WAKATI
Watanzania kwa mamilioni wakiendelea kukosa huduma mbalimbali muhimu
ikiwamo afya na njaa kutawala katika maeneo mengi nchini, imebainika
kuwa viongozi wastaafu wanarundikiwa mafao.
Ukubwa wa
mafao hayo na posho kwa marais, makamu wa rais na mawaziri wakuu
wastaafu unatajwa kuwa huenda ndiyo chanzo cha uongozi kupiganiwa kwa
udi na uvumba na kwa gharama yoyote, kutokana na kuwa vyeo hivyo
huwanufaisha katika maisha yao yote na baada ya wao kufariki wategemezi
wao huendelea kunufaika.
Sheria ya
Mafao ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1999, ambayo ilirekebishwa mwaka
2005, inaeleza kuwa Rais Mstaafu anapomaliza kipindi chake cha uongozi,
hupata mafao ya mkupuo.
Ingawa
kiwango cha mshahara wa Rais wa Tanzania ni siri, sheria hiyo inaeleza
kuwa mafao yao hukokotolewa kwa kuzingatia mshahara wa juu aliowahi
kupata miezi aliyofanya kazi.
Kiwango cha
mafao hayo hukokotolewa kwa kutumia kanuni za kiwango cha asilimia
itakayopangwa na mamlaka husika.
Mbali ya
mafao yake ya kazi, Rais Mstaafu hulipwa posho ya kila mwezi kiasi cha
asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani. Kiasi hicho ni sawa
na Sh80 kwa kila Sh100 anayopata Rais aliye madarakani.
Licha ya
posho hiyo, Rais hupewa ulinzi, msaidizi, katibu muhtasi, mhudumu wa
ofisi, mpishi, dobi, mtumishi wa ndani, mtunza bustani, madereva wawili
na gharama za mazishi atakapofariki.
No comments:
Post a Comment