Saturday, March 09, 2013

ODINGA: KAMWE HATUWEZI YATAMBUA MATOKEO YA URAIS KENYA

Aliyekuwa Mgombea Urais nchini Kenya kwa tiketi ya ODM, Raila Odinga na Waziri Mkuu wa Zamani wa Serikali ya Mwai Kibaki amesema hayatambui matokeo na Ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Odinga amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari na halaiki na kushusha lawama zake kwa tume Huru ya uchaguzi ya IEBC kuwa imerudia madudu ya mwaka 2007 ambayo yaliingiza nchi katika vurugu kubwa.

“Kamwe hatuwezi kuyatambua matokeo hayo yaliyotangazwa hivi punde, hivyo tumeamua kwenda Mahakamani kudai haki ya wakenya Walio wengi kisheria”.

WEMA SEPETU APATA AJALI, amgonga mtembea kwa miguu

 Gari la wema likiondoka maeneo ya ajli hiyo
Wema Sepetu amepata ajali mbaya baada ya gari ambalo alikuwa akiliendesha aina ya Audi Q7 kuacha njia na kugonga gari lingine kisha kumgonga mtembea kwa miguu.
Tukio hilo ambalo lilivuta umati wa watu lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Makumbusho, jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa Wema alikuwa katika mwendo wa kasi na kushindwa kulimudu gari hilo barabarani.
Ajali hiyo ilisababisha foleni na baadhi ya vijana wanaosadikiwa ni vibaka kuanza kumzingira.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyeomba hifadhi ya jina, inawezekana alikuwa na mawazo mengi kichwani kwani licha ya kuwa kwenye mwendo wa kasi, hakukuwa na sababu ya wazi iliyosababisha aache barabara.
Boneti la gari hilo likiwa limeumia baada ya ajali hiyo
“Yaani mi nahisi alikuwa na mawazo mengi au alikuwa ‘amepata’ kidogo,” alisema shuhuda huyo aliyedai aliona mchezo mzima.
Baada ya kugonga, ilidaiwa kuwa mwigizaji huyo alishuka kwenye gari na kutaka kumpiga
vibao mtembea kwa miguu huyo lakini ghafla watu waliingilia kati na kumzuia huku wakimuonya kuwa akithubutu wangemshushia kichapo.
“Huyu dada vipi? Ajali amesababisha yeye halafu anataka kumpiga mtembea kwa miguu, angejaribu tu tungemvua nguo hapahapa,” alisema shuhuda mmoja aliyekataa kuchorwa jina lake gazetini.
Paparazi wetu alipotonywa na kufika eneo la tukio,  alilishuhudia gari la mwigizaji huyo likiwa limebondeka kwa mbele huku akiliendesha kulipeleka katika gereji iliyokuwa karibu na eneo hilo.
Hata hivyo, Wema alipomuona paparazi akiwa na vitendea kazi vyake  akimfuatilia kwenye gereji hiyo, aliondoa gari lake haraka ambapo umati uliokuwa ukifuatilia kwa makini tukio hilo ulimzomea. Haikufahamika alilipeleka wapi.    
credit-globalpublishers

MASTAA WA FILAMU RAY,JB,UWOYA,NA KING MAJUTO WANATARAJIWA KUTUA KIGALI RWANDA KWA MUALIKO MAALUMU

Mwenyekiti wa bongo movie Vicent kigosi (Ray) katika pozi 

Wale mastaa wa filamu nnchini tanzania Vicent kigosi Ray,Jacob Stephan Jb,Irene uwoya,na yule king wa vichekesho nchini King Majuto kwa pamoja wanatarajiwa kutua nchini rwanda kwa mualiko rasmi uliowataka kwenda nchini humo.

Wasanii hao wamepata mualiko huo kutokana na nchi hiyo kuzikubali sana kazi za wasanii watanzania na kuona njia pekee ni kuwaita kwaajili ya kuwapa nguvu wasanii wao,Akizungumza na thesuperstarstz huko kigali kwa njia ya simu Ndwimana Ngikonwa ambaye ni mmoja wa mapromota wa nchi hiyo amesema yeye anawafahamu sana wasanii hao na amefurahishwa sana na ujio wao kwani itasaidia kuleta changamoto kwa wasanii wao.

