WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa
matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa
Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato
cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.
Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati
wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule
na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of
Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa
huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za
Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.