi ya mastaa wa filamu na muziki Bongo, wameandaa mkesha wa kumuombea ili hukumu hiyo iende vizuri na aachiwe huru arudi uraiani. |
Kajala anakabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu kwa kuuza
nyumba iliyokuwa imewekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru), kwa kushirikiana na mumewe, Faraji Agustino. Kwa mujibu wa mwigizaji mmoja maarufu wa kiume, tayari ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na ujumbe kupitia mitandao ya kijamii umeanza kusambazwa kwa baadhi ya mastaa hao ambao kila mmoja anaonesha kuwa tayari kwa ishu hiyo ya kumuomba Mungu amsaidie Kajala. |
“Mwanzoni ilikuwa ni kuhamasishana tu kumkumbuka Kajala katika sala zetu za kila siku kama ilivyokuwa kwa Lulu (Elizabeth Michael), lakini sasa tumeona ni vema tukakutana kwa pamoja tumlilie Mungu ili hukumu yake imuendee vizuri,” alisema mwigizaji huyo na kuongeza: |
Katika kesi hiyo iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Kajala amesota Segerea kwa takribani mwaka mmoja ambapo sasa hatma yake itajulikana tarehe tajwa hapo juu. |
CHUCHU HANS: NIMEANZA KUIGIZA TANGU NIKIWA MDOGO
Tangu
akiwa mdogo alikuwa anaigiza na kufanya umiss wakati alipokuwa shuleni
mkoani Tanga. Chuchu who has acted in many films including Lose
Control, Hit Back and Tone la Damu.
Mshindi
huyo wa taji la Miss Tanzania talent in 2005.Kiukweli mimi toka
utotoni nilikuwa na kipaji cha u-miss na kuigiza nimeanza tangia shule
Tanga nilikuwa naigiza maigizo na nafanya fashion shows so naamini
nilikuwa na talent that's y nilivyoingia miss Tanzania pia niliweza
kutwaa taji la Miss Tanzania Talent Tanzania 2005" . Some of her
upcoming films include Mimba by Chekibud, Safari produced by Rich and
her own film Raula.
US Hip Hop Rapper Lil Wayne is Recovering After Seizures.
The hip hop star tweets that he is “good” after suffering a reported seizure that led to claims he was in a coma and near death.
Grammy-winning
hip hop star Lil Wayne has said he is recovering and has thanked fans
for their concern after he suffered a reported seizure.
One
of the Celebrity news website claimed the star was in critical
condition in Los Angeles after being admitted to hospital twice this
week.
In a message from his official Twitter account Lil Wayne said: “I’m good everybody. Thx for the prayers and love.”
The
30-year-old rapper, who has a history of seizures, was first rushed to
Cedars Sinai hospital on Tuesday after suffering multiple episodes, it
said.
He left the following day but was re-admitted hours later.
His
spokeswoman Sarah Cunningham said in an email that “Lil Wayne is
recovering,” but did not specify what he was suffering from.
In
October last year, the star, who won four Grammy awards in 2008
including best rap song and best rap album, reportedly suffered a number
of seizures while on his private jet.
Wazimbabwe wanapiga kura ya maoni leo huku wanachama wa upinzani wakidaiwa kushambuliwa.
Wananchi
wa Zimbabwe leo wanapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo
itaweka kikomo cha muhula wa urais na kuongeza uhuru wa vyombo vya
habari.
Hata hivyo, wasiwasi
umeongezeka baada ya wanachama kadhaa wa chama cha upinzani cha Waziri
Mkuu Morgan Tsvangirai kushambuliwa wakati wakifanya kampeni katika
kitongoji cha Mbare kwenye mji mkuu Harare, hapo jana.
Msemaji wa chama hicho
cha Movement for Democratic Change-MDC, Douglas Mwonzora, amewashutumu
wafuasi wa Rais Robert Mugabe kuhusika na tukio hilo.