King Majuto atakuwepo 

Jacob stephan Jb atakuwepo pia 
Promota huyo ambaye inasemekana alishawahi kuwachukua wanamuziki kibao toka bongo kwenda kupiga shoo huko kigali anaendelea kusema kuwa kama wasanii hao watakubaliana nae atawapa dili jingine mara baada yakumaliza kazi iliyowapeleka, Tulipomuuliza kama anahusika na safari hiyo alikana nakusema hapana ila anajua mchongo wote na kuendelea kusema kuwa hakujiingiza kwenye inshu hiyo kwani imekaa ki serekali zaidi bila kufafanua maana yake.

Uwoya na Jb katka pozi wakati wakirekodi filamu
The superstarstz ilipomalizana na promota huyo ilimuendea hewani Jb kama mmoja wasanii waliotajwa katika safari hiyo kutaka kujua ukweli wa habari hizi na alipopatikana alisema,Ni kweli kaka tunasafari ya huko ila mengi mpigie Ray kwasababu yeye ni mwenyekiti wa bongo movie atakueleza mengi zaidi kama kiongozi wetu

The superstarstz ilitaka kujua kama safari yenyewe ni kweli inahusu mwaliko wa serekali ambapo Jb alijibu kwa kifupi yote mtajulishwa na ray,

Ray na Uwoya katika picha za filamu ya PRETTY GIRL 
Tulipomalizana na jb moja kwa moja thesuperstarstz ilimuendea hewani msanii Vicent kigosi ambae ni mwenyekiti wa bongo movie kwa sasa na kumuuliza kama yeye na vijana wake wana safari ya kigali nchini Rwanda. Nae kama jb alikiri kuwana na safari hiyo na hapo ndipo thesuperstars ilipotaka kujua kinachowapeleka rwanda ambapo ray alisema Ni safari ya kawaida kaka unajua kwa sasa tunamshukuru mungu sana kwani imefika hatua nchi jiran wanaamini sisi tunaweza kuwa chachu ya wasanii wao kufanya vizuri katika filamu na hili limefanya tuitwe huko.

Tulipotaka kujua kama safari hii inahusisha serekali ray alicheka na kusema Unajua wenzetu ni tofauti na sisi wao kila kitu kinaenda kisheria huwezi kufanya jambo mpaka chama kijue na kikishajua ni serekali japo sisi kama sisi tutakutana viongozi mbali mbali wa nchi hiyo kwa sababu nnchi nzima ya rwanda imeshajua na imejiandaa kwa ajili yetu na imeandaa mapokezi makubwa sana wanasema wanataka yavunje yazidi yale ya congo niliyoyafanya nikiwa na swahiba marehemu steven kanumba.

Uwoya katika pozi
Ray alipoulizwa wataondoka lini kuelekea huko amesema kesho nitakupa jibu kaka maana mambo yote yapo poa ila elewa muda wowote kuanzia leo tutaondoka Nae kiongozi wa msafara amesema kuwa katika ziara hiyo wasanii hao wanatarajia kukutana na mheshimiwa rais na kumuelezea kiundani wigo wa sanaa na nini kifanyike kuinua sanaa ya rwanda Ray amewataja wasani atakao ongozana nao kuwa ni pamoja na Irene uwoya ,,Jacob Stephen Jb, na Mzee King Majuto the superstarstz inawatakia kila la kheri na kuwaomba waitangaze tanzania kila dakika watakayopata nafasi hiyo

UWOYA USO KWA USO NA NDIKUMANA LEO NCHINI RWANDA

Irene Uwoya

Msanii mwenye tittle bubwa kunako tasnia ya filamu Tanzania Irene Uwoya leo atakutana uso kwa uso na mumewe Ndikumana nchini Rwanda ambapo amepata mualiko maalum wa utoaji tuzo za filamu zilizoandaliwa nchini humo, Katika msafara huo Uwoya maongozana na wasanii wengine kama Mzee Majuto,Jb na Ray.

Uwoya pamoja na kundi hilo watakuwa moja kati ya watoaji wa tuzo hizo kwa washindi watakaotangazwa kama washindi wa Tuzo zinazojulikana kama Rwanda movie Awards, wasanii waliondoka jijini Dar es salaam siku ya jumatano kwa ajili ya utoaji wa tuzo ambazo zimezidi kujichukulia umaarufu Rwanda na Afrika Mashariki.

Wasanii hao wakiwa nchini Rwanda wataonana na mke wa nchi hiyo Paul Kagame mama Jeannette Kagame na kubadilishana mawili matatu kisha kurudi nchini Tanzania, pia kampuni ya Steps Entertainment ambayo ndio wasambazaji wakubwa wa filamu Swahiliwood itapata fursa ya kutangaza filamu zake katika tamasha hilo siku ya utoaji wa tuzo.

Tamasha hilo linafanyika leo tarehe 9. March. 2013.

Ndikumana

Rwanda yaiomba Tanzania kuimarisha Mahusiano.

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akimkaribisha Balozi wa Rwanda hapa nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Ben Rugangazi, wakati Balozi huyo alipomtembelea Spika ofisini kwake Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao, Balozi Rugangazi alimuomba Spika kupitia Bunge nchi mbili hizi zizidi kuimarisha mahusiano mzuri yaliyopo.
 
Spika Makinda alimhakikishia Balozi Rugangazi kulisimamia jambo hilo huku akimweleza kwa muhtasari nia ya mabadiliko ya Bunge ya kuanza mkutano wake wa Bajeti mwezi Aprili badala ya mwezi Juni kama ilivyozoeleka. Mkuu huyo wa mhimili wa Bunge amesema hatua hii itaisaidia serikali kuanza kutumia fedha za mapato na matumizi mara tu mwaka wa fedha wa serikali (Julai Mosi) unapoanza. “Siku ya kusomwa bajeti kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itabakia kuwa ni ile ile ila sisi tutaanza kujadili wizara zote za kisekta isipokuwa wizara ya Fedha hadi mwezi Juni,” alisema Spika na kuongeza.
 
Balozi Rugangazi aliifurahia hatua hiyo huku akisisitiza kuwa Rwanda inayo mengi ya kujifunza kutoka Tanzania. Aidha Balozi huyo alitoa mwaliko na taarifa ya maadhisho ya siku ya ‘Utu wa Binadamu’ ambayo taifa la Rwanda huadhimisha kila tarehe 7 Aprili kwa ajili kuwakumbuka wale wote waliouawa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu takriban milioni moja waliuawa kikatili kufuatia mchafuko baina ya kabila la Wahutu na Watutsi.

MBUNGE WA CHADEMA KORTINI

MBUNGE wa Ukerewe, Salvatory Machemli (CHADEMA) amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka ya uchochezi. 
Machemli (39) amesomewa mashitaka hayo jana mbele ya 
hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya, Rouben Luhasha akidaiwa kutenda kosa hilo mwaka mmoja na nusu uliopita. 

MAKAMPUNI YA SIMU YAUNGANA KUTOA HUDUMA YA MAWASILIANO KWA WOTE

Wawakilishi mbalimbali wa makampuni ya simu wakitiliana saini ya makubaliano ya kuendesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kulia ni Mkuu wa kitengo cha uhimalishaji mitandao wa Voda Com Eng,Nguvu Kamando anaefuata ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Bw, Kamugisha Kazaura na wengine wanaoshudia makubaliano hayo nyuma kushoto ni Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Tekinolojia Profesa Makame Mbawara 

WAWAKILISHI WA MITANDAO

RAIS DK SHEIN AHUDHURIA MAULIDI YA MTUME, TEMEKE JIJINI DAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali
Mohamed Shein,akisalimiana na Sheikh Alhad Mussa Salum,alipowasili
katika msikiti Masjid majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho kuhudhuria
katika maulid ya Mtume Muhamad SAW.
Sheikh,Dk.Usama Mohammed Esmail,kutoka nchini Misri akitoa mawaidha wakati wa Maulid ya Mtume Muhammad SAW,yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho,yaliyohudhuriwa na Viongozi wa Dini mbali mbali,na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Sheikh Alhad Mussa Salum,wa Mkoa wa Dar es
Salaam,akiwatambulisha wageni mbali mbali waliohudhuria katika Maulid
ya Mtume S.A.W. yaliyohudhuriwa na maelfu ya waumini wa Jiji la Dar
es Salaam,katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiwaongoza Viongozi mbali
mbali wa Dini na Serikali katika Maulid ya Mtume Muhammad S.A.W
yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke
mwisho.
Wanamadrasatul Az-har ya Koma Kisiwani Dar es Salaam,wakisoma Qaswida Ya swalatu Alan Nabii,katika Maulid ya Kumswalia Mtume Muhammad SAW,yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wa Jijini Dar es Salaam,waliohudhuria katika Maulid ya Kumswalia Mtume Muhammad SAW,yaliyofanyika jana katika Kumswalia Mtume Muhammad
SAW,yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa
Temeke mwisho.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

MKE WA MTU ATUPIA PICHA YA NUSU UCHI FACEBOOK KWA MADAI KUWA MUMEWE HAYUKO FACEBOOK, HIVYO HAWEZI KUONA

Picha Hii ni Imepostiwa kwenye facebook na Mke wa mtu sasa hapo we can't tell if ni yeye ama la...ila kwa kifupi nimemuuliza why ameweka na haoni itamsababishia matatizo na mumewe akanijibu kwa kifupi kuwa mumewe hayupo Facebook so hawezi kujua ..

WATU WATATU WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUMTUSI SPIKA WA BUNGE

Watu watatu wamefikishwa mahakamani katika mikoa ya Kilimanjaro, Dodoma na Mkoa mpya wa Simiyu kwa tuhuma za kutumia lugha za matusi na uchochezi dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri yak Muungano wa Tanzania.

UHURU KENYATTA AIBUKA MSHINDI WA KITI CHA URAIS NCHINI KENYA

Mchuano  ulikuwa  mkali  kweli  kweli, lakini  hatimaye  Uhuru Kenyatta ameibuka  mshindi wa  kinyang'anyiri  hicho  kwa  asilimia  50.3  ya  kura  zote  zilizopigwa  huku  Raila Odinga  akijipatia  asilimia 43.28  ya  kura zote

UN's Navi Pillay condemns Tanzania attacks on albinos

Salum Khalfani Bar'wani - November 2010  
Salum Khalfani Bar'wani became the first Tanzanian with albinism to be elected an MP in 2010
.
 
The UN human rights chief has condemned a recent spate of "horrific attacks" on people with albinism in Tanzania, including the murder of a young boy. The government should act to stop the "vicious killings" and discrimination they faced, said Navi Pillay. 

The mutilation and murder of people with albinism is often linked to witchcraft, the UN says. Only five people have been convicted in Tanzania since 2000 for killing people with albinism, it adds. Some 72 people have been killed in that time.

In 2009, President Jakaya Kiwete said the murders had brought shame to Tanzania and launched a national campaign to end the persecution of people with albinism.
 
'Arm hacked off'
In 2010, Salum Khalfani Bar'wani became the first person with albinism to be elected as an MP in Tanzania.
 
Navi Pillay UN human rights chief

In a statement, Ms Pillay said four attacks on Tanzanians with albinism had been documented in just 16 days between the end of January and mid-February. They included:
  • the murder of a seven-year-old boy, Lugolola Bunzari, on 31 January at Kanunge village in the Tabora region. His attackers slashed his forehead, right arm and left shoulder, and chopped off his left arm just above the elbow. The boy's grandfather, aged 95, was also killed in the attack as he tried to protect his grandson;
  • a seven-month-old baby, Makunga Baraka, narrowly escaped death on 5 February after armed men attacked his home in the Simiyu region. Villagers chased the attackers away and surrounded the house to protect him. The baby and his mother were taken to the police station the following morning and given temporary sanctuary;
  • a 39-year-old woman Maria Chambanenge was attacked on 11 February by five armed men, allegedly including her husband, in Mkowe village in the Rukwa region. They hacked off her left arm while she was sleeping with two of her four children. The five suspects were subsequently arrested and the victim's arm recovered - their trial is reportedly under way
  • a 10-year-old boy, Mwigulu Matonange, was attacked on his way home from school and his left arm chopped off above the elbow by two unidentified men in Msia village in Rukwa. Three men have been arrested in connection with the attack.
"These crimes are abhorrent. People with albinism have the right to start living, like anyone else, without fear of being killed or dismembered," Ms Pillay said. Tanzania's authorities needed to step up efforts to bring the attackers to justice, she added.

Public awareness campaigns should also be launched to end the stigma associated with albinism, Ms Pillay said. "I am deeply alarmed by the general discrimination and social exclusion many people with albinism suffer, as a result of their skin colour, not just in Tanzania but in other countries as well," she said. Some witchdoctors say that magic charms are more powerful if they contain body parts from people with albinism - this has led to a lucrative criminal trade in these body parts.

Balozi Tuvako Manongi akisaini kitabu cha maombolezo ya Hugo Chavez

 Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, jana  Ijumaa aliungana na  Mabalozi wengine katika kutia saini kitabu cha Maombolezo  kufuatia kifo cha Rais wa Venezuela,  Hugo Chaves, aliyefariki siku  ya jumanne wiki hii kwa ugonjwa wa  kansa. Kitabu hicho  kilifunguliwa katika Ubalozi wa Kudumu wa  Venezuela katika Umoja wa Mataifa.

RAIS KIKWETE NA ABDULRAHAMAN KINAN WAMJULIA HALI MHARIRI MTENDAJI WA HABARI CORPORATION ABSALOM KIBANDA AFRIKA KUSINI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg, Afrika ya Kusini leo jioni. Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...