Katiba hiyo mpya itadhibiti mamlaka ya Rais Mugabe na kuweka misingi ya kufanyika kwa uchaguzi mwezi Julai, mwaka huu.
Uchaguzi huo
utahitimisha makubaliano yaliyokumbwa na matatizo ya kugawana madaraka
kati ya Rais Mugabe na Waziri Mkuu Tsvangirai.-DW.
MNYIKA::Tutaandamana kudai maji
MBUNGE wa Ubungo
John Mnyika leo ataongoza maandamano ya amani kwenda Wizara ya Maji
kupata majibu kuhusu matatizo ya maji, licha ya kuzuiwa na Jeshi la
Polisi.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, ACP
Charles Kenyela amekataza maandamano na mkutano huo kwa madai kuwa eneo
la Manzese Bakhresa walilopanga kufanyia mkutano ni maegesho ya magari ya mizigo.
Akizungumza kwa niaba ya Mnyika, mratibu
wa maandamano hayo kutoka ofisi ya mbunge, Gaston Garubindi, alisema
kuwa maandalizi yamekamilika na mbunge huyo ataongoza kama
ilivyopangwa.
Garubindi alisema kuwa Kenyela
amewadanganya wananchi kwa kueleza kuwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne
Maghembe hakuwa na taarifa wakati ofisi ya mbunge ilimwandikia barua
yenye kumbukumbu namba OMU/MJ/001/2013 na nakala nyingine kupelekwa kwa
viongozi wengine wa wizara hiyo.
RAFIKI WA RAILA ODINGA AMPA TALAKA MKEWE KWA KUMSIFIA UHURU KENYATTA KUWA NI HANDSOME
Rafiki
wa karibu wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga Jumatatu hii anadaiwa
kumpa talaka mke wake baada ya kumsifia Rais mteule wa Kenya Uhuru
Kenyatta ni ‘handsome’ mbele yake.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa
Kenya, mwanasiasa huyo wa chama cha CORD anayetokea magharibi mwa Kenya,
alikuwa akitazama taarifa ya habari akiwa na mke wake na ndipo
alipoonekena Uhuru Kenyatta kwenye TV akizungumza na wawakilishi wa nchi
mbalimbali nyumbani wake.
Baada ya kumuona mke huyo ambaye
ana miaka 30 na kitu alisikika akisema kwa sauti ya chini kuwa anapenda
muonekano wa Uhuru Kenyatta.
Hata kabla hajamaliza neno
Kenyatta, inadaiwa kuwa mwanaume huyo aliye na ukaribu na Raila Odinga,
alimpa kichapo cha haja na kumfukuza nyumbani usiku huo.
Simba hapatoshi leo,mkutano wa wanachama wake wapigwa stop.!
WAKATI
wanachama takribani 700 wanatarajia kufanya mkutano wa dharura leo
Mnazi Mmoja, uongozi wa klabu hiyo umepiga stop kumkutano huo kwa madai
kuwa wanachama hao hawana haki ya kuitisha mkutano wakati tayari
uongozi ulishatoa tamko la kufanya mkutano huo wa dharura wakati wowote
kuanzia sasa.
Uongozi huo wa Simba kupitia kwa ofisa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga ulisema kuwa mkutano utakaofanyika leo ni batili kwa kuwa hauna baraka za uongozi na kuwataka wanachama wa Simba kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho mwenyekiti wao Ismail Aden Rage akiwa India kwenye matibabu na anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki ijao.
Kauli hiyo ya uongozi imekuja ikiwa leo wanachama hao wakitarajia kufanya mkutano wao kwa mujibu wa katiba yao ibara ya 22 ambayo inatamka wazi wanachama wasiopungua 500 wana haki ya kuandaa mkutnao mkuu kama mwenyekiti hayupo tayari kuitisha mkutano ndani ya siku 30.
Hata hivyo jana Kamwaga alisema "Mwezi uliopita mwenyekiti alitangaza kuitisha mkutano wa dharura siku yoyote ajenda ingekuwa moja tu kujadili mwenendo wa klabu bahati mbaya alishikwa maradhi ikabidi aende India kutibiwa, kuna uwezekano mkubwa akarejea wiki ijayo.
"Uongozi umeridhia kufanyika kwa Mkutano wa wanachama. Kimsingi, kama uongozi umeridhia, hakuna mwanachama mwingine anayeweza kuitisha mkutano mkuu mwingine, hao wanaoitisha mkutano wana nguvu gani ya kisheria kufanya hivyo? Walichaguliwa na nani kuwakilisha wanachama? Lini na wapi?" alihoji Kamwaga.
"Uongozi unaweza kuitisha mkutano kwa vile wenyewe ndiyo wenye leja ya wanachama, Klabu ina database yake ya kompyuta inayotambua wanachama walio hai na wasio hai, hakuna mtu mwingine yeyote, aliye nje ya uongozi huu anayefahamu wanachama walio hai na wasio hai hao wanachama wanaoitana kufanya mkutano, wamehakikiwa na nani kubaini uhalali wao huo?"
Alisema wanachama wanaolazimisha kufanyika kwa mkutano wana ajenda binafsi na si za maslahi ya klabu, Kama kweli wangekuwa na nia njema na klabu wangesubiri mkutano ambao utaitishwa punde na kwamba mkutano huo wa leo una lengo la kuleta vurugu na mifarakano ndani ya klabu yao.
" Michezo ni amani na furaha na michezo si vurugu, uongozi wa Simba umetoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na ubatili wa mkutano huo, tunapenda kuwaomba wanachama wetu wasiopenda fujo na vurugu kwenye michezo kukaa mbali na mkutano huo kwa vile vyombo vya dola vitaufuatilia.
"Uongozi hautajiingiza katika kutoa dhamana au msaada wa namna yoyote kwa yeyote ambaye atachukuliwa hatua na vyombo vya dola kutokana na kujihusisha na mkutano huo."alisisitiza Kamwaga.
Hata hivyo pamoja na kauli hiyo ya Kamwaga wanachama wa Simba kupitia kwa mmoja wa waratibu wa mkutano huo Mohamed Wandi wamesisitiza kufanyika kwa mkutano huo ambao utakuwa na ajenda mbili moja ikiwa ni mwenendo wa timu yao katika mashindano pamoja na kutokuwa na imani na uongozi wa Rage.
Watu wanne wafikishwa mahakamani wakituhumiwa kumuua kwa maksudi John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe..
BREAKING NEWZZZZZ .... Jeshi la Polisi Lapiga Marufuku Maandamano ya Chadema Leo, Latoa Sababu Za Kupiga Marufuku Maandamano
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela
---
Jeshi
la Polisi mkoani Dar es Salaam kanda ya Kinondoni limekataza
maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika tarehe 16 Machi 2013
yaliyokuwa yameiratibiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika yaliyolenga
kufika katika Wizara ya Maji ili kufikisha ujumbe kwa Waziri wa Maji,
Prof Maghembe kuhusu kero ya maji katika jimbo hilo ambayo
haijatatuliwa wala kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu. Kamanda wa Polisi
wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela amesema endapo maandamano hayo
yatafanyika:
1. Upo wasiwasi wa kutokea kwa vurugu pale watakaposhindwa kufikia muafaka kuhusu hoja zao.
2. Amewasiliana na Ofisi ya Waziri husika na kufahamishwa kuwa haina taarifa rasmi za ujio wa maandamano hayo.
3. Barabara yatakakopita maandamano hayo ipo katika ujenzi na hivyo maandamano hayo yatazuia shughuli za mkandarasi kukamilisha kazi yake kwa wakati na kuisababishia Serikali hasara.
Credits: Lukaza Blog
Subscribe to:
Posts (Atom